Nabii la uongo katika ubora wake wa kupotosha! umezungumzia Maandiko ya biblia na hoja inahusu biblia umeogopa kuweka hata kifungu kimoja cha ku backup huu upuuzi wako hapa atleast ungeweka hata vifungu vya kuunga unga tukuone umetumia maandiko kufikiria ila umekurupuka baada ya kushiba mahaerage sijui ya Mbeya hayo!
Anyway nitakusaidia kidogo kujua maandiko,Torati ni SHERIA,Mungu aliweka sheria za kuwaongoza wanadamu kipindi kile cha zamani kabla ya kuja kristo Yesu,ndio hiyo torati ulikuwa unaandika hapo juu,
Watu woote waliokuwa chini ya Sheria ya Torati walikuwa chini ya Laana! (Wagalatia 3:10-11),Hakuna binadamu yeyote atakayehesabiwa haki kwa matendo ya TORATI(SHERIA)!!! (Warumi 3:19-26)
Alivyokuja Yesu sasa matendo yoote ya sheria (Torati) Yalikoma! au yalibadirika kutoka matendo ya kimwili kwenda matendo ya kiroho!!!!!,Yesu alikuwa ndio mwisho wa SHERIA!!! Warumi 10:4-6,Hayo matendo yoote ya sheria ya Musa yalikoma baada ya Kristo Yesu kufa na kufufuka ndio maana Wale Mitume walipoanza kuhubiri injili walikuja na standard MPYA kabisa walikuja na Njia Moja tu,Injili moja tu, na Mungu mmoja!
Angalia sasa namna Mambo Ya TORATI/SHERIA yafuatayo yalivyobadirika baada ya Yesu Kuja
1.NDOA
Ndoa ni ya mke mmoja na mume mmoja TU!
>Kwa mwanamke anafungwa kwenye kifungo cha Ndoa kama mumewe bado yupo HAI! kama akiachana na Mumewe wa ndoa akaolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe wa ndoa bado yupo hai Biblia inasema anakuwa anafanya UZINZI (WARUMI 7:1-3,1Wakorinto 7:39)
>Kwa mwanaume akimuacha mkewe akaoa mwanamke mwingine anakuwa anafanya UZINZI (Luka 16:18,Marko 10:11)
Biblia imeweka wazi kabisa baada ya Yesu kuja kuwa mume mmoja kwa mke mmoja mpaka kifo sasa endapo wawili hawa wakashindwa kuelewana Je biblia inasemaje kuhusu hilo? Mungu sio mjinga alijua sio Mahusiano yoote ya mwanaume na mwanamke yatakuwa yakudumu hadi kifo katika ndoa kwahiyo Mungu aliweka utaratibu ambao unatakiwa ufuate KUTENGANA/KUACHANA kama endapo kwa namna moja au nyingine mtashindana ndani ya ndoa ila bado mnabakia kifungoni hadi mmoja wenu afariki imeandikwa hapa (1wakorinto 7:10)
Sheria ya Mungu imewabana woote katika ndoa mwanaume na mwanamke!
2.SABATO
Sabato kipindi cha Musa ilikuwa ni siku ya Kupumzika kwa mwili,hakuna kufanya kazi siku ya sabato kama sehemu ya kumkumbuka na kumuheshimu Mungu katika zile siku 7 za wiki basi siku ile ya mwisho wa wiki iliwekwa maalumu kwa ajili ya hivyo kutoa PUMZIKO la kimwili!
Alivyokuja Yesu hakuitunza sabato! alifanya kazi na kuhubiri hadi ndani ya masinagogi siku ya sabato hadi wayahudi wakakasirika,wayahudi ambacho hawakujua nikwamba Yesu mwenyewe ndio alikuwa SABATO! Marko 2:27-28,maana yake nini?? sabato ya sasa ni kumfuata Yesu then Yesu ndio atatupa Pumziko la MILELE maana yake atatupa sabato ya milele ndiomaana alisema Nifuateni ninyi nyoote mnaoelemewa na mizigo na mimi nitawapa PUMZIKO! (Matahyo 11:28) ile sabato ya enzi za Musa ilishakoma sasahv kuna sabato Kubwa zaidi ambayo ni kumfuata Yesu!
3.TOHARA
Tohara ya wayahudi wa zamani ilikuwa kwa mujibu wa sheria/torati na ilikuwa ya Nyama! baada ya yesu tohara ya wayahudi halisi ikawa tohara ya MOYO na inafanywa na Mungu mwenyewe! (Warumi 2:28) sio tena ile ya NYAMA!
Kuna vitu vingi sana naweza kuviandika hapa ambavyo vilibadilika baada ya Yesu kuja hatuko tena CHINI YA SHERIA !!!!
Ndoa ni ya mke mmoja na Mume mmoja usidanganye na kudanganyika Ukioa/Kuolewa Unakuwa ndani ya kifungo endapo mkatofautiana Mnaruhusiwa kutengana Tu! na kama mkisuluhishwa mnaweza kurudiana ila hamruhusiwi kuachana na kila mtu kuoa/kuolewa Biblia imezungumza wazi kabisaa kama ukifanya hivyo unakuwa una fanya UZINZI!!!!!!!!!!!!!,I mean mfano rahisi tu ni kama Frola Mbasha kaachika kwa mumewe wa kwanza kaenda kuolewa na Mwanaume mwingine kila mara Wanapokutana naye kimwili mbele za Mungu na kwa Mujibu wa biblia ANAKUWA ANAFANYA UZINZI
Na wazinzi hawaendi MBINGUNI! kuwa makini na maandiko unayoyatoa hapa usije ukawapoteza watu kama huna uhakika na jambo lolote la kibiblia bora uliza au kaa kimya ukipotosha hiyo dhambi itakuwa mikononi mwako!