Tambua mambo sita ya ajabu kutoka kwa jamii ya Aghori nchini India

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,085
Habarini za Alhamisi natumaini mpo vizuri sana, poleni kwa wale wagonjwa Mungu awape afya njema. kama ilivyo kawaida yangu ya kuwaletea makala za kutambua mambo mbalimbali kuhusu jamii kadhaa hapa duniani. kuanzia utamaduni wao, mila pamoja na namna ya maisha yao kwa ujumla.

Leo nitakuja kuelezea mambo sita kutoka katika jamii ya watu wa Aghori. Karibuni sana.

Aghori ni jamii ndogo inayopatikana India Pamoja na maeneo jirani kidogo na India. Ni wafuasi wa Dini pamoja na Imani ya Shiva Sadhus ndani ya Wahindu ila ni tofauti sana na Wahindu Waorthodox kwani hawa wana namna tofauti ya kuabudu pamoja na kusihi maisha yao. Imani yao imesimamia kwenye misingi ya ascetic yaani kuwa na nidhamu kali pamoja na kujiepusha na kila aina ya ulafi.

Wengi wa walimu wa imani ya Aghori wanaamrisha heshima kubwa kutoka kwa watu wa vijijini, kwa kuwa wanastahili kuwa na nguvu za uponyaji zilizopatikana kupitia ibada zao za kiasili.

Kutokana na Walimu wa Dini ya Kihindu hudai Neno Aghori linatokana na moja ya sura tano za Shiva zilijulikana kama Aghor. Neno hilo ni la zamani kama Shiva mwenyewe. Katika hadithi za SHIVA PURANA, moja ya hadithi kongwe za Uhindi, kuna wimbo wa utukufu wa Shiva na Pushpadanta, mkuu wa Gandharvas, anayeitwa Shiva Mahimnah Stotram.
Nalo mstari mmoja husema hivi:

"Jina moja la Aghor (Shiva, au yule ambaye amepata jimbo la Aghor) ni kuu ambalo liko juu ya maneno mengine yote. Hakuna kitu cha juu kujulikana kuliko asili halisi ya Shiva."

Hapo mwanzo neno "Aghor" lilimaanisha kitu cha ajabu lakini taratibu lilianza kuchukua sura tofauti kwan lilianza kuingiza matendo ya kutisha sana. Baada ya uhusiano mkubwa katika ya jamii hii ya Aghori pamoja na Lord Shiva ambaye ndo alikuwa kiini kikuu cha Wahindu kwa kuwafundisha mambo mengi, elimu pamoja na ujuzi mbalimbali.

kinaramji.jpg

Katika karne ya 16 mtawa anayeitwa aliyejulikana kidini kama Aghoreshwar, huyu jamaa inasemekana alizunguka sana na kutafuta hekima mpaka alipokutana na Darshan kutoka Bhagwan Dattatreya, ambaye alimtokea akiwa katika milima ya Girnar, sehemu takatifu kwenye mji wa Gujarat. Huyu ndo aliyewapa Aghori elimu yenye hekima mwanzoni kabsa.

Kuna historia ndefu sana ila nitajaribu kuelezea wakati ya maswali na masahihisho ya hoja mbalimbali.
Haya ni mambo sita ya ajabu kuhusu jamii hii ya Aghori:

6. Wanatumia majivu ya marehemu kama namna ya kujikinga na magonjwa pamoja na kujikinga na kifo.

index.jpg

Jamii hii inaamini kuwa ili waweze kuibadilisha miili yao ya kidunia kwenda katika hali ya kiroho basi hawana budi kujipaka majivu ya maheremu waliokwisha kuchomwa moto au Cremation. Aghori wanaamini kuwa ipo siku lazma watakufa na kuoza na kwa sababu hii nchini India hawa jamaa wanajulikana kwa kukusanya majivu ya maiti kutoka mahali pakuchomea miili hiyo. Na kisha hujipaka mwili mzma kuanzia kichwani mpaka miguuni.
Inatisha eehh.

Lakini pia kwa kufanya hivi wanaamini huwafanya wawe karibu zaidi na mungu wao Shiva, na wanaweza kupata ulinzi na kinga katika magonjwa mbalimbali.

5. Je wajua kuwa makazi ya hawa jamaa ni maeneo ya makaburini pamoja na sehemu za kuchoma maiti? Ndio hawa jamaa wanaweka kambi has hasa kwenye makaburi ya zamani & kitambo sana pamoja na maeneo ya kuchomea maiti. Ijapokuwa watu wengi hudai kuwa Waaghori wana faida kwani hupunguza miili ndani ya makaburi hayo na hivyo kupelekea ardhi kuwa na nafasi kubwa yakuweka miili mingine. kauli ambayo imepingwa vikali na jamii kama za Wakristo pamoja na Waislamu kuwa waheshimu kifo pamoja na shughuli za maziko kwa ujumla. Ila sasa katika matambiko yao hutumia mpaka maiti za binadamu.

indexuu.jpg

4. Aghori humuambudu Shiva al maarufu kama Shiva the destroyer.
Najua kuwa mpaka sasa kuna watu wanajiuliza kuwa kwanini haswa hawa jamaa wanafanya vitu hivi.Lakini jibu ni kuwa Shiva the destoryer ndo sababu husika. kwani kila dini au imani inaamini kuwa kujitolea kuelewa imani ya upande fulani upelekea kufanya mambo ya ajabu au sahihi. Shiva anayeabudiwa kapewa majina mengi sana mfano: Kwa Waaghora wamempa majina kama Shiva wa kushangaza, au Shiva muangamizaji. Ijapokuwa Aghori ni sehemu ya Wahindu lakini Wahindu wengine humuona Shiva tofauti na Aghora, hii ni kutokana na mapokeo na tafsiri mbalimbali za maandiko yao. Ijapokuwa imani zingine humuona Shiva tofauti sana na Waaghori.

Namna Waaghori humuona Shiva

Picha tofauti ya Shiva

Picha tofauti na ile ya Waaghori

3. Je wajua Waaghori hufanya tafakari ya kiroho wakiwa na maiti?
Ndio inashangaza sana lakini ndo hali halisi, hawa jamaa wanafanya tafakari (tafsiri sio rasmi) meditation wakiwa na maiti.

Kama moja ya tamaduni ya imani ya Wahindu ya kufanya meditation ya ufanyaji wa takafari hii kama shabaha yao kuu ya kufikia ufahamu mkuu wa kiroho. lakini kwa Aghori ni tofauti kidogo kwani wao mpaka maiti huusishwa kabsa. Tamaduni ya Aghori husimamia kuwa asili yao kubwa ni kutokuogopa kifo hivyo hufanta mediation aidha wakiwa pembeni ya maiti au juu ya maiti. Wanaamini kuwa kwa kufanya hivi huwasaidia kukishinda kifo na kukiepuka kwa namna ya kipekee.

Kwa video ingia hapa https://www.google.com/url?sa=i&rct=j&q=&esrc=s&source=images&cd=&cad=rja&uact=8&ved=0ahUKEwjYjpW8hpbkAhWuQRUIHUNhCDAQMwhWKAQwBA&url=https://www.youtube.com/watch?v=41TREI_MCF8&psig=AOvVaw05RkfpsKfemvUQ6oFAMDth&ust=1566548609326147&ictx=3&uact=3
Picha zilizopo zinaweza kumkera mtu hivyo sidhani kama ni vyema sana kuziweka.
main-qimg-ed9817e166459bf48de6d3f152ad68d1.jpg

2. Wana imani a kuwa kupitia matambiko yao wanaweza kutibu magonjwa mbalimbali.
Aghori ina waganga ambao kiukweli ni kati ya waganga wa ajabu sana duniani.
Waaghori hutumia mwili kama kiungo kikubwa sana katika matambiko yao, hawa hutoa mafuta kutoka katika maiti na kuyatumia mafuta haya kutibu watu na wagonjwa mbalimbali, wanaamini kuwa kipindi cha matambiko hayo, ugonjwa wowote ule uwe wa kuambukiza kama Ukimwi, Kansa, au Homa au wa kichawi basi utamtoka mgonjwa husika na kumuingia mganga, ambaye naye atautoa kutoka mwilini mwake kwa dawa zingine. Wanaamini kuwa yote haya ufanyika kumfurahisha Shiva.
Shivaww.jpg

1. Je unajua kuwa Aghori hufanya mapenzi wakati wa ibada na matambiko yao.
Wana imani ya kuwa kufanya mapenzi wakiwa miongoni wa Maiti huwapatia ngivu za kipekee sana. Wanaume hupakwa majivu ya maiti zilizochomwa kuanzia dhakari mpaka makalioni na hufanya mapenzi wakiwa kwenye majivu hku wamezungukwa na maiti hizo. Ngoma hupigwa huku maneno ya ajabu yakitajwa, lakini kikubwa ni kuwa mwanamke ni lazima awe period wakati wa ufanyikaji wa tendo hili. yaani kwa lugha nyepesi Mwanamke anayefanya ibada hii lazma awe kwenye siku zake, hivyo mwanaume atamuingilia mwanamke akiwa yupo bleed. Damu ya bleed hupakwa kifuani mwa mwanaume na kwenye dhakari kabla ya kuanza tendo.
aaex-10-Jaw-Dropping-Facts-About-Aghoris-600x358.jpg

Bonus: Hawa jamaa wana uwezo wa kuishi maeneo yasiyoweza kukaliwa na binadamu wa kawaida.
Ndio hawa jamaa wanaishi kwenye mazingira ya ajabu sana, ambayo kwa binadamu wa kawaida hawezi kukaa hata kwa siku moj. Mfano: Makaburini???? Ni nani mwenye uwezo wa kupiga kambi makaburii=ni zaidi ya miaka 20 au hata 10 tu. Pia wanasifika kwa kukaa maporini, sehemu zenye baridi na majangwani. Baadhi ya maeneo yao ni kama vile Ravindrapuri huko Varanasi nchini India.
Ukiachilia mbali ishu ya kujipaka majivu mbaya zaidi ni ufanyaji wa mapenzi na maiti.
Yaap hawa ni wa ajabu sana kwani hufanya vitu vya ajabu na maiti kwa kiwango kikubwa, kuanzia kulala nao, kula karibu yao, kufanya mapenzi karibu yao na hata kufanya mapenzi nao.
Wazee kama hawa ndo wenye elimu hii

Mpaka hapo sina cha ziada ila ninaanda makala kubwa na undani zaidi kuhusu hawa jamaa ila mpaka hapa asanteni sana kwa kusomauzi huu.
Karibuni kwa maswali, masahihisho pamoja na hoja zaidi.
 
Asee bora nilizaliwa mtz kwanza wanatisha kwa yale matendo
Young Dee anakuambia Bongo Bahati Mbaya mkuu ila wameniacha hoi kwenye kufanya mapenzi wakati mwanamke yupo period!!!!!!
 
Hawa ni waabudu shetani.
 
Back
Top Bottom