Tamaduni Music Punchlines Special Thread

Hakuenda shule ila aliheshimika kama mwalimu // alikuwa mzuri kweli lakini shobo hana
Hakuna aliyemgusa kwani alikuwa wa moto sana...

Alipopita tulio balehe tulimwaga mbegu....

Walikuja madogo wajanja na mapesa wakamuuliza mama ukivaaje unapendeza....


Dizasta vina - mwanajua.
Huu wimbo nmeusikiliza Mara kibao Ila unatafakarisha

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Swahili... Stereo

Chini dundo kama kawa voko ya kigumu
Hizi floo haziendi Sawa na miondoko ya kidumu
Tisha kama fiva viva black viva necha
Nasikika mpaka jenifa beniva deliver lekicha
Maisha sio matamu jimudu pasua kibubu
Nazijua kalamu hata kabla sijakua vidudu
Kipaji na ujuzi wa mengi unafanya nisishinde bubu
Wanga mkikesha mungu atanilinda nisipigwe juju
Acha kasumba kayumba nayumba wema
Naposaka mchumba nikifa muumba ataniumba tena
Snitch kibao pumba
Masnitch nao wanadundwa
Unaweza ukapata mchumba na usipate unyumba mwema
Neema za manati
Rehema za hayati
Napotema sina wema kwa nyangema wa masaki
Cheza kila gemu na usicheze bila nguo
Bongo fleva kama demu yule mliekutana chuo
Mi n mmang'ati mwenye bifu na Masai
Nipe chati niko safi kama tripu za maksai
Donoa tachi niwamiminie mwani
Ka vipi waibuke chachi niwafukizie ubani

Stereo Soo
 
Nafunguka mtumwa anakua Huru /
The great hawezi kufa kwa kusukumwa na lulu
NIKKI MBISHI
 
Hamaki au piga Mbiu kwa washikaji/
Niite songa samaki mwenye kiu ndani ya maji/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom