Nilikutana nae pande za kinondoni/
Mida ya saba mchana ilisoma saa ya mkononi/
Stendi ya daladala maarufu Kama Morocco/
Me natokea mbagala naenda pande za kinoko/
Ghafla,nikastuka aliponigusa bega/
Kwa gadhabu nilipogeuka ni yeye nikaona shega/
Ila sikuamini nilipomuona/
kama ni Bibi au msichana mdomo haukushona/
Ikanibidi,namkumbuka nilisoma nae shule ya msingi/
Ndugu hawana mpango nae toka alipokufa dingi/
Darasa la Saba na uhakika hakumaliza/
Usawa ulikaba akikumbuka ilimuumiza/
Yamemsibu rafiki ukimwona huwezi kumjua/
Kachakaa hatamaniki hana viatu anapekua/
Dhambi kumpa kisogo hana tiba anapougua/
Shida zake tangu mdogo sasa mtu mzima amekua/
Siku ikipita hajala insha'Allah MOLA anajua/
Wapi usiku atalala ni msala anaomba dua/
Anatamani kufa msalaba apate kuutua/
Kafeli kujiua MUNGU hajapenda kumchukua/
Song:Rafiki
Artist: Stereo