Tamaduni Music hawajawahi kufanikiwa kwenye chochote kile wanachokianzisha

Vesper-valens

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
5,287
7,388
Hawa wasanii wa tamaduni Music hapa nawazungumzia

Nikki mbishi

Stereo

One the incredible

Songa

P the Mc

Zaiid

Ghetto ambassador

Kad go

Azma

Nash mc

Wakazi

Man su lee

Dizasta

Ni wasanii wenye vipaji vikubwa sana , kitu ambacho kimenifanya niwe shabiki yao mkubwa sana , Napenda tungo zao, flows n.k.

Lakini kinachonisikitisha hii crew kifedha hawana mafanikio yoyote ukija kwa msanii mmoja mmoja ukimtoa Stereo ambaye kaajiriwa na Azma ambaye kafungua biashara zake nje ya music.

Hawa wengine wote wana maisha ya kuikitisha sana tofauti na ukubwa wa vipaji vyao

Kuna kauli yao wanaipenda sana VITENDO DHIDI YA MANENO Lakini ukiangalia uhalisia wa mambo hii kauli yenyewe inawapinga kwakua hakuna hata moja walilo lianzisha likafanikiwa kwa asilimia

Tukianza na

Kilinge

Hii ilikua tamasha ambalo ilikua kila jumamosi wanakutana pale Msasani club kwa ajili ya kufanye vitu vingi kama battles , kuuz album, mixtape na project zao mbali mbali

Lakini kutokana na kukosa kwao nidhamu walishindwa kuendeleza huu utamaduni wa kilinge

Rap City Battle
Hii ni project nyingine iliyo anzishwa na Wakazi, One the incredible, P the Mc & Man su lee
Hii ilikua inafanyika pale Micasa lounge Riverside.

Walikua wanakutanisha underground Artists kwa ajili ya freestyle battle lakini baada ya muda walishindwa kuiendeleza

Kinasa
Hii ni project ya Nash Mc inafanyikia Temeke lakini hii nayo mpaka leo hatujawahi kuona impact yoyote coz hakuna kipaji kipya (New artist) chochote alichokitoa huko ushwahilini

Kikosi kazi kazini
Hii ni project ya mwisho ambayo iliongozwa na Azma , hapa waliunda kama kundi lakini hawakua tamaduni crew wote walikua kama nane, walitoa baadhi ya nyimbo na walisema washafanya album.

Lakini ukweli ni kwamba nyimbo iliyofanya vizuri ilikua ni ile Dis truck ya WEUSI na hii ilipata media coverage kubwa kwa sababu wali diss Kundi la weusi.

Baada ya kutoa ile dis truck ngoma zilizofuata hakuna media iliyokua na mpango nazo
Taaribu wakaanza kukaa kimya mpaka leo

Ukiwauliza mmoja mmoja watakuambia bado kikosi kazi ipo lakini ukweli ni kwamba walishaona financially haikua na impact yoyote zaidi ya kujichoresha tuu

Inasikitisha sana kuona hawa jamaa wanaenda kuzeeka bila kunufaika na vipaji vyao , wameku wakiwa diss sana wasanii wengine wa HIPHOP walio main stream kuwa wanapendelewa lakini ukweli hawa jamaa wanafeli kutokana na ujinga wao wenyewe.

Bado wana mentality za kimtaa mtaa na hawajua jinsi soko la Music linavyoenda

Inashangaza sana mpaka leo bado wanaendelea na mfumo wao wa kuuza Santuri na kanda mseto kwa kuzungusha mtaani , email na whatsapp ..eti madai yao hizi plartform zinazouza music zinawaibia

Huu ulimbukeni wao ushawagharimu na utaendelea kuwa gharimu sana

Ukianza hata level ya umaarufu hawa jamaa wanafahamika na watu wanaofuatilia sana HIPHOP
 
Aina ya muziki wanaofanya hata Marekani kwa sasa haulipi... hawa wangekuwepo miaka ya 90 mwishoni hadi 2000 mwanzoni wangepiga hela... kwa sasa hiphop yao hata Marekani hawafanyi. Kwa sasa watu wanataka vitu laini sio hizo ngumu zao. Huko USA ndo kwanza wanazidi kujichanganya kwenye Afro music... Tamadun wasipobadilika kama Weusi watazidi kupiga miayo. Nampongeza sana Azma kwa kufanya biashara zake nyingine ambazo pia zinafanya vizuri.
 
Azma me mwenyewe namkubali sana kwa anachokifanya ....akili kubwa

Stereo naye ajira inam'beba

Wengine n walala hao tunakutana nao kwenye daladala
 
Mengi kama sio yote uliyoeleza ni ya kweli kabisa, jamaa ni wasanii wakali sana lakini wasio na mafanikio makubwa kimuziki. Wana mauzo duni, hawana endorsement na deals nyingine, hawana tuzo za muziki nk

Sababu ya wao kutofanikiwa ni ipi sasa?
Kwenye Kilinge umeeleza kuwa project ilikufa kutokana na wao kutokuwa na nidhamu. Hujaeleza kwa kina ni vipi walikosa nidhamu na ni vipi kukosa kwao nidhamu kukapelekea kufa kwa project.

Rap city battle
Hii nayo hujaeleza kwa undani kwa nini ilishindwa kuendelea. Nafikiri Wakazi tutamtag twitter aitolee ufafanuzi. Vivyo hivyo kwa kikosi kazi kazini na nyingine pia.

Maoni yangu
1. Hujuma na Fitna
Hawa wana Tamaduni Muzik wanafanyiwa hujuma kubwa ya kimuziki na magodfather wa kiwanda cha muziki, hiyo ndiyo sababu kuu ya wao tamaduni kushindwa kutoboa. Watu kama kina Tale na Fella, hawa ndio wanaolalamikiwa sana kuwa waamuzi wa nani atoke na nani asitoke. Hapa ilikuwa ni pamoja na marehemu Ruge kupitia Clouds fm, na yeye alikua mmoja wa wauaji wa Hiphop muziki kabla ya Tamadun na hata baada ya Tamaduni. Hujuma na Fitna zinafanywa sababu ya hao magodfather kutaka wasanii walio chini yao waende zaidi, au kutaka wagawane mapato na hawa tamaduni muzik katika uwiano ambao unaoonekana wa kinyonyaji kwa tamaduni, hali inayosababisha wanatamaduni kukataa na hivyo kudispliniwa kwa kubaniwa, Rejea wimbo wa Babu Talent wa Nikki Mbishi.

Hapa kwenye fitna unakuta makampuni makubwa hayawapi endorsement hawa wana bila sababu ya msingi. Mfano labda CRDB au AIRTEL wanataka tangazo la huduma yao lifanywe kwa Rap, wapo tayari kufanya na msanii asiyejulikana kabisa kuliko kufanya na hao tamaduni. Au wanaweza mpa AY ambaye uwezo wake kirap hauwezi kuzidi hawa wa tamaduni, na hata relevancy yake kwa sasa angeweza kuitwa msanii mkongwe.

Kibiashara, new school artist ndio huhitajika matangazoni maana wateja wengi targeted ni wa kizazi cha new school. Kuna tangazo moja la airtel money, jamaa amerap sijui ni nani, tangazo ni kali ila msanii aliyelifanya sidhani kama ni maarufu. Sasa fitna inapelekea wakose pesa na kukosa pesa inafanya wasitoke.

Fikiria Harmonize anapata endorsement ya milioni 300 hapo CRDB kufanya matangazo ya audio na picha mnato, hiyo deal angepewa Nikki Mbishi hata kwa nusu bei, si angetoboa kabisa mwana na impact ya tangazo ingekuwa sawa tu na anavyofanya harmonize.

Mwaka 2010 au 2011, tamaduni muzik walikuwa wanaitwa wasanii wa internet, yaani wasanii wanaojulikana mitandaoni tu. Hili neno lilikuwa linatumiwa na weusi pamoja na watangazaji wa radio kubwa kama clouds. Tuzo za Kili mwaka huo zikafanyika kwa kupiga kura mtandaoni, lilikuwa ni jambo jipya. Tungetegemea waliojitanabaisha kuwa wasanii wa internet washinde hizo tuzo, ila nako walipigwa fitna hata nominations tu walikosa. Uzingatie wasanii wengine hawakuwa wamezingatia soko la mitandaoni kwa wakati huo.

2. Fedha na uwekezaji
Jambo kubwa linalowaangusha hawa tamaduni ni uwekezaji. Fedha inahitajika ili kufanya ngoma kali za kiwango bora (quality) lakini kwa kujiself sponsor inasabanisha wana washindwe kufanya track za mixing kali na pia kufanya video kali na directors wakubwa.

Mfano huo wimbo wa Babu Talent licha ya kuwa na mashairi supa, video yake ni ya kiwango cha kawaida kabisa - yaani kuchezwa na tv hata za ndani inakuwa ni kwa kudra tu za Mungu.

Mfano, kwa sasa studio kama za WCB au kina Mocco genious, zina kiwango kikubwa sana cha utayarishaji wa muziki, hawa tamaduni wangeweza kufanya mixing na mastering zao huko lakini ama hawana fedha kulipa hizo studio ama hawahitajiki kwa hizo studio ama ego tu inawafanya wenyewe tamaduni waone ni uwack kwenda kwenye hizo studio.

3. Mentality
Kufanya commercial muziki tamaduni wanaona ni uwack. Hapa wanapishana pakubwa sana na biashara. Duniani kote muziki sasa hivi ni biashara. Inabidi wakubali mabadiliko kuendana na nyakati na pia soko.

Wao watakwambia, mfano sasa hivi ushoga ndio umetrend duniani, kwa hiyo na sisi tuwe mashoga ili kuendana na nyakati?? Hapo labda umewaambia wafanye muziki kwa beat zilizo kisasa (trap, drill nk). Mo Famous aka Mo Tecnic aka Jay Moe alifanya ile pesa ya madafu kwa beat ya trap na akarap kiufundi, haikumuondolea uana hiphop wake na ilimrejesha kwenye game japo hakuendeleza sana uwepo wake.

Sasa tamaduni inabidi wabadilike mtazamo, wakubali kujiendesha kibiashara. Wakubali kula na kuliwa kibiashara, heri nusu shari kuliko shari kamili. Kuna kipindi Stereo alifanya kazi na WCB na alisogea sogea sana, hata sasa nafikiri ndio msanii anayeingiza kipato kikubwa kupitia muziki kwa hao tamaduni.
 
Aina ya muziki wanaofanya hata Marekani kwa sasa haulipi... hawa wangekuwepo miaka ya 90 mwishoni hadi 2000 mwanzoni wangepiga hela... kwa sasa hiphop yao hata Marekani hawafanyi. Kwa sasa watu wanataka vitu laini sio hizo ngumu zao. Huko USA ndo kwanza wanazidi kujichanganya kwenye Afro music... Tamadun wasipobadilika kama Weusi watazidi kupiga miayo. Nampongeza sana Azma kwa kufanya biashara zake nyingine ambazo pia zinafanya vizuri.
Sure
 
Back
Top Bottom