TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

.....wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?



Hili wakilifuatilia katika mihimili yote ya dola..sijui ni wapi watapona!
Kama kuna auditors humu JF proove me wrong.
 
Wakuu, rushwa ni kosa kama makosa mengine you need to prove beyond reasonable doubt. Hata kama ni kweli dalili zote za mazingira ya rushwa lakini hakuna concret evidence, then mla rushwa anaachiwa huru to take the advantage of benefit of doubt. Hivi ndivyo alivyo achiwa kamanda Zombe na wenzake huku wafanya biashara ni kweli wameuwawa na polisi.
Hivyo ndivyo ilivyo rushwa ya Richmond jamani Hosea hakuona rushwa pale sasa mnataka kulazimisha?. Mbona hata kwenye rada hakuna rushwa ndio maana hata mashitaka ya vithlani siyo rushwa.
Amini amini nawaambieni, hata Liyumba anaonewa bure sambamba na kina Mramba they all clean kama kama kiranja wao Mr. Clean-Mkapa

Pasco.. kwani ni nani aliyedai kuwa Richmond imetoa rushwa hadi kulazimisha PCCB kuchunguza?
 
Hili wakilifuatilia katika mihimili yote ya dola..sijui ni wapi watapona!
Kama kuna auditors humu JF proove me wrong.

ndio maana suala la posho lingeangaliwa kimfumo mzima. Ni taasisi ngapi zinalipa posho za mambo mbalimbali? mwaka jana watumishi wa ATCL waliojitokeza kuandamana siku ya Mei Mosi walilipwa posho ya shilingi elfu ishirini kila mmoja kwa kuandamana!
 
Tatizo lako una kaujeri jeuri flani hivi. You need to have a spirit of humbleness in you if you want to go further in your political career.

Mimi nimekuuliza wewe unajuaje hao wabunge wanafanya kama ulivyodai wanafanya. Wewe ukanijibu unajua. Kunijibu kuwa unajua hujajibu swali langu. Jibu swali, wewe umejuaje wanafanya hivyo? Siyo swali gumu hili.

And does it matter if you are clean or not? Of course it does. You can't be throwing all these stones while you live in a glass house.

And don't get it twisted. I know good and well that two wrongs don't make a right.

julius open your mind kidogo kujua kitu sio lazima uwe unahusika ama auhusiki lete hoja kama unakubaliana au la.
 
- Mkuu Fundi, hatuwezi kukoroma tu for the sake of kukoroma ili tuonekane tunakoroma bila kujua sheria iliyovunjwa, kila mwananchi yuko innocent until proven otherwise na hakuna aliyejuu ya sheria wala aliye chini, ingawa that is not the case na taifa letu,

- Hili suala zima linachekesha kwa sababu hatuambiwi ukweli wote, sheria iliyovunjwa haihitaji haya yote tunayoyaona yanatendekea, na ukizingatia kwamba Hosea anatakiwa kuwajibishwa kutokana na ushauri wa ripoti ya wabunge hao hao anaowaandama sasa kuhusu posho!

- Sasa hapo inakuwa sio kukoromeana tu bali wote tunashuka hadhi as a nation.

Ahsante.

William.

Mkuu William! Tunaingia kwenye mtego tukingojea ushahidi wa sheria kuvunjwa. Hao wanaotoswa uingereza sio kwa sababu walivunja sheria bali ilitambulika kuwa vitendo walivyofanya vilionyesha kwamba morally corrupt. Kwa mfano ingawa waheshimiwa walijipitishia sheria kuruhusu walichoita takrima kila mmoja alijua kuwa ilikuwa ni pathetic attempt ya kumwagia pafyum kilo kilichooza. Hata kama hakuna sheria inayowakataza kuchukua posho hata kumi kutoka kwa watu wanaowasimamia lakini morally wamejithibitisha kuwa ni wachafu. Na watu kama hawa hawastahili kupewa heshima ya kutuwakilisha.

Kuchanganya hoja ya Hosea ili kujaribu kufunika maovu wanayoyafanya si sahihi. Kila mtu anajua kuwa ingekuwa bora zaidi kama wenyewe wangeweza kuwekana sawa. Lakini kutokana na majibu ya hao waliowachagua kuwaongeza ni wazi kuwa hawana hata chembe ya nia kufanya hivyo. Sense yao ya entitlement ni kubwa mno. Ndio maana nilishauri kuwa wale wabunge ambao hawapendezwi na tabia hii wainuke na kuwataja wale wote wenye haka kamchezo. Pengine wachache wao wataona aibu na kujirekebisha. Na muhimu zaidi pengine wapiga kura wao wataipa uzito unao stahili kura yao na kuchagua watu walio waadilifu badala ya hawa ambao wanaowachagua kutokana na mazoea.

Amandla........
 
julius open your mind kidogo kujua kitu sio lazima uwe unahusika ama auhusiki lete hoja kama unakubaliana au la.

Sawa, kujua kitu sio lazima uwe unahusika moja kwa moja na hiko kitu. Mimi nilichouliza yeye huyu mheshimiwa kajuaje hicho alichodai. Ila naona mheshimiwa is too big to answer my question and has decided to ignore me. It's all good...I ain't gonna lose or gain a pound over it.
 
Zitto hawezi kumwaga Mpunga juu ya source ya hoja yake juu ya wabunge kuforge risiti! kaka si kila kitu utaelezwa ati kiunagaunaga! Kwani wewe hujui Waheshimiwa wetu wanavyopigaga vibomu watu? Na kama Mh. hapa anasema anajua na yuko kamati ya Fedha, unabisha nini? Au ndo mmetumwa na Makamba mje kupeleleza watu humu ndani?
 
hakuna kitu kinachoweza kuhalalisha kitendo cha TAKUKURU; wamevuka mpaka wa hatari sana na ni lazima HOsea kama ana chembe ya uwajibikaji basi aachie ngazi. As a matter of fact, Bunge linatakiwa kuing'oa PCCB kutoka chinii ya ofisi ya Rais..
 
hakuna kitu kinachoweza kuhalalisha kitendo cha TAKUKURU; wamevuka mpaka wa hatari sana na ni lazima HOsea kama ana chembe ya uwajibikaji basi aachie ngazi. As a matter of fact, Bunge linatakiwa kuing'oa PCCB kutoka chinii ya ofisi ya Rais..

Hata kama walialikwa? Hata kama wanachochunguza ni makosa ya jinai?

Amandla........
 
Takukuru wanaweza kuwa sahihi lakini timing yao ndiyo inatia kichefuchefu - inaufanya uchunguzi mzima uwe ni ufisadi in its own right! Labda wasimamishe liishe hilo la Richmond ndio waanze uchukuzi makini kuanzia mwanzo wa ENZi sio juzi tu! Waanze na akina JK wakiwa wabunge ili na akina Pinda na wengine wasafishwe! Waende mpaka kwenye vikao ya ndani vya mashirikani (eg senates kule vyuoni) - ili tuone kwa nini mwalimu au mwanafunzi ahudhurie kikao halafu alipwe pesa - kama wataiona rationale basi tutafute muafaka wa kitaifa! La sivyo, tukikubali kufuata kila upepo, tutaishia kupoteza mwelekeo! Lazima tujue ku prioritise!
Ni kweli TIMING MBOVU ila hoja ipo.. tatizo la wabunge vigeugeu (wa CCM) kushabikia miswada mibovu ya serikali kama kuwepo kwa Takukuru chini ya ofisi ya Raisi na mkuu wa Takukuru kuteuliwa na raisi bila hata uthibitishoo wa bunge (kamati)..

mwakyembe umesoma na kufundishaa sheri ila bado unaushabikii katika hata mioswadaa mibovuu ili mradi unalinda serikali na chama chako..BADILIKENI.
 
Bhaghosha,

Vote of no Confidence with MP inakuja very soon msihofu na ndilo hilo linalowatisha IKULU wakijua fika kibarua kinaota majani, Kaeni mkijua serikali inajua vyema jinsi ya kutuyumbisha muda wote huo toke 1979 iyo posho 2 ipo al over the suddny wamekuja na iyo issue yao wanadhani sie ni mambumbumbu nini?? wanajipotezea muda na kujiwekea maisha ya watoto wao pabaya ni meisha waonya na kuwaambia Rwanda na Burundi ilianza chokochoko kama hizi na viongozi wakapuuzi kilichotokea buuuuuummmmm Vita ndiko huko viongozi wetu wanatupeleka.

kwani wameshindwa kututoa mahali tulipo kwa ajili ya maslahi yao binafsi hawaju chakurekebisha ni kipi nanikipi cha kufanya nchi isonge mbele. Ukweli ni kwamba nchi iko nyuma sana kimaendeleo ilo liko wazi na serikali hii haicha move hata step mbili mbele
 
Yaani watanzania tumeishiwa kiasi hiki mpaka tunafikia kuhalalisha UOZO wa posho tunazozipigia kelele hapa kila siku just kwa sababu tunadhani kuwa kufanya hivyo kutawaumiza MASIHA FEKI wetu....Credability haijengwi na tunayoyasema majukwaani bali matendo yetu ndiyo nguzo muhimu ya uaminifu kwa wananchi. Tuache uvivu wa kimatumaini na tuamini kuwa tunaweza kuwa na harakati za kweli zitakazoongozwa na watu walio wasafi na wenye kuamini kwa dhati yale wanayoyatetea na sio kuangalia umaarufu na nafasi zao kisiasa tu....

omarilyas

Huyu Masiha feki unayemzungumzia hapa ni nani?
 
Wakuu zangu ebu nifahamisheni kitu kimoja..
Hili swala la posho mbili kwa kazi moja linakuja vipi haswa maanake nasikia kinachodaiwa ni pale Wabunge wanapolipwa posho ya siku bungeni kisha hao wa kamati wanapotembelea wizara, mashirika au taasisi za serikali hudai posho kwa semina hizo.
Ikiwa hivyo ndivyo, mimi sioni ubaya wake hata kidogo ikiwa baada ya Bunge kufungwa, kuna wabunge wanarudi mahotelini, na wengine wanaendelea na kazi kuhudhulia hizo semina sasa iweje malipo yawe sawa?...

Kisha Bunge linapofungwa kwa siku hiyo, sii ndio halali ya malipo posho hizo yanapolenga kikazi jamani au vipi? Je, wale wabunge wanaomaliza bunge na kwenda funga deal kwa Pc mahotelini haihesabiki kwamba nao wameingiza fedha kinyume cha sheria maanake wameisha lipwa na Bunge iweje watumie muda wa siku hiyo kufanya madeal yao!.. yaani mimi naona kama ni ujinga mtupu hili swala la posho mbili ikiwa kweli kinachoendelea ndio kama nilivyosikia.

Wakuu zangu nipeni somo hapa, nachoweza kusema mimi labda tuzungumzie kiwango wanacholipwa lakini kama serikali yenyewe ina fungu la kulipa hizi Posho na wabunge wanaelewa wazi kila wizara, shirika au taasisi ya serikali ina fungu la Posho kwa ajili ya semina zao.. kwa nini wasiombe posho zao, kwani hata wakiacha wizara itatafuta matumizi ya kijinga na pengine hata ku forge risiti kuchukua hizo posho...
Navyofahamu mimi hata viongozi wa serikali wanapokwenda wilayani hudai wahudumiwe na mfuko wa wilaya hizo, nakumbuka hata Dr. Slaa amewahi kuwatoa nishai kule jimboni kwake na ikawa swala zito sana. Dr. Slaa alikataa kulipa iweje wizara, mashirika na taasisi za serikali wanashindwa kukataa kulipa posho hizo hizo..
 
Mkuu Mkandara.
Kinachogomba hapa si posho za vikao vya bunge kwa namna unayozungumzia. Mbunge anapewa posho ya kikao kwa kuhudhuria kikao husika. Kama hajahudhuria kwa sababu yeyote ile hastahili kulipwa posho hiyo. Kinachodaiwa ni kuwa kuna baadhi ya wabunge ambao wenzao huwasainia kuwa walikuwepo kwenye vikao wakati hawakuwepo ili wasikose posho ya siku hiyo.
Kulipwa posho mara mbili kunatokea hivi. Moja ya majukumu ya kamati za bunge ni kutembelez na kukagua wizara na mashirika ya umma yanayoangukia chini yake. Kwa vile wanakuwa nje ya vituo vyao vya kufanyia kazi basi wabunge wanalipwa na ofisi yao posho ya kujikimu wakiwa safarini na gharama za usafiri kwenda na kurudi kutoka sehemu zinazohusika. Baadhi ya wabunge hao wanapofika huko wanakokwenda wanadai/ wanapokea posho nyingine za kujikimu wakiwa safarini. Wakati mwingine wanarudishiwa tena gharama za usafiri. Huu ndio moja ya udanganyifu unaofanywa.

Amandla......
 
Shukran mkuu wangu kwani baada ya kuona mada moja humu ikizungumzia jinsi hizo posho mbli zilivyotolewa nikauliza mtu wangu naye anakanimbia ndio hivyo imetokea...Sasa ikiwa bunge linawapa posho kwa ajili ya kutemeblea hizo wizara kisha wakafika huko na kudai posho nyingine hapo kweli ni kinyume kabisa cha sheria na inabidi wafuatiliwe kwa makini lakini sio kosa la RUSHWA kwa sababu rushwa wahusika huwa ni wote wawili - Mtoaji na Mpokeaji.. Hapa Wabunge hutumia udanganyifu hivyo wanachotakiwa ni kurudisha fedha hizo including a fine, na pengine hata kuchukuliwa hatua za makosa ya Udanganyifu.
Nionavyo mimi hii sio kazi ya PCCB kabisa kwani haiangukii ktk kifungu chochote cha aina za Rushwa.
 
Mkuu Mkandara.
Kinachogomba hapa si posho za vikao vya bunge kwa namna unayozungumzia. Mbunge anapewa posho ya kikao kwa kuhudhuria kikao husika. Kama hajahudhuria kwa sababu yeyote ile hastahili kulipwa posho hiyo. Kinachodaiwa ni kuwa kuna baadhi ya wabunge ambao wenzao huwasainia kuwa walikuwepo kwenye vikao wakati hawakuwepo ili wasikose posho ya siku hiyo.
Kulipwa posho mara mbili kunatokea hivi. Moja ya majukumu ya kamati za bunge ni kutembelez na kukagua wizara na mashirika ya umma yanayoangukia chini yake. Kwa vile wanakuwa nje ya vituo vyao vya kufanyia kazi basi wabunge wanalipwa na ofisi yao posho ya kujikimu wakiwa safarini na gharama za usafiri kwenda na kurudi kutoka sehemu zinazohusika. Baadhi ya wabunge hao wanapofika huko wanakokwenda wanadai/ wanapokea posho nyingine za kujikimu wakiwa safarini. Wakati mwingine wanarudishiwa tena gharama za usafiri. Huu ndio moja ya udanganyifu unaofanywa.

Amandla......

Fundi Mchundo; Waziri Mkuu ni Mbunge. Je anapokea posho ya mafuta ya magari ya wabunge?
 
wanajipotezea muda na kujiwekea maisha ya watoto wao pabaya ni meisha waonya na kuwaambia Rwanda na Burundi ilianza chokochoko kama hizi na viongozi wakapuuzi kilichotokea buuuuuummmmm Vita ndiko huko viongozi wetu wanatupeleka.

Hivi ni vitisho mkuu, hujui kilicho nyuma ya Rwnada na Burundi.
 
Ninyi mnadhani ni posho za kawaida. Subirini uchunguzi ukamilike. Kelele za nini kuzuia uchunguzi huu? Hakuna aliyewekwa ndani, hakuna aliyefunguliwa mashtaka, hakuna aliyekamatwa, ni uchunguzi tu! Mnataka kuwaweka kundi gani Wabunge wetu?
Nchi inatafunwa hii jamani; mbele, nyuma, kushoto,kulia, juu na chini. Wanasiasa wetu ndio CHANZO cha madhila yote haya.
 
Tukikubali hata kinadharia kuwa chombo cha utendaji kinaweza kuanzisha na kuendesha uchunguzi dhidi ya mbunge au kundi la wabunge tutakuwa tumekubali jambo la hatari sana. Itakuwaje huko mbeleni polisi au uwt wakiona wanajadiliwa vikali bungeni wakaanzisha uchunguzi ambao utawazuia wabunge wakali kushiriki mjadala bungeni? Na vipi kama kura ya kutokuwa na imani na WM inatarajiwa kupigwa na mara wabunge kadhaa wanasombwa kusaidia uchunguzi na kuondoa wingi wa kura zinazohitajika? Tukiwakubalia kwa wabunge nani atawazuia ikija kwa majaji?


Mkuu Mwenzangu Mwanakijiji,

Hizo ni nadharia tu na hii inaonesha ni mapenzi gani uliyonayo na yakiyo kubuhu kwa Mwakyembe.Naomba kukwambia kuwa Unapenda sana ushabiki na hili nilishakuonya muda mrefu na hautaki kuliacha.

Sauala la mwakyembe kuhojiwa halina uhusiano wowote na kwamba itafikia stage watu watanyamazishwa.Mwakyembe kachukua posho mara mbili which ni wizi kama anavyosema zito na mimi namuunga mkono zito

Cha msingi ,Mwakyembe ahojiwe na kama vipi afunguliwe mashtaka ya Rushwa.Hatuwezi kuwa na watu ambao hawashikiki eti kisa ni kamamnda wa ufisadi.

ukamanda gani huo wakati hata ubunge alioupata aliupata kwa kutoa Rushwa.au ukamanda ni kwa ajili ya watu wachache ambao yey hawapendi?

Mpaka sasa naunga Mkono Dr. Edward Hoseah na PCCB kuwa jamaa ahojiwe na afikishwe mahakamani kwa kukika sheria ya Rushwa ya mwaka 2007.


kuhusu Kinga ya Mbunge,Kinga ipo katika hoja za bunge tu na siyo kwenye tabia ya kula posho mara mbili.
 
Back
Top Bottom