TAMISEMI: AJIRA 6,000 bado, Achaneni na Matapeli

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
DODOMA : AJIRA 6,000 bado, Achaneni na Matapeli

Atley Kuni na Veronica Simba- TAMISEMI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ametegua kitendawili kuhusu ajira elfu sita za watumishi wa kada ya walimu kama ilivyoamriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwamba waajiriwe walimu ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada hiyo hasa kwakuzingatia waliostaafu na walioacha kazi kwa sababu mbalimbali.

Akizungumza leo Aprili 23, 2021 jijini Dodoma, wakati wa ziara yake ya kwanza katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), ambayo ni moja ya taasisi inayosimamiwa na Ofisi yake, Prof. Shemdoe amesema, utaratibu wa kuajiri utafuata Sheria, Taratibu na Kanuni, huku akionya wale wote walioanza kutumia matapeli kusaka ajira waache mchezo huo mara moja.

Prof. Shemdoe amesema tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipo ielekeza Ofisi hiyo kufanya mchakato wa kuajiri walimu 6,000 ili kufidia baadhi ya watumishi hao kwa sababu mbali mbali, kumezuka wimbi la matapeli na wengine kuwadanganya watu wanaoomba ajira kwamba watawasaidia kupata ajira hizo.

“Nimepata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa, wapo baadhi ya watu kwa nia ovu wamekuwa wakiwatapeli kwa kuwaomba fedha baadhi ya walimu wanaotaka kuomba ajira na kuwataka watoe pesa ili zifikishwe Wizarani kwa ajili ya kuwapatia ajira, nipende kusema wazi kwamba jambo hili halipo,” amesema Prof. Shemdoe.

Prof. Shemdoe na kuongeza kwamba, vishoka wote watakaobainika kutekeleza utapeli huo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola, huku akiwataka wale wote watakaokumbana na adha hiyo kutosita kutoa taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika chombo hicho kinachoangalia nidhamu ya watumishi walimu, Katibu Mkuu, Shemdoe amewataka watumishi wa ofisi hiyo kutoa ushirikiano kwa Katibu Mtendaji aliyeteuliwa na Kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kushika wadhifa wa Ofisi hiyo.
 
Bado watu watapigwa tu. Maana hali mtaani ni tete. Ajira zenyewe ni elfu 6 tu! Halafu waombaji labda ni elfu 40!! Unategemea nini!
 
Nimeona taarifa ya tamisemi kutatua kitndawili cha vishoka katika ajira mbona watu wanapigwa tuu

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ametegua kitendawili kuhusu ajira elfu sita za watumishi wa kada ya walimu kama ilivyoamriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwamba waajiriwe walimu ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada hiyo hasa kwakuzingatia waliostaafu na walioacha kazi kwa sababu mbalimbali.

Akizungumza leo Aprili 23, 2021 jijini Dodoma, wakati wa ziara yake ya kwanza katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), ambayo ni moja ya taasisi inayosimamiwa na Ofisi yake, Prof. Shemdoe amesema, utaratibu wa kuajiri utafuata Sheria, Taratibu na Kanuni, huku akionya wale wote walioanza kutumia matapeli kusaka ajira waache mchezo huo mara moja.

Prof. Shemdoe amesema tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipo ielekeza Ofisi hiyo kufanya mchakato wa kuajiri walimu 6,000 ili kufidia baadhi ya watumishi hao kwa sababu mbali mbali, kumezuka wimbi la matapeli na wengine kuwadanganya watu wanaoomba ajira kwamba watawasaidia kupata ajira hizo.

“Nimepata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa, wapo baadhi ya watu kwa nia ovu wamekuwa wakiwatapeli kwa kuwaomba fedha baadhi ya walimu wanaotaka kuomba ajira na kuwataka watoe pesa ili zifikishwe Wizarani kwa ajili ya kuwapatia ajira, nipende kusema wazi kwamba jambo hili halipo,” amesema Prof. Shemdoe.

Prof. Shemdoe ameongeza kwamba, vishoka wote watakaobainika kutekeleza utapeli huo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vymbo vya dola, huku akiwataka wale wote watakaokumbana na adha hiyo kutosita kutoa taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika chombo hicho kinachoangalia nidhamu ya watumishi walimu, Katibu Mkuu, Shemdoe amewataka watumishi wa ofisi hiyo kutoa ushirikiano kwa Katibu Mtendaji aliyeteuliwa na Kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kushika wadhifa wa Ofisi hiyo.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, alisema Tume hiyo inafanya kazi vizuri na imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mashauri ya kero mbali mbali za walimu zinasikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati.

“Ndugu Katibu Mkuu, Tume hii pamoja na kuhudumia idadi ya watumishi walimu wanaofikia asilimia 51 ya watumishi wote wa umma bado wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mashauri yanayofikishwa yanatatuliwa kwa wakati. Aidha miongoni mwa mambo ambayo tulikubaliana katika mwaka wa fedha 2020/21, wameweza kufikia malengo kwa asilimia 90, amesema Mweli.

Awali akimkaribisha kuongea na watumishi hao, Katibu Mtendaji wa TSC Bibi Paulina Nkwama, alisema wamefarijika sana kuona wamekuwa miongoni mwa taasisi za mwanzo kabisa za Wizara hiyo kutembelewa ili kujua utendaji wao.

“Ndugu Katibu Mkuu, sisi kwanza tumefarijika sana na ujio wako, ukiangalia una takriban ni majuma mawili toka, Mhe. Rais akuteue na kukuapisha kushika wadhifa wa Katibu Mkuu, TAMISEMI, lakini kwa kuthamini, mchango wa kada ya walimu, umeona ziara yako ya kwanza ujielekeze kwenye Ofisi ya Tume ambayo ndiyo yenye kushughulikia mambo mbalimbali ya walimu,” amesema Bibi Paulina.

Tume ya Utumishi wa Walimu ndiyo chombo kinachoratibu na kushughulikia masuala yote ya walimu, ikiwepo kero na malalamiko ya kada hiyo.
 
Back
Top Bottom