TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 28, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tukikubali hata kinadharia kuwa chombo cha utendaji kinaweza kuanzisha na kuendesha uchunguzi dhidi ya mbunge au kundi la wabunge tutakuwa tumekubali jambo la hatari sana. Itakuwaje huko mbeleni polisi au uwt wakiona wanajadiliwa vikali bungeni wakaanzisha uchunguzi ambao utawazuia wabunge wakali kushiriki mjadala bungeni? Na vipi kama kura ya kutokuwa na imani na WM inatarajiwa kupigwa na mara wabunge kadhaa wanasombwa kusaidia uchunguzi na kuondoa wingi wa kura zinazohitajika? Tukiwakubalia kwa wabunge nani atawazuia ikija kwa majaji?
   
 2. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kutakuwa na mkanganyiko katika utendaji wa taasisi za dola iwapo tutaruhusu viongozi wa taasisi moja wanaotuhumiwa kutenda makosa na taasisi moja inapolipa kisasi kwa kuanzisha uchunguzi kwa chombo husika kwa kisingizio kuwa kinatimiza wajibu wake. Kwa nini wasisubiri hukumu itolewe ndipo nao wajipe kazi kama wanaoona inashihi.
   
 3. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #3
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kaka unajua Mramba alihojiwa na kufikishwa mahakamani akiwa Mbunge? Unajua stori ya yule mbunge wa Morogoro aliyeburuzwa na Landrover la Polisi kwa madai ya Maji? Hawa nani alikuja hapa kuwatetea na kusema tawi la utendaji lisiingilie Bunge?

  Kuna tatizo la msingi katika Taifa letu na katika mfumo wa Bunge. Fanya tafiti zako, ni Bunge la Tanzania tu duniani ndilo halina utaratibu wa kudhibiti mienendo ya Wabunge. Nchi nyingine wana mtu anaitwa Kamishna wa mienendo (Office of the Commissioner for standards). Huyu huchunguza mienendo na ile ambayo ni ya kijinai huenda katika jinai na ile ya kimaadili (hili la posho ninadhani ni la kimaadili) linakwenda kamati ya Maadili na kisha Bunge kutoa adhabu.

  Mwaka 2004 Sheria ya maadili ilirekebishwa ili Bunge lipitishe 'code of conduct' kwa wabunge. Mpaka leo hatujapitisha. Mwaka 2008 niliwasilisha muswada binafsi ili kuunda code na kisha kuunda ofisi ya Kamishna huyu. Mpaka leo Ofisi ya Spika imekalia muswada huu na kukataa kuupeleka kuwa gazzetted ili ujadiliwe Bungeni.

  Hivi MwanaKijiji unajua wabunge wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?

  Tunafanya makosa, halafu hakuna code wala mamlaka ya kutuchunguza halafu tuachiwe. Hapana. Mwanakijiji wewe kwa heshima yako hupaswi kutetea uvunjifu wa maadili.

  Waache TAKUKURU wafanye kazi yao. Lazima Wabunge tujue kuwa hatupo juu ya sheria na kwamba tupo accountable na answerable kwa vitendo vyetu (for actions and inactions).
   
 4. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #4
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Usipotoshe. Uchunguzi ni wa muda mrefu. Umekuwa public hivi karibuni tu. TAKUKURU kimsingi chombo cha dola chini ya Ofisi ya Rais (Head of State). Head of State yupo juu ya mihimili yote mitatu. Rais kama Head of the Executive ndio mhimili mmoja. Lakini kama Mkuu wa Nchi ni mlinzi wa Katiba na sheria zilizotungwa kwa mujibu wa Katiba. Mbona Tume ya Maadili ya Viongozi inaendesha zoezi la kuchunguza mali za wabunge kwa kutuita na kutuhoji hamna kelele.

  Msitetee uhalifu. Acheni tuhojiwe na kama tuna makosa tuwajibike. Hakuna visasi hapa!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Oct 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Wewe umejuaje wanafanya haya yote? Ni mmoja wapo?
   
 6. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #6
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mimi najua.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Oct 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Ahaaa....unajua kwa sababu ni mmoja wao. Kama si mmoja wao sema umejuaje.
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yote haya ni kupunguza kasi ya kuifatilia Richmond...
   
 9. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Takukuru wanaweza kuwa sahihi lakini timing yao ndiyo inatia kichefuchefu - inaufanya uchunguzi mzima uwe ni ufisadi in its own right! Labda wasimamishe liishe hilo la Richmond ndio waanze uchukuzi makini kuanzia mwanzo wa ENZi sio juzi tu! Waanze na akina JK wakiwa wabunge ili na akina Pinda na wengine wasafishwe! Waende mpaka kwenye vikao ya ndani vya mashirikani (eg senates kule vyuoni) - ili tuone kwa nini mwalimu au mwanafunzi ahudhurie kikao halafu alipwe pesa - kama wataiona rationale basi tutafute muafaka wa kitaifa! La sivyo, tukikubali kufuata kila upepo, tutaishia kupoteza mwelekeo! Lazima tujue ku prioritise!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Julius ndugu yangu. Unauliza pua iko wapi wakati unauona mdomo?

  Kumbuka kuwa Zitto ni mbunge na kama sikosei yuko kamati ya fedha.

  Zitto tuko pamoja kabisa. Mie nasema TAKURURU waendeleze zoezi lao na Wabunge nao waendeleze zoezi lao la kuchunguza Richmonduli na TAKURURU na ikibidi madude mengine ingawa sidhani wabunge wa CCM watakubali maana huko itakuwa kujitia kitanzi wenyewe.

  Hilo joto la hii FRICTION ndiyo linaweza kuibadili MILELE Tanzania. Watu ifike sehemu waanze kuheshimu mali ya uma. Kwa upande wangu simuonei huruma Mwakyembe wala HOSEA. Kama wamekosa basi wao wote na hata Pinda/Kikwete kama walilamba, basi hizo pesa WAZIRUDISHE.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Oct 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Unaamini Zitto yeye yuko msafi na hafanyi kama anavyodai wengine wanavyofanya?
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kuna zile habari nyingine juu ya Mwakyembe, Zitto kaandika kuwa uchunguzi umeanza tangu mwezi wa pili kwa kuwahoji makatibu wa wizara na mwezi wa Mei wakaanza kuhojiwa Wabunge. Hivyo siyo kitu kigeni kbisa Tanzania. Sema kimekuja kujulikana tu mara Mwakyembe alipogoma kuhojiwa na kama angelikubali si ajabu wala tusingelisikia.....
   
 13. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #13
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Does it matter? Kama na mimi nafanya nishughulikiwe tu. To you WRONG+WRONG=RIGHT
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako una kaujeri jeuri flani hivi. You need to have a spirit of humbleness in you if you want to go further in your political career.

  Mimi nimekuuliza wewe unajuaje hao wabunge wanafanya kama ulivyodai wanafanya. Wewe ukanijibu unajua. Kunijibu kuwa unajua hujajibu swali langu. Jibu swali, wewe umejuaje wanafanya hivyo? Siyo swali gumu hili.

  And does it matter if you are clean or not? Of course it does. You can't be throwing all these stones while you live in a glass house.

  And don't get it twisted. I know good and well that two wrongs don't make a right.
   
 15. M

  Mbala-mwezi Member

  #15
  Oct 28, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Nakupongeza Mh Zitto kwa ujasiri wa kukubali PCCB iwachunguze wabunge ilhali wewe ni mmoja wa wabunge. Hiyo ndio misimamo ya viongozi tunaowataka...nakumbuka Nyerere aliwahi kupunguza mshahara wake kabla hajaruhusu kupunguza mishahara ya mawaziri,nk....uongozi ni kuwa tayari hata kusimamia maamuzi machungu kwa ndugu, jamaa, rafiki na hata maisha yako mwenyewe ili kuweka misingi imara kwa hatma ya taifa.

  2. Mwanakijiji naamini una hoja ya msingi kwa unachokisema, lakini kumbuka kwamba hakuna mfumo usio na mapungufu...mapungufu ya hoja unayopendekeza ni ujenzi wa tabaka fulani katika mihimili ya dola lisilo hojika wala kuwajibika kwa miendo yao...huu ni upungufu mkubwa. zinaweza kuwekwa taratibu za viongozi fulani kuhojiwa lakini hatuwezi kuacha wazi wafanye wanavyotaka...kama tunajadili kitaalamu, sio kwa hisia!...nasema tusijadili kwa hisia kwa sababu tuna wabunge kama kina mwakyembe ambaye yeye kila anapotuhumiwa kwa masuala ya msingi anasingizia"kusakamwa kwa sababu aliongoza kamati ya richmond" sasa nchi haiwezi kuenmdeshwa hivi jamani....

  3. Naunga mkono hoja ya zitto ya kuwa na ofisi ya kamishna wa mienendo....afu ndio maana nakukubali sana zitto, yani kila unapopinga au kuunga mkono hoja unatoa mapendekezo...hii nzuri sana kijana....huna siasa za kulalama lalama tu....UNAPENDEKEZA, safi....nadhani utafika mbali muda si mrefu
   
 16. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,086
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Zitto nadhani hoja yako ni sahihi. Hata hivyo, unatakiwa kufahamu kuwa kuwajibika kwa viongozi na uongozi hakupaswi kuwa jukumu la watendaji wa dola, yaani serikali. Huu ni upungufu wa kisera. Kushughulikia mbunge mmoja mmoja leo au kesho, hakuwezi kuwazuia watendaji/maofisa wa serikali wasifanye hayo hayo. Tunafahamu fika kuwa maofisa wa serikali, takriban wote, wanaishi kwa hizo posho. Na ndiyo maana wanakuwa wa makini kuhakikisha kuna posho za kutosha katika bajeti mnazi pitisha kila mwaka. Kwa maana hiyo hili haliwezi kuwa suala la TAKUKURU. Iwekwe sera bayana kuwa maofisa wa serikali na wabunge sawia wasipewe posho ila mishahara, basi! Vinginevyo mtu atajiuliza:

  Hizo posho walizolipwa wabunge zilikuwa kwenye bajeti?

  Iwapo, hivyo hiyo pesa ingewekwa wapi kama wabunge husika wasingelipwa?

  Kama haikuwemo katika bajeti MDA husika, hilo fungu lilichotwa wapi wapi na kuidhinishwa nani, na kwa maslahi gani?

  Nani amewajibika kuhusiana na hilo?

  Nadhani maamuzi ya kisera hayapaswi kuwa ya 'tuanze' na fulani au 'nikamatie' fulani.

  Na ninadhani hali iko hivyo katika maeneo mengi ya kisera serikalini. The policy are are too discretionary intending to give sweeping powers of manupulations to government officials' and their accomplices. Kwa mfano, angalia TRA na mfumo wake wa misamaha ya kodi. Ukiwa kijana mzuri kwa watawala, nobody cares about your mess, ila ukikosana nao kidogo tu, kesho ofisa wa TRA yuko dukani kwako. Huu ni mfumo wa ovyo hatupaswi kuutetea hata kama umewabana wabaya wetu.
  Mwiliwe
   
 17. M

  Mbala-mwezi Member

  #17
  Oct 28, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Mimi nadhani unamwonea zitto...hilo sio jibu la jeuri...ni jibu la utayari wa kuwajibishwa kama anakwenda kinyume....kwasababu WRONG+WRONG=RIGHT?....sasa ulitaka akubembembeleze badala ya kujibu hoja?...acha zako hapa! jenga hoja kiume!
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Oct 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Swali nililouliza ni jepesi mno. Nimeuliza yeye kajuaje baadhi ya wabunge hufanya hivyo? Nikupe mfano, angeweza tu kusema kuwa nimeambiwa, nimeshuhudia, nimewahi kufanya, n.k....lakini siyo kunjibu "najua". Heck..I didn't ask if you know, I asked you how do you know?
   
 19. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Naomba niulize maswali.
  1. Hivi hizo hela wanazodaiwa wabungu kuchukua zilikuwa zinatolewa na nani?
  2. ni ni kwa ajili ya nini?
  3. na aliyekuwa anawapa alipata ruhusa wapi?
  3. na zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya nini?
  3. halafu hizi pesa zimeanza kutolewa lini?
  4. Je aliyetoa hizo pesa amehojiwa?
  5. Je wabunge walikuwa wanadai au walikuwa wanapewa tu?
  6. Pinda na JK walishapokea kiasi gani wakati wakiwa wabunge?
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wabongo tunapenda kupongeza mno hata ujinga sisi ni kupiga makofi tu!

  mwingine

  Athali za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti bado hazijafutika....poleni watzania wenzangu!
   
Loading...