Nchi yetu ni ya kusadikika kweli kwani tunangoja mpaka mambo yameharibika ndio tunaanza kupiga mayowe!!! Acha hilo sakata la hilo ghorofa karibu na Ikulu; hivi sasa kuna ufisadi wa hali ya juu unafanywa kuhusiana na viwanja vya TANGANYIKA PACKERS, ambavyo inasemekana serikali imemrudishia fedha zake yule muwekezaji kutoka arabuni na sasa wameamua kuhujumu wenye nchi viwanja pale mahala. Ukipita kule chini karibu na hotel ya Mediterranian utakuta jamaa amekatiwa kiwanja kikubwa na anaharakisha kuzungusha ukuta na kuendeleza ile sehemu ingawa inasemekana kuna mpango kabambe wa NHC kujenga sehemu ile!!! Sasa ni wakati muafaka wa kumzuaia yule anayejenga ukuta sehemu ile kwani ujenzi wake utaathiri ramani iliyotayarishwa na NHCya kuendeleza sehemu ile!!! Meya wa Kinondoni Mwenda should be held accountable kwa ufisadi huu.