Tamaduni na mila za kufikirika (ajabu) Tanzania na duniani

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,213
"Anayesoma ana mengi sana asiyoyaelewa, asiyesoma hana asichoelewa".

Kama umewahi kusikia kuona au kukutana na mila ambayo kwako ilikuwa ni ya ajabu au haijakukalia sawa lakini ulipoiona au kuikuta ilikuwa ni kitu cha kawaida, itupie uzi huu.

Pia tupia hapa mila ambazo kwako au kwenu ni kawaida kabisa lakini wengine wanazishangaa na kuziona za ajabu au zina walakin.

Binafsi naanza na:
1) Kwetu ni kawaida kabisa mtu kuowana na watoto wa babake mdogo au mkubwa au watoto wa shangazi zake au wa mama zake wakubwa au wadogo au watoto wa wajomba zake.

Hii ni mila ambayo ipo kwetu na inakubalika katika sharia za Kiislam.

Kumbuka; Ni kuowana siyo kufanya uzinzi na uasherati.

Tena mila hiyo tunaisisitiza sana kwetu.
 
Kwetu marufuku kijana wa kiume kutahiriwa hospitalini au kwa ganzi. Ni lazima atahiriwe nyumbani kwa kisu bila dawa ya vidonda au ganzi. Kidonda kinapaswa kipone chenyewe naturally. Na govi linachongwa kwahiyo inakuwa Kama mtu ana uume mbili. Inauma Sana wakuu imagine unakatwa na kisu bila ganzi kwa muda wa dakika 7
 
Yes ni Mila nzuri sana halafu ndoa za hivi huwaga zinadumu sana.
Hilo ni kweli, kwetu walioowana namna hiyo nimewahi kusikia kesi ya moja tu ya kuwachana kati ya nyingi sana, tena ndoa iliyodumu zaidi ya miaka 30.

Waliwachana kwa mambo ya biashara ulioleta wivu na cha kufurahisha zaidi kukawa hakuna uhasama uliodumu, kila mmoja akaishi maisha yake kwa salama na amani ingawa kila mmoja alifunga ndoa nyingine.

Ni kama walishindwa ku "cope" na "midlife crisis".
 
Kama umewahi kusikia kuona au kukutana na mila ambayo kwako ilikuwa ni ya ajabu au haijakukalia sawa lakini ulipoiona au kuikuta ilikuwa ni kitu cha kawaida, itupie uzi huu.

Pia tupia hapa mila ambazo kwako au kwenu ni kawaida kabisa lakini wengine wanazishangaa na kuziona za ajabu au zina walakin.

Binafsi naanza na:
1) Kwetu ni kawaida kabisa mtu kuowana na watoto wa babake mdogo au mkubwa au watoto wa shangazi zake au wa mama zake wakubwa au wadogo au watoto wa wajomba zake.

Hii ni mila ambayo ipo kwetu na inakubalika katika sharia za Kiislam.

Kumbuka; Ni kuowana siyo kufanya uzinzi na uasherati.

Tena mila ihiyo tunaisisitiza sana kwetu.
Mila ya kuto kuhoji na unafundiswa namna ya kuhoji kwa staha, mwizi wa pesa nyingi mwite fisadi na anaundiwa tume hadharani majibu ya tume jee...............yanabaki kwa mwenye tume
 
Hilo ni kweli, kwetu walioowana namna hiyo nimewahi kusikia kesi ya moja tu ya kuwachana kati ya nyingi sana, tena ndoa iliyodumu zaidi ya miaka 30.

Waliwachana kwa mambo ya biashara ulioleta wivu na cha kufurahisha zaidi kukawa hakuna uhasama uliodumu, kila mmoja akaishi maisha yake kwa salama na amani ingawa kila mmoja alifunga ndoa nyingine.

Ni kama walishindwa ku "cope" na "midlife crisis".
Ndo maana mnazaa matahira huko kisutu kisa kuowana ndugu
 
Hilo ni kweli, kwetu walioowana namna hiyo nimewahi kusikia kesi ya moja tu ya kuwachana kati ya nyingi sana, tena ndoa iliyodumu zaidi ya miaka 30.

Waliwachana kwa mambo ya biashara ulioleta wivu na cha kufurahisha zaidi kukawa hakuna uhasama uliodumu, kila mmoja akaishi maisha yake kwa salama na amani ingawa kila mmoja alifunga ndoa nyingine.

Ni kama walishindwa ku "cope" na "midlife crisis".
Hii ya kwako ilotumika mashariki yakati kwa Waarabu na waebrania.

Isaka aliowa ndg yake
Yakobo aliowa binamu zake
 
Maharimu

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur-an na Sunnah. Wanaume wa Kiislamu wameharamishiwa kuwaoa wanawake wanaobainishwa katika aya zifuatazo:

Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; isipokuwa yale yaliyokwishapita. Bila shaka jambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya (kabisa). Mmeharamishiwa (kuoa) mama zenu, watoto wenu, dada zenu, shangazi zenu, ndugu za mama zenu, watoto wa ndugu zenu, watoto wa dada zenu, na mama zenu waliowanyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, walio zaliwa na wake zenu mliowaingilia. Lakini kama nyinyi hamjawaingilia basi si vibaya kwenu (kuwaoa). Na mmeharamishiwa wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharamishiwa) kuwaoa madada wawili wakati mmoja, isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kurehemu na Mwenye kusamehe. (4:22-23)

"Na pia mmeharamishiwa wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairiya hawa..." (4:-24)

Aya hizi zinabainisha wanawake walioharamishwa kuwaoa kuwa ni hawa wafuatao:
1.Mwanamke aliyepata kuolewa na baba yako, (babu yako, baba wa baba yako - wa kuumeni na kikeni).
2.Mama aliyekuzaa (babu aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa...).
3.Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa...). Pia binti wa kunyonya na mwanao (na kikazi chake...).
4.Dada yako khalisa au wa kwa baba au wa kwa mama.
5.Shangazi yako- dada wa baba yako,(na dada wa babu yako...).
6.Mama mdogo; ndugu wa mama yako (au ndugu wa bibi yako...).
7.Binti wa ndugu yako mwanamume, khalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).
8.Binti wa dada yako khalisa au wa kwa baba au kwa mama
9.Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).
1O.Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na aliyekunyonyesha).
11 .Mama yake mkeo wa kumzaa au wa kumnyonyesha (na bibi yake pia wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani mama mdogo wake au shangazi yake wa kuzaliwa au kunyonya; unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.
12.Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake...).
13.Mke aliyeolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chake); si mke wa mtoto wa kupanga au mtoto wa kulea.
14.Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Akifa mke au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake, au shangazi yake, au mama yake mdogo.
15.Mke wa mtu, bado mwenyewe hajafa wala hajamuacha ni Haram kumuoa. Wanawake hao wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni.
 
Ikiwa hivyo basi dunia nzima ni "mataahira". Adam na Eva wa kwenye biblia walizaana vipi?
Kwa wanaoamini. Hao walikuwa na vinasaba vingi. Ndiyo maana wakatoa wazungu, weusi, wachina, wahindi, mbilikimo na kdhalika. Kadri watu wanaofanana wanavyozidi kuzaliana ndivyo vizazi vyao vinavyozidi kuwa dhaifu. Udhaifu mkubwa zaidi hutokea ndugu wanapozaliana. Unawafahamu Harbsburg na Harsburg chins?
 
Back
Top Bottom