Tamaa ya fedha kupita kiasi; does it worth it?

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,436
Reaction score
4,927
Nisinukuliwe vibaya, ni kwa nia ya kuchokoza mada ili tujue ni kwanini ufalme wa pesa unazidi kuwa mkubwa duniani na Tanzania kwa ujumla.

Nitazungumzia Tanzania kwa sababu ndo ninaishi, huko duniani kwengine siwezi ku-draw conclusion sababu sijaishi.

Aisee, yaani sasa kila mtu hapa Tanzania anachowaza ni ufalme wa fedha! Kila kitu anachokifanyika, ajenda yake kupata fedha zaidi!

Kiongozi mwanasiasa anapewa nafasi fulani, siku yake ya kwanza ofisini, anaanza kuwaza atafanya mitikasi gani ili aanze kupata fedha kwa kutumia hiyo nafasi aliyonayo. Na akianza kupata hizo fedha, akili yake inachangamka anaanza kuwaza, atapataje fedha nyingine zaidi ya hizo anazozipata. Na endapo yeye kupata fedha zaidi, kunahusisha kumkanyaga mwenzake mguuni, basi yupo radhi amkanyage mara 100, ili aendelee kupata fedha zaidi.

Naenda kwa muuza bucha leo kununua maini, ananiambia bei ni 15,000 wakati jana ilikuwa ni 14,000 na najua bei ni 14,000. Namuambia nipe gram 500 ananipimia gram 460, namuambia, 'mbona haijatimia?' anasonya kwa kukasirika, anairudisha kwenye mzani na kuongeza gram 40, ili zitimie gram 500. Nakaa najiuliza, hii shida yote nini? Najijibu: Anataka kukupunja wewe, apunje na wengine 100, ili atengeneze fedha zaidi!

Huko makazini ndo kabisa. Yaani vikao kila siku mwenyekiti akiitisha AOB, wajumbe wakianza kuongea basi malalamiko yao ni kuhusu wao kupata pesa au kupunjwa pesa, au kufikiria kupewa pesa fulani. Yaani ni kupata pesa zaidi.

Tamaa ya pesa inatia kichefuchefu kwa sababu kuna mambo yanafanyika kwa ajenda ya tamaa ya fedha nyingi, yamejeuka kuwa machukizo kwa jamii. Huduma hazitolewina zikitolewa ni kwa ubora wa chini, dhulma, wizi, utapeli, mauaji... etc

Naomba kuuliza: Hivi huu ulafi wa fedha utaisha lini? Kwa nini watu wawe na mentality ya fedha kwanza, na fedha zaidi kwa gharama yeyote?

Kwa sababu unakuta mtu anakurusha fedha, au anakudhulumu haki yako, halafu mwisho wa siku unakuta anaandamwa na matatizo makubwa kiasi kwamba hata hizo fedha nyingi kwake hazina maana.

Tamaa ya kupata mahela mengi hata kwa njia haramu; does it worth it?

Tujadili.
 
Financial freedom ni muhimu
Hata kwa kukanyaga miguu ya wengine? Maana hoja yangu ndo ipo hapo.

Kwa hiyo seeking financial freedom ndo iwe kali mpaka kupata hela hata pale ambapo hujapanda?

Na kingine: hicho unachosema ni 'financial freedom,' ni jambo gani haswa?

Ukiwa na Milioni 500 au bilioni 1, hiyo ndo maana ya financial freedom?
 
Pole sana , Hali itakua mbaya Zaid miaka ijayo...si unaona hata machawa wa ccm unafikiri kwanini ni machawa ..wengine wako tayar hata kufirwa ili wapare pesa ..
Kuna mmoja alifirwa ili apate elfu 90 tu.
Ndo maana najiuliza ni kwanini hii kitu? Yaani hii mentality ya, 'kupata fedha kwa gharama zozote,' kwanini imekuwa hivi yani? Kwanini tamaa ya fedha inafanya watu wazitafute kwa gharama yoyote ikiwamo kutenda dhambi?

Halafu wakishapata hiyo 'ultra wealth,' kwa njia za panya wanaifanyia nini? Hiyo ndo furaha yao?
 
Acha basi mkuuu 90 ikamtoa mtu rindaa aiseee
Yawezekana kabisa, fedha imetengenezewa ufalme kiasi kwamba hata mtu akiiona tu tayari anafunmbwa macho na shetani anamnong'oneza, 'pokea tu hiyo elfu 90, ku-***** sio kitu kikubwa hata!'

Yaani maana yangu ni kwamba: yawezekana nafsi inayopia ufalme fedha, ikawa rahisi kudanganyika na shetani kutenda kosa lolote ili tu, mtu huyo apate fedha, haijalishi ni kidogo au kikubwa.
 
Kariri tu kuwa hakuna pesa nyingi kwa mkupuo zinazotoka kwa Mungu. Ukipata ufurahiye mapesa, chungulia tu ulimwengu wa roho ila uwe tayari kwa masharti.
 
Nisinukuliwe vibaya, ni kwa nia ya kuchokoza mada ili tujue ni kwanini ufalme wa pesa unazidi kuwa mkubwa duniani na Tanzania kwa ujumla.

Nitazungumzia Tanzania kwa sababu ndo ninaishi, huko duniani kwengine siwezi ku-draw conclusion sababu sijaishi.

Aisee, yaani sasa kila mtu hapa Tanzania anachowaza ni ufalme wa fedha! Kila kitu anachokifanyika, ajenda yake kupata fedha zaidi!

Kiongozi mwanasiasa anapewa nafasi fulani, siku yake ya kwanza ofisini, anaanza kuwaza atafanya mitikasi gani ili aanze kupata fedha kwa kutumia hiyo nafasi aliyonayo. Na akianza kupata hizo fedha, akili yake inachangamka anaanza kuwaza, atapataje fedha nyingine zaidi ya hizo anazozipata. Na endapo yeye kupata fedha zaidi, kunahusisha kumkanyaga mwenzake mguuni, basi yupo radhi amkanyage mara 100, ili aendelee kupata fedha zaidi.

Naenda kwa muuza bucha leo kununua maini, ananiambia bei ni 15,000 wakati jana ilikuwa ni 14,000 na najua bei ni 14,000. Namuambia nipe gram 500 ananipimia gram 460, namuambia, 'mbona haijatimia?' anasonya kwa kukasirika, anairudisha kwenye mzani na kuongeza gram 40, ili zitimie gram 500. Nakaa najiuliza, hii shida yote nini? Najijibu: Anataka kukupunja wewe, apunje na wengine 100, ili atengeneze fedha zaidi!

Huko makazini ndo kabisa. Yaani vikao kila siku mwenyekiti akiitisha AOB, wajumbe wakianza kuongea basi malalamiko yao ni kuhusu wao kupata pesa au kupunjwa pesa, au kufikiria kupewa pesa fulani. Yaani ni kupata pesa zaidi.

Tamaa ya pesa inatia kichefuchefu kwa sababu kuna mambo yanafanyika kwa ajenda ya tamaa ya fedha nyingi, yamejeuka kuwa machukizo kwa jamii. Huduma hazitolewina zikitolewa ni kwa ubora wa chini, dhulma, wizi, utapeli, mauaji... etc

Naomba kuuliza: Hivi huu ulafi wa fedha utaisha lini? Kwa nini watu wawe na mentality ya fedha kwanza, na fedha zaidi kwa gharama yeyote?

Kwa sababu unakuta mtu anakurusha fedha, au anakudhulumu haki yako, halafu mwisho wa siku unakuta anaandamwa na matatizo makubwa kiasi kwamba hata hizo fedha nyingi kwake hazina maana.

Tamaa ya kupata mahela mengi hata kwa njia haramu; does it worth it?

Tujadili.
Kwenye mambo yako ya kifedha usiambatane na mtu mwenye usongo sana na pesa
 
Kariri tu kuwa hakuna pesa nyingi kwa mkupuo zinazotoka kwa Mungu. Ukipata ufurahiye mapesa, chungulia tu ulimwengu wa roho ila uwe tayari kwa masharti.
ndo najiuluza sasa, mtu akishazisukua hizo 10 billion halafu ndo atakuwa na furaha ya kudumu? au ndo watu wakimshobokea kwamba ni tajiri, 'don' basi ndo kufanikiwa kwake huko??

Kwanini yani mtu anasema atapata fedha kwa gharama yeyote, ikiwemo hata kuua?
 
Maandiko yamesema "fedha ni jawabu la mambo yote"

Mimi nani niende kinyume na maandiko?
lakini maandiko hayo hayo yanasema, 'usidhulumu'

Kwahiyo kwako kujipatia fedha nyingi hata kwa kukanyaga wenzako ni sawa? maana ndo hoja yangu ilipo hapo.
 
Kwenye mambo yako ya kifedha usiambatane na mtu mwenye usongo sana na pesa
sahihi kabisa. zamani baba yangu alikuwa anafanya biashara ya ubia na wenzake, wakamjeuka baba, wakakimbia na hela zote. Mzee akarudi kwenye umasikini.

Huwezi amini wale wababa waliomtapeli dingi wameshafariki na wengine walijiua kalafu hata na watoto wao wakageuka kama vichaa wengine wezi majambazi, ndoa zao zikavunjika wengine

Kuna mda nakaa najiuliza, so what? walifanya hayo yote na dhuluma, halafu ikawaje?
 
Kuna hawa viongozi wanao kula Nauri Sijui huwa wana waza nini
Ndo hayo hayo, kujipatia fedha zaidi. Huwezi amini mimi nilipiga dili la hela na mzee mmoja mkubwa sana, halafu akanirusha laki tatu. Yaani laki tatu, mtu anaendesha v8 anakurusha laki tatu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom