Tamaduni Music Punchlines Special Thread

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Wakuu Umofia kwenu,

Karibuni katika Special Thread ya Tamaduni Music
Hapa tutakua tunatupia Line Kali tulizowahi kuziskia kupitia tracks za members wa Tamaduni

Tamaduni Music members

Nikki mbishi

Stereo

One the incredible

Songa

P the mc

Zaiid

Azma

Ghetto ambassador

Kad go

Dizasta vina

Nash Mc Madina

Phil technic

Man-sulii

Kila mmoja atupie punchline Kali anayoipenda ,ataje msanii na jina la nyimbo husika kama ifuatavyo
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Hamaki ama piga mbiu Kwa washkaji/
Niite Songa Samaki mwenye kiu ndani ya maji/

Songa-Utandarymes
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Haijalishi we ni mkali Zaid ya mentor wako/ na Enter kwako/ kama vile ume sign for trouble/ Nataka nimshukuru duke na M-Lab/ Hapa Nina pozi shughuli ina enter hapo/

One the incredible -Classsic material
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
22,098
2,000
Mi ndo mbaya wakuchana tungo zaki mafia, nafanya laana juu ya dundo la kihasla.../

mbeba lawama maana nina fujo kwa kinasa, amani kwa panorama ndugu na dizasta.../

kwenye vita waliita cheetah mark chui, so ukipita mbele yangu dakika ni majeruhi.../

Sijipi sifa wengi wanaobisha hawanijui, na sijali hawaumizi kichwa hawasumbui.../

Sina promo wala sijajulikana kwa TV, na ninawapa kero wanaojifanya HAWASIKII.../

Ila bongo bwana wasichana wana BIDII, nakia wema sepetu ndo rihanna wa TZ.../

Mi ndo M.A.W.E.N.G.E, kwenye mchezo wa kinasa mi ndo M.V.P.../

Got a flow like mine oh let me SEE, but im sure that you cant be me P.../
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
22,098
2,000
Mi niko ndani we ni mlinzi, ingia kwenye gemu we ni mshindani mi ni mshindi/


Ukiniona sizi usinichukulie kipimbi, wakati kitaani master naheshimika kama dingi/


Mi ni mfanya kazi we ni kazi nakufanya, hazichaniki maana hauna hadhi ya kuchana/


Tahadhari changa rambi rambi na dhamana, yakua ukaishi kwenye kambi za lawama/


Kule siskiki sishawishiki, kusaliti we ni mwanafunzi mi ndo shule ya muziki/


We ni mume mbona mke halidhiki, unajiita mcee na bado uko nje ya msingi/


Mi kibaka we ndo shingo ya kabali, mi ndo driver we ndo konda au tingo kwenye gari/


We kapuku mi na' bingo la mistari, ogelea kote dizasta ndio kingo za bahari/


Mi ndo tungo shazi nazisuka kama jamvi, we ndo pusha zungusha mi ndo mzuka kwenye nyasi/


Najua ku rythms ma mcee wanajua nini, vilio kila masta navyotua kwenye scene/


Nina mama bora,mama nuru,mama funzo, we ni mtumwa kwenye soko niko huru kwenye tungo/


Tukirudi class we ni good mi ni better, mulize kingo kitaani mi ni babuu we ni sheta/


Wauza sura wana ghani tu majina, wao majini kama kabula mi ndo shetani la vina/


Mi nimenuna bwege cheka na hii vocal, beat tope na dizasta mi ndo mega mining volvo


Mi ndo folder, mi ndo hoja, mi ndo mada kwenye somo kwenye jeshi mi ni soldier


Mi ndo muosha naogesha midundo, niite dizasta wananiita profesa tungo
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
22,098
2,000
P the mc wakorea huniita jumong, hasira ndo zinafanya sura kuonekana utong.../

Hatubebwi na tuna move on, kupata au kukosa yote heri men who knows.../

Wasanii chuki kibao, wakilalamika kwamba nawatusi kivyao.../

Sina mkuki wala ngao, ila bado nawasumbua kama musa mbele ya nuksi za farao.../

Hamuelewi mnapoambiwa stay true, mwache jigga mwache fifty hii inamaana stay you.../

Nyie mmekuja kuuza sura tu shameful, na nitazinunua zote hata kama ni bei juu.../
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Napiga punch kama judo/Ma-Rapper Wana simanzi kama nafsi iliyo Kosa mvuto/
Ma fans hawana wasi wala mstuko / Wanajua hata kama akifa Nas songa Yupo/

Toka zama -Songa
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Naacha mashaka kama mauti kwenye roho/ Sikukosi nakusaka kila Chaka nakufata mpaka round about Kariakoo/ Technic knock out sitoi draw/

Sina vina feki vya kichina/ mistari haibebeki kama drake kamuona Sina/ afu Fetty kamauona phina /

Au zillah kaniona Mimi/
Ewe msomi wa shahada jiulize umesoma Nini

Nikki mbishi-Tamaduni
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Ipo njia uliyepagawa na zama hizi/
Nipo pia usijepagawa na Taasisi/
Nauza madawa wananita pharmacist/
M-Lab mzawa hakuna wakuchana kama sisi/

Songa-Toka zama
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
1,702
2,000
Nilikutana nae pande za kinondoni/

Mida ya saba mchana ilisoma saa ya mkononi/

Stendi ya daladala maarufu Kama Morocco/

Me natokea mbagala naenda pande za kinoko/

Ghafla,nikastuka aliponigusa bega/

Kwa gadhabu nilipogeuka ni yeye nikaona shega/

Ila sikuamini nilipomuona/

kama ni Bibi au msichana mdomo haukushona/

Ikanibidi,namkumbuka nilisoma nae shule ya msingi/

Ndugu hawana mpango nae toka alipokufa dingi/

Darasa la Saba na uhakika hakumaliza/

Usawa ulikaba akikumbuka ilimuumiza/

Yamemsibu rafiki ukimwona huwezi kumjua/

Kachakaa hatamaniki hana viatu anapekua/

Dhambi kumpa kisogo hana tiba anapougua/

Shida zake tangu mdogo sasa mtu mzima amekua/

Siku ikipita hajala insha'Allah MOLA anajua/

Wapi usiku atalala ni msala anaomba dua/

Anatamani kufa msalaba apate kuutua/

Kafeli kujiua MUNGU hajapenda kumchukua/

Song:Rafiki
Artist: Stereo
 

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
8,000
2,000
Wakuu Umofia kwenu,

Karibuni katika Special Thread ya Tamaduni Music
Hapa tutakua tunatupia Line Kali tulizowahi kuziskia kupitia tracks za members wa Tamaduni

Tamaduni Music members

Nikki mbishi

Stereo

One the incredible

Songa

P the mc

Zaiid

Azma

Ghetto ambassador

Kad go

Dizasta vina

Nash Mc Madina

Phil technic

Man-sulii

Kila mmoja atupie punchline Kali anayoipenda ,ataje msanii na jina la nyimbo husika kama ifuatavyo
Sasa hawa wanamuziki ama wasanii tu wanaoiga miziki ya watu na kuifanya yo? Ebu tuondolee stress zao hapa, tuwekee wanamuziki wa kweli tuku-follow, wanamuziki wa ukweli ni wanamuziki wa dansi si hawa wasanii wa mtandao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom