Kwani hilo jengo limeota ghafla kama uyoga, wakaamka asubuhi wakalikuta lipo? (Hapana)
Limejengwa muda wote kwa siri? (Hapana)
Unaweza kulificha ghorofa refu kwa kuliwekea uzio? (Hapana)
Watu wa Ikulu walikuwa wanapita njia gani kuelekea Ikulu wakati ujenzi ukiendelea? (Njia hiyo hiyo)
Walikuwa hawalioni wakati mkandarasi kaweka na vibao kulitambulisha ujenzi wake? (Waliona)
Hakuna mamlaka za Serikali yetu tukufu zilizobariki ujenzi huo? (Zipo)
Wanausalama wanaotoa assessment zao za kiusalama sasa, hawakuwepo wakati linaanza kujengwa (Walikuwepo)
Walichukua hatua gani kulizuia kwa sababu za kiusalama? (Walinyamaza)
HIVI WATANZANIA WENZANGU, HATUWEZI KUACHA USANII HATA KIDOGO? (Tumejitahidi tumeshindwa)
Sasa mtajeni kigogo aliye "nyuma" ya ghorofa hili, au mnyamaze milele! Tushachoka sisi.