Habari zenu Wakuu!
Mimi ni Mkristo, nimezaliwa huku na nimekulia huku. Nimelelewa na kufundishwa Biblia na maandiko mengi ya kidini. Hivyo ni kusema kwa habari ya dini ya kikristo ambayo inamadhehebu mengi kuliko hata dini nyingine huwezi nidanganya kitu chochote.
Wakristo wengi hufuata mapokeo kuliko neno la Mungu. Husikiliza sauti za wachungaji kuliko hata kile ambacho neno la Mungu linasema. Madhebu bora zaidi katika ukristo ni yale yanayofuata kila kisemwacho na maandiko yaliyomo katika biblia.
Mapokeo hayo yamewafanya waumini kuishi kama misukule, wakiishi bila raha na kuona maisha hayana maana yoyote ile.
Leo nitazungumzia habari za Talaka katika ndoa.
Mungu alimpomuumba Adam alimpa zawadi muhimu ambazo ni:
1. Kumiliki na kuvitawala Viumbe wengine
2. Chakula
3. Bustani
4. Mwanamke
Baada ya kutoa zawadi hizo Mungu alitoa vigezo na masharti kwa kila zawadi alizompa.
Zawadi ya mwisho inazaa kitu kinaitwa ndoa. Yaani Muunganiko wa kimahusiano ya kimwili, kiroho, hisia, kimwili, kiuchumi, kijamii n.k baina ya mwanaume na mwanamke.
lengo la zawadi ni kumfurahisha mtu, hivyo Mungu alijua kuwa moja ya zawadi itakayompendeza mwanaume ni kumpatia msaidizi ambaye ni mwanamke. Hakika ilikuwa hivyo. Kitu cha pekee ambacho Mungu alikitaka kutoka kwa Adamu ni kumuona akifurahi. Ndio maana upweke wa Adamu ulimfanya Mungu afikiri kitu kingine kitakacho ondoa ukiwa wake.
Kumbuka Dunia iliumbwa kwaajili ya Mwanaume, Vingine vyote ni zawazi na rasilimali ambazo zitamuwezesha Mwanaume aishi maisha ya raha Mustarehe. Hivyo Mwanaume usijichukulie Poa. Hii dunia ipo kwaajili yako. Tumia chochote ukipendacho kwa mapenzi ya Mungu.
Baada ya watu kuwa wengi, wanawake walikuwa wengi kuliko wanaume. haikutokea kwa bahati mbaya hii. Bali yote ni kuhakikisha kuwa Mwanaume anakuwa na option nyingi ili apate uhuru wa kuchagua akipendacho. Mungu alijua kama angefanya idadi ya wanaume na wanawake kuwa sawa ingeleta tabu sana. Kwani kwa jinsi alivyomuumba mwanaume alijua wapo wanaotaka kuoa wanawake zaidi ya mmoja. Hivyo wengine wangekosa na hii ingezua balaa chini ya jua. Hakuna mwanamke anayependa kiasili kumilikiwa na wanaume wawili. Hata Maandiko yanasema huwezi tumikia Mabwana wawili Lakini haijasema huwezi kutumikia mabibi?wake wawili.
Talaka katika Biblia inaelezewa katika Torati ya Musa ambapo ndio msingi wa sheria ya Mungu. Hayo mengine ni historia na mafundisho ya kuwafunza watu na kuelezea hiyo Torati. Hivyo ni kusema, vitabu kama zaburi, injili na vitabu vya unabii ni mafundisho kuhusu Mungu lakini Totati ndio msingi na kitu pekee kitakachotumika kukutia hatiani. Hata siku ya hukumu kitabu pekee kitakachotumika ni torati yaani sheria ya Mungu.
Kumbukumbu la torati 24
1 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.
3 Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe;
4 yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi.
5 Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.
Aya ya kwanza inaelezea kuwa mtu akiisha kutwaa Mke kwa kumwoa, lazima apate kibali machoni mwake. Hapa ni kulingana na muono wa mhusika. Endapo ataona neno Ovu juu yake, neno ovu kulingana na aya zingine linaweza kuwa endapo hajakuta ubikra anaweza pia kuvunja ndoa hiyo na kutoa talaka. lakini ni kulingana na muono wa muoaji. Ikiwa bikra si tatizo lakini anatatizo la kitabia basi pia anaweza kumpa talaka. Lengo si kuishi kwa taabu katika ndoa bali kufurahia maisha.
Mungu amempa mwanadamu uwezo wa kuchagua kile atakacho, hakuona sababu ya kukutafutia na kukulazimisha umuoe fulani wakati wewe humtaki. Ndio maana akasema utatafuta wakufanana na wewe. Si kazi yake kukutafutia mke. Baada ya kupata mke kazi yake ni kukupa watoto kwa jinsi utakavyo wewe. Suala la kuwalea lipo juu yako. Sasa Watu wanachanganya madesa kuwa kila kitu ni mipango ya Mungu jambo ambalo si kweli, na kama ni kweli basi Hakuna Hukumu.
Mungu anampa mamlaka Mwanaume kumtoa mwanamke/mke asiyepata kibali kulingana na muono wake. Mwanamke anahaki ya kupewa talaka kama hati itakayomruhusu aolewe na mwingine. kumaanisha bila talaka mwanamke hajapewa kibali cha kuolewa tena.
Sasa Watu wanachanganya maandiko, hawajui kila kitabu kinadhima yake. Vipo vitabu vya sheria, hivi vinajitegemea na vinaeleza mwanadamu aishi vipi duniani. Yani hivi ni kama Katiba. Dhima yake kubwa ni kuelezea sheria za Mungu. Vitabu vingine vinaunga mkono sheria hizo na kutoa mafundisho mengine na unabii.
Sasa Mtu sheria inasema Kwa mfano: Mtu asile chakula fulani. Mtu anatoa kifungu kutoka katika aya za injili au Zaburi, au vitabu vya unabii. huu ni upuuzi ambao Wakristo wengi wameingizwa mkenge. Huwezi vunja Torati kwa kutumia vitabu vya injili au zaburi.
Talaka ni muhimu ikiwa ndoa imekuwa chungu. Mwanamke kama hamuheshimu mume wake, endapo mumewe ataamua kutoa talaka asilaumu kwani anahaki na ni wajibu wake kufanya hivyo.
Hizo zingine ni porojo za kidunia. Eti alichokiunganisha Mungu Mwanadamu asikitenganishe. Hii nukuu imechukuliwa tofauti sana. Mungu akiunganisha kitu hata mwanadamu afanyeje hawezi kukitenganisha na Mungu akikitenganisha kitu Mwanadamu hata afanyeje hawezi kukiunga. Ndoa haipo kwenye listi ya vitu vilivyoungwa na Mungu. Bali ni makubaliano baina ya mke na mume. Endapo ndoa ingeunganishwa na Mungu isingewepo sheria ya talaka kwenye Biblia au Quran. Na pia ndoa zisingefunjika kamwe.
Nawasilisha
NAKARIBISHA POVU