Talaka Haijakatazwa

Talaka Haijakatazwa

Hoja ya kupinga talaka kwa madheheb ya ukristo dhumun lake ni nn??

Inaana hao mapadri hilo torati hawalifaham??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo mana kuna ulalamishi kuna walio ongeza maandishi kwenye vitabu vya mwanzo kwa manufaa yao ya kupinga imani.

Yani imekua ngumu kumwambia mtu hakuna Mungu sasa basi wenue akili wakaona tuwageuze humu humu kwenye imanizao waende ndivyo sivyo ndicho kinacho endelea

KUNA MADHEBU MPAKA KESHO KUNAVITU VINAENDELEA KUFANYIWA MAREKEBISHO hii nikutokana na mikono ya wasio wema kuharibu maandishi ya kweli.yale ya muumba huoni tatizo ila haya ya kibinadam ni fikirishi ndomana muda ukifika watu wana sema hili hapana nakubadili vifungu
 
ntapambana nae sitoi talaka


Huwezi pambana na mtu mkuu. hata Mungu alimfukuza Adam na Hawa bustanini japokuwa hakuwaahidi kuwa wakila tunda angewafukuza. Hata shetani alifukuzwa mbinguni. Biblia inasema usishindane na mtu muovu. Busara ni kufukuza tuu.

Take from your God
 
Tupo pamoja mkuu, "alichounganisha Mungu asitenganishe binadamu" Tangu lini Mungu akaunganisha watu na starehe zao? Nashangaa wana ndoa wanadundana kila siku wanashindwa kutengana kwa kuogopa huo msemo! Talaka kama kazi hakuna cha kuunganishwa, haunganishwi mtu hapa!hongera waislamu kwa kuliona hilo!


Kweli kabisa
 
Kitu kilichonifurahisha ni jinsi ulivyo jijengea hoja yako ya namna ya kumfukuza mwanamke uliyempiga sound kuwa unampenda kumbe unamtamani tu.
Nadhani kama mambo yenyewe yamekuwa hivi, basi tusioe kabisa bali tuwalale huko huko kwao au gesti tujirudie nyumbani wepesi.
Mke sio papuchi tu ila mke ni msaidizi. Tena mmoja tu. Hujiulizi, Adam alikuwa na mbavu ngapi ila Mungu akautoa mmoja tu na kuufanya mwanamke?? Hujiulizi, kwa nini Mungu hakumwongezea Adam mke mwingine??
Usioe, kama unataka kumlala halafu umwache. Huyo sio wako ni wa mtu hivyo wazini. Na wazinzi mwisho wenu ni lile shimo la moto milele. Mbona mnamwona huyo mwanamke ka takataka flan hivi mnayoweza kuitupa nje tu ikawe mbolea na wanaume sisi ndio bora zaidi?? Kwani huyo mwanamke hawezi kututimizia wanaume 2, 4, 6 kwa siku nasi tukatosheka? Tumpe basi na yeye ruksa kuolewa siku akitaka na kutoa talaka siku akitaka.
Mungu hajawahi kukosea na hatakaa akosee. Aliujua ugumu wa moyo wako ndo maana akakuacha ufanye utakalo ila alishakuambia; Mume mmoja kwa Mke mmoja tu. Zaidi ni uzinzi na uasherati na mwisho ni ukimwi
 
Inatolewa kwa sharti hiyo talaka....sio umeamka asubuhi chai haijawekwa iriki unatoa talaka...makazi yako motoni tu.......talaka itolewe pale inapobidi na unaona kabisa hakuna namna lazima itoke na si vinginevyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hivyo inatolewa pale inapotokea sababu za msingi kama unavigezo vinavyojitosheleza ruksa kupewa au kutoa talaka huwezi kulazimishwa eti muishi mpaka kifo kiwatenganishe na ndio maana hata cku ya ndoa mnaambiwa kabisa mmeoana kwa heri na ikibidi kuachana kwa heri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu Wakuu!

Mimi ni Mkristo, nimezaliwa huku na nimekulia huku. Nimelelewa na kufundishwa Biblia na maandiko mengi ya kidini. Hivyo ni kusema kwa habari ya dini ya kikristo ambayo inamadhehebu mengi kuliko hata dini nyingine huwezi nidanganya kitu chochote.

Wakristo wengi hufuata mapokeo kuliko neno la Mungu. Husikiliza sauti za wachungaji kuliko hata kile ambacho neno la Mungu linasema. Madhebu bora zaidi katika ukristo ni yale yanayofuata kila kisemwacho na maandiko yaliyomo katika biblia.

Mapokeo hayo yamewafanya waumini kuishi kama misukule, wakiishi bila raha na kuona maisha hayana maana yoyote ile.
Leo nitazungumzia habari za Talaka katika ndoa.

Mungu alimpomuumba Adam alimpa zawadi muhimu ambazo ni:
1. Kumiliki na kuvitawala Viumbe wengine
2. Chakula
3. Bustani
4. Mwanamke

Baada ya kutoa zawadi hizo Mungu alitoa vigezo na masharti kwa kila zawadi alizompa.
Zawadi ya mwisho inazaa kitu kinaitwa ndoa. Yaani Muunganiko wa kimahusiano ya kimwili, kiroho, hisia, kimwili, kiuchumi, kijamii n.k baina ya mwanaume na mwanamke.

lengo la zawadi ni kumfurahisha mtu, hivyo Mungu alijua kuwa moja ya zawadi itakayompendeza mwanaume ni kumpatia msaidizi ambaye ni mwanamke. Hakika ilikuwa hivyo. Kitu cha pekee ambacho Mungu alikitaka kutoka kwa Adamu ni kumuona akifurahi. Ndio maana upweke wa Adamu ulimfanya Mungu afikiri kitu kingine kitakacho ondoa ukiwa wake.

Kumbuka Dunia iliumbwa kwaajili ya Mwanaume, Vingine vyote ni zawazi na rasilimali ambazo zitamuwezesha Mwanaume aishi maisha ya raha Mustarehe. Hivyo Mwanaume usijichukulie Poa. Hii dunia ipo kwaajili yako. Tumia chochote ukipendacho kwa mapenzi ya Mungu.

Baada ya watu kuwa wengi, wanawake walikuwa wengi kuliko wanaume. haikutokea kwa bahati mbaya hii. Bali yote ni kuhakikisha kuwa Mwanaume anakuwa na option nyingi ili apate uhuru wa kuchagua akipendacho. Mungu alijua kama angefanya idadi ya wanaume na wanawake kuwa sawa ingeleta tabu sana. Kwani kwa jinsi alivyomuumba mwanaume alijua wapo wanaotaka kuoa wanawake zaidi ya mmoja. Hivyo wengine wangekosa na hii ingezua balaa chini ya jua. Hakuna mwanamke anayependa kiasili kumilikiwa na wanaume wawili. Hata Maandiko yanasema huwezi tumikia Mabwana wawili Lakini haijasema huwezi kutumikia mabibi?wake wawili.

Talaka katika Biblia inaelezewa katika Torati ya Musa ambapo ndio msingi wa sheria ya Mungu. Hayo mengine ni historia na mafundisho ya kuwafunza watu na kuelezea hiyo Torati. Hivyo ni kusema, vitabu kama zaburi, injili na vitabu vya unabii ni mafundisho kuhusu Mungu lakini Totati ndio msingi na kitu pekee kitakachotumika kukutia hatiani. Hata siku ya hukumu kitabu pekee kitakachotumika ni torati yaani sheria ya Mungu.

Kumbukumbu la torati 24
1 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.
3 Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe;
4 yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi.
5 Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.

Aya ya kwanza inaelezea kuwa mtu akiisha kutwaa Mke kwa kumwoa, lazima apate kibali machoni mwake. Hapa ni kulingana na muono wa mhusika. Endapo ataona neno Ovu juu yake, neno ovu kulingana na aya zingine linaweza kuwa endapo hajakuta ubikra anaweza pia kuvunja ndoa hiyo na kutoa talaka. lakini ni kulingana na muono wa muoaji. Ikiwa bikra si tatizo lakini anatatizo la kitabia basi pia anaweza kumpa talaka. Lengo si kuishi kwa taabu katika ndoa bali kufurahia maisha.

Mungu amempa mwanadamu uwezo wa kuchagua kile atakacho, hakuona sababu ya kukutafutia na kukulazimisha umuoe fulani wakati wewe humtaki. Ndio maana akasema utatafuta wakufanana na wewe. Si kazi yake kukutafutia mke. Baada ya kupata mke kazi yake ni kukupa watoto kwa jinsi utakavyo wewe. Suala la kuwalea lipo juu yako. Sasa Watu wanachanganya madesa kuwa kila kitu ni mipango ya Mungu jambo ambalo si kweli, na kama ni kweli basi Hakuna Hukumu.

Mungu anampa mamlaka Mwanaume kumtoa mwanamke/mke asiyepata kibali kulingana na muono wake. Mwanamke anahaki ya kupewa talaka kama hati itakayomruhusu aolewe na mwingine. kumaanisha bila talaka mwanamke hajapewa kibali cha kuolewa tena.

Sasa Watu wanachanganya maandiko, hawajui kila kitabu kinadhima yake. Vipo vitabu vya sheria, hivi vinajitegemea na vinaeleza mwanadamu aishi vipi duniani. Yani hivi ni kama Katiba. Dhima yake kubwa ni kuelezea sheria za Mungu. Vitabu vingine vinaunga mkono sheria hizo na kutoa mafundisho mengine na unabii.

Sasa Mtu sheria inasema Kwa mfano: Mtu asile chakula fulani. Mtu anatoa kifungu kutoka katika aya za injili au Zaburi, au vitabu vya unabii. huu ni upuuzi ambao Wakristo wengi wameingizwa mkenge. Huwezi vunja Torati kwa kutumia vitabu vya injili au zaburi.

Talaka ni muhimu ikiwa ndoa imekuwa chungu. Mwanamke kama hamuheshimu mume wake, endapo mumewe ataamua kutoa talaka asilaumu kwani anahaki na ni wajibu wake kufanya hivyo.

Hizo zingine ni porojo za kidunia. Eti alichokiunganisha Mungu Mwanadamu asikitenganishe. Hii nukuu imechukuliwa tofauti sana. Mungu akiunganisha kitu hata mwanadamu afanyeje hawezi kukitenganisha na Mungu akikitenganisha kitu Mwanadamu hata afanyeje hawezi kukiunga. Ndoa haipo kwenye listi ya vitu vilivyoungwa na Mungu. Bali ni makubaliano baina ya mke na mume. Endapo ndoa ingeunganishwa na Mungu isingewepo sheria ya talaka kwenye Biblia au Quran. Na pia ndoa zisingefunjika kamwe.

Nawasilisha
NAKARIBISHA POVU

Naona talaka uiongeleayo ipo upande mmoja wa wanaume! Kwa maelezo yako na mwanamke anaruhusiwa talaka iwapo mumewe yupo kinyume nae!
 
Talaka ni muhimu ikiwa ndoa imekuwa chungu. Mwanamke kama hamuheshimu mume wake, endapo mumewe ataamua kutoa talaka asilaumu kwani anahaki na ni wajibu wake kufanya hivyo.
Umeongea vitu vya msingi,ila nachokiona kwa sasa ndoa nyingi ni chungu na zenye kuleta mateso kutokona na viburi vya wanadamu,kujiona bora,kuridhika na kutomchukulia mwenza wake kuwa mtu wa maana kwake,kipato ,elimu na kutokufata viapo vya ndoa.Cha msingi hapa ni sisi wanandoa kuishi kwa unyenyekevu na kufata amri za mungu,apo ndoa zetu zitakuwa zenye amani na utulivu.MUNGU AWABARIKI.
 
Na ndiyo inavyoaminishwa mpaka sasa kwamba ndoa ikishafungwa haiwezi tenguliwa labda mpaka mmoja afe kwa upande huu...

Kwa upande ule mwingine... talaka ruksa...


Cc: mahondaw
 
Mathayo 19: 3-9
3. Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4. Akajibu, akawaambia, hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo , aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5.akasema, kwasababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6. Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7. Wakamwambia, jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8.Akawaambia, Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9. Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakaye mwacha mkewe, isipokuwa ni kwasababu ya uasherati, akaoa mwingine , azini naye naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mathayo 19: 3-9
3. Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4. Akajibu, akawaambia, hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo , aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5.akasema, kwasababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6. Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7. Wakamwambia, jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8.Akawaambia, Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9. Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakaye mwacha mkewe, isipokuwa ni kwasababu ya uasherati, akaoa mwingine , azini naye naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa talaka imeruhusiwa ila kwa kosa la uzinzi. The problem is, je ni uzinzi wa wote au wa mke tu?
 
Umeongea vitu vya msingi,ila nachokiona kwa sasa ndoa nyingi ni chungu na zenye kuleta mateso kutokona na viburi vya wanadamu,kujiona bora,kuridhika na kutomchukulia mwenza wake kuwa mtu wa maana kwake,kipato ,elimu na kutokufata viapo vya ndoa.Cha msingi hapa ni sisi wanandoa kuishi kwa unyenyekevu na kufata amri za mungu,apo ndoa zetu zitakuwa zenye amani na utulivu.MUNGU AWABARIKI.
Tunatetea talaka kwakuwa tumejiandaa kutenda maovu.
 
8.Akawaambia, Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9. Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakaye mwacha mkewe, isipokuwa ni kwasababu ya uasherati, akaoa mwingine , azini naye naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Soma vizuri hilo andiko na ulielewe. 8. Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa. Hili lilitokana na watu kutaka wapewe ruhusa kuwaacha wake zao kwa sababu tu ya tamaa zao.
Tangu mwanzo Mungu hakutaka tuwakiane tamaa. Alitaka tutimiziane haja zetu kistaarabu. Mtu unamkandia mkeo, mke wako mwenyewe unamkandia bao 6!! Za nini?? Kwani yu aenda safari??
Akilalamika kuwa punguza kiu hadi kesho, tiyari; Unaninyima. Huwa nawahurumia saana wanaume wenzangu wanao wakandia mabao 6 na zaidi wake zao. Kisa asichepuke. Kule nje cha mchepuko kimoja tena haraka haraka nako anaona raha zaidi kuliko huo mchezo wako wa kumuumiza.
 
Back
Top Bottom