TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

Mwenzako ni mheshimiwa mbunge, kodi yako unamlipa mshahara kila mwezi! pole we!. Kama unamwongelea Zitto na hakuna anayekuongelea wewe nji hii, mkuu ujue kakuacha sana, na kinachoonekana kwako ni wivu tu, nothing else lakini sio mitazamo tofauti, hii sio Dowans, hii ni thread nyingine kuleta mambo ya Dowans huku ni kuwa na kihoro na kijiba cha moyo mkuu ebu jiangalie tena. ebu anzisha thread wewe na aanzishe Zitto uone nani watachangia sana! Duhu!

Duh,

Naona sasa JF imekuwa kama michezo ya kidali poh. Yaani mkuu waberoya umeamua kuongea utumbo kiasi hiki. Kwamba unaleta michezo ya kitoto ya kutaka kuonekana nani popular vile. Yaani mambo yale ya high school kind of.

Mf:

Waberoya -- baba yangu anamzidi baba yako
Zitto -- no, baba yangu ni bora kuliko baba yako
mwanajf mwingine -- baba yangu ni askari polisi wakati baba yako ni mlinzi

waberoya -- baba yangu akitoka kuoga nyumba yote inajaa moshi
Zitto -- nyie hamnijui mimi kuwa ni mbunge kwa hiyo baba yangu ni mdosi.

mwanajf mwingine -- acha hizo wewe, ndio maana una koti la njano.
waberoya -- nyie wote na baba zenu mkichanganywa na maji mnabaki maji tu
kengele inagongwa na watoto wanakimbia kurudi darasani.



Kuna watu tunapingana thread moja na kupatana thread nyingine!, this is how life is in JF , mkuu umebakia na Dowans vithibitisho huna(kasema vitoeni), nenda mwenge pale kanunue nguo mpya! hujasema hili la posho kama kapatia ama kakosea unabaki amefulia! aibu hii.

Zitto yuko very familia na jina langu, nampinga na niligombana naye sana swala la ruzuku, na anapotoa point nampa credibility yake, lakini sina kinyongo naye , I too making mistakes sometimes!

Unajua wakati nakua nilielezwa wambeya dunia hii ni jinsia ya kike, siku hizi ideology hii siikubali tena!

Haya ya umbea na jinsia za kiume na kike sijui yameingia vipi hapa? Au ndio kuishiwa huku?

Mchukie mwenyewe na familia yako, wengine hatumo huyu kijana kafanya remarkable changes and moves nyingi ndani ya bunge kiasi ambacho wewe hutaweza kufanya katika maisha yako yoote achilia mbali ukoo wako


wakati huo huo wakati wakiwa darasani ***

waberoya -- unajua ukoo wetu ni mkubwa kuliko wa mwalimu sayi?
Zitto -- acha hizo wewe, ukoo wangu unazidi wa kwako na mwl Sayi.

*** Mwl Sayi -- hivi nyie hapo si mnyamaze?

Huyu Zitto alitaka kunipindua mimi na serikali yangu(nikiwa waziri) DARUSO kwa madai ya tunabebwa na uongozi wa chuo, yet I have no any enemity with him! neither that I will have

Waberoya -- sawa mwl tutanyamaza baada ya huyu chakubanga hapa
mwanajf mwingine -- unamwita nani chakubanga?
waberoya -- wewe hapo na baba yako polisi

*** Mwl Sayi -- nyie watoto acheni bange zenu


Kuna watu mpaka mnaboa! nimekaa sana uchagani miaka sita, nimesoma Umbwe, Moshi Technical na Old Moshi, I know history of people over there , najua ni nani wana hasira ya kuua mtu, ni nani wapole maana wachaga ni mjumuisho wa makabila madogo madogo mengi na wanaongea lugha tofauti

Kwa haraka haraka ile point yako ya uchaga nimeshajua wewe ni wawapi na ndio maana unahasira sana

Waberoya -- hapana mwl, siyo bange, ni bangi
Mwl Sayi - what.......ever!!!!!!!!

Ungekuwa na uwezo wa kuona na na Zitto haraka haraka ungeweza hata kumchoma kisu!

Nikiendelea na analysis wewe ni mzee ki-umri kuliko hata Zitto maana ndiye pekee wenye damu za kizamani, damu mpya ya wachaga yaani kizazi kipya hawana hizo tabia za hatred!

Waberoya (huku akimgeukia Zitto) -- au wewe unasemaje?
Zitto -- je kwenye nini?
Waberoya -- ni bange au bangi?
Zitto -- ni bange

Mkuu nimeoa kwenu(Kilema) usishtuke, mimi mnyaki ukisema wanyaky wanapenda wanawake nitacheka na kusema ok, nikisema wakibosho kama wewe visu mkononi! usishtuke pia, nikisema wamarangu wanapenda maendeleo, warombo wasomi, wamachame wafugaji yet, wanatananiwa wanawake wao wanapenda fedha , Hizi story zipo mkuu, lakini tunasihi kwa raha.Zitto angetukana wachaga kama ulivyosema hili hali yuko Chadema, hata wachaga wenzako ukiwaambia hili wanakuwa confused! anyway hakuna mchaga mwenye akili ata-incline na wewe!


Waberoya -- wewe nawe sasa unaniangusha

Flap flap flap flap (mwl Sayi anasogea taratibu)

*** Hivi nyie mna matatizo gani?

Zitto -- sio mimi mwl, ni hawa wachagga (huku akinyoosha kidole)
Mwanajf mwingine -- mimi sio mchaga, mimi ni msukuma

Waberoya -- si ulisema wewe mnyaki?

***** makelele kibao hata hawaeleweki ...

Zitto -- Nani kasema yeye mnyaki?

Waberoya -- sio wewe mheshimiwa zitto, ni huyu mtoto wa polisi!
Zitto -- ah haaa

Kusema kuhusu kabila mkuu umeweka moyoni kiasi hicho( na alisema nini, alikuwa kwenye mood gani, wewe haukosei??), Tanzania hii, kila kabila linasemwa kwa tabia yake mbaya, ambayo imegeuka visifa zama za leo!

Kizazi cha sasa hatuzungumzii chuki , hoja na facts! after all Zitto hakulishi! why bother
I am assuming that I am writing sms in my cellphone, the moment I send message, it displays


'MESSAGE SENT'

When you send yours I can opt to read or to delete! ila ujumbe umefika.

La mwisho ukumbuke JF ni hiyari si lazima ujibiwe

Mwl Sayi -- Zitto na waberoya, wachaga wamewakosea nini?
waberoya -- simu yangu imeishiwa chaja

Mwl Sayi -- simu ya nini sasa hapa?

Waberoya -- sio lazima ujibiwe..... message sent.
 
Huwezi kutumia historia ya Zitto kwa miaka iliyopita kufanya watu wanyamaze au kupiga vigelegele kila mara Zitto anapoongea (hata kama ni pumba).

Watu hubadilika; Tonny Blair wa uingereza alibadilika sana na kuwa kibaraka wa Bush na MIC. The same thing imetokea kwa Zitto, Zitto wa leo sio yule wa Buzwagi. Zitto wa leo anatetea ufisadi. Zitto wa leo hatoi jibu la moja kwa moja akiulizwa kuhusu hatima ya Buzwagi.

Zitto wa leo hii hajatoa mjadala binafsi tena kama zamani (BTW issue ya Buzwagi ilikuwa ya pamoja kwa viongozi na wabunge wa chadema). Zitto wa leo aliwashambulia wachaga hapa jf na kwenye vyombo vya habari.

Zitto AKA mzee wa Dowans amepoteza credibility na ni watu kama wewe tu ndio mnampigia magoti kila mara mkimwona (on his way to political hell).

Zitto nilimshauri arudi zizini ccm lakin bado hajanijibu, labda anasubiria mwakani baada ya uchaguzi. Si unajua tena atalipwa fadhila kwa kuzima issue ya buzwagi na richmond.
 
Mkuu wangu usifikiri utani hawa jamaa wanakula bata kichizi kiasi kwamba hata viongozi wa huku hushangaa tunapodai Tanzania ni nchi maskini..majuzi tu wameingia jamaa wa madini team nzima yaTaifa stars, sijui wamejificha wapi lakini walipofikia siku ya kwanza mwenyewe nilishika adabu...Maneno ya Mwinyi, ama kweli watamkumbuka JK!

Kweli umaskini wa nchi yetu ni wa kujitakia! Vijisenti vya watu hawa vinawekwa "offshore accounts" sijui kwa kuhofia nini wakati tunazo benki kibao Tz! Laiti kama Azimio la Arusha lingefufuka, lakini wa kulifufua nani? Kaazi kweli kweli!
 
Naomba wenye ujuzi wa Sheria watusaidie jambo moja bayana.
Hivi raia yoyote wa Tanzania anapohisiwa amefanya kosa, wakati huo labda anamatatizo na viongozi wa jeshi la Polisi, mzee Saidi Mwema, au yoyote mwingine mwenye ushawishi. Na hali hiyo ya MIGOGORO BAINA YENU, inakufanya uhisi kuwa huwezi kuhojiwa kwa haki, au zile taarifa wanaweza kuzitumia kwenye migogoro yenu.
Je ninahaki ya kukataa kuhojiwa , na kuomba tukutane mahakamani ambako nitatoa taarifa zangu ? ipi haki yangu ya utoaji taarifa kwa chombo nisichokua na Imani nacho.
 
Naomba wenye ujuzi wa Sheria watusaidie jambo moja bayana.
Hivi raia yoyote wa Tanzania anapohisiwa amefanya kosa, wakati huo labda anamatatizo na viongozi wa jeshi la Polisi, mzee Saidi Mwema, au yoyote mwingine mwenye ushawishi. Na hali hiyo ya MIGOGORO BAINA YENU, inakufanya uhisi kuwa huwezi kuhojiwa kwa haki, au zile taarifa wanaweza kuzitumia kwenye migogoro yenu.
Je ninahaki ya kukataa kuhojiwa , na kuomba tukutane mahakamani ambako nitatoa taarifa zangu ? ipi haki yangu ya utoaji taarifa kwa chombo nisichokua na Imani nacho.

Katika maelezo yangu mwanzo wa thread niliandika kwamba ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 10 (2A) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 (RE, 2002), kukataa wito wa Polisi au mamlaka nyingineyo na adhabu yake ni faini isiyozidi TSh 500,000/= au kifungo kisichozidi miaka 3 jela au vyote faini na kifungo kwa pamoja! Hata hivyo kama unaona kwamba mamlaka inakuita kwa kosa ambalo halipo ila mamlaka hiyo inatumika vibaya, the way out sio kukataa maana unaweza kumpa nafasi mbaya wako kuachana na madai ya mwanzo na kukufungulia mashtaka ya kukataa wito halali! The way out ni kuitikia wito na kama utakuwa na ushahidi ufungue mashtaka kuhusu malicious arrest au prosecution, whatever the case may be! Sasa kama watu watakuwa na uhuru wa kuchagua vyombo vya kuwashughulikia mbona hata mahakama zenyewe zinanuka kwa rushwa na tutakuwa na ahueni ya kutoshtakiwa! Na kama mkwepa wito analalamikia uvunjaji wa sheria mbona na yeye anavunja sheria ambayo kashiriki kuitunga?
 
[FONT="]Mwafrika[/FONT]
[FONT="]Huwezi kutumia historia ya Zitto kwa miaka iliyopita kufanya watu wanyamaze au kupiga vigelegele kila mara Zitto anapoongea (hata kama ni pumba).

Watu hubadilika; Tonny Blair wa uingereza alibadilika sana na kuwa kibaraka wa Bush na MIC. The same thing imetokea kwa Zitto, Zitto wa leo sio yule wa Buzwagi. Zitto wa leo anatetea ufisadi. Zitto wa leo hatoi jibu la moja kwa moja akiulizwa kuhusu hatima ya Buzwagi.

Zitto wa leo hii hajatoa mjadala binafsi tena kama zamani (BTW issue ya Buzwagi ilikuwa ya pamoja kwa viongozi na wabunge wa chadema). Zitto wa leo aliwashambulia wachaga hapa jf na kwenye vyombo vya habari.

Zitto AKA mzee wa Dowans amepoteza credibility na ni watu kama wewe tu ndio mnampigia magoti kila mara mkimwona (on his way to political hell).[/FONT]
Inaelekea kwako wewe mbunge ama kiongozi anayefanya kazi ni yule anayesema na kupigia kelele yale unayoyataka wewe na sio vinginevyo. Na zaidi kwako wewe mbunge, mwanasiasa ama kiongozi anayethubutu kusimamia misingi ya ukweli katika masuala ambayo yanaenda tofauti na maslahi yako ama ya "wenzako" basi huyo hafai. Yawezekana hafai kwako na hao "wenzako" lakini kumbuka maslahi ya watanzania yanapimwa kwa uzito wa watanzania zaidi ya milioni arobaini.

Iweje mbunge anayeaminiwa na asilimia 25 ya sample ya watanzania asiwe na credability lakini yule anayeminiwa na asilimia 7 ndiye kwako awe authority yako katika kuhalalisha nini ama msiamamo upi una maslahi kwa watanzania na upo hauna?

By the way, hivi juzi tu hatukusikia kuwa wabunge wakiwemo MASIHA FEKI WENU wamepinga Zitto asiwasilishe hoja ya kukataza wabunge wasiwe wajumbe katika bodi za mashirika ya umma ili kuondoa mgongano wa kimaslahi na kuongeza uweledi katika mashirika hayo?

No wonder mnaendelea kukumbatia MASIHA FEKI ambao kwao wao Tanzania sio zaidi ya maslahi yao kisiasa dhidi ya hao wanaodai ni maadui zao...


- Kwenye Mramba na Yona hakukuwa na hizo uchunguzi za bunge wala interogations, walikamatwa na kuepelekwa lupango, mahojiano yakafanyika huko huko ndivyo sheria ya jamhuri inavyosema ni wapi sheria yetu inasema wabunge wakivunja sheria kuwe na uungwana katika uchunguzi wa kesi zao?
FMEs!

Kaka si kweli kuwa Mramba na Yona hawakohojiwa kwanza. Na hata walipoenda mahakamani waliitwa kwa simu na wito rasmi na wao wakajisalimisha wenyewe wakiwa tayari wameshajiandaa vya kutosha....

[FONT="]Quote:[/FONT]
[FONT="]Ndege ya Uchumi[/FONT]
[FONT="]Mi Nadhani ni Wakati wa Wabunge ( Kama wanahisi huu ni Mpango uliosukwa na Serikali) kuonyesha kwamba hawawezi kunyamazishwa na Sauti yeyote ile na Waishughulikie Richmond vikali. Daima uongo hujitenga na Ukweli.[/FONT]
Endapo watafanya haya na wakati huohuo kukubali uchunguzi huu wa kupokea posho zaidi ya mara moja kutoka serikali kuu na mashirika yake na machafu mengine yaliyowazunguka basi tutawapa heshima ya kutukuka. Vinginevyo wengi wengi wataendelea kuwadharau....kitu ambacho ni hatari zaidi kwa taifa letu kuliko hata hizo posho ama richmond...

[FONT="]Quote:[/FONT]
[FONT="]Susuviri[/FONT]
[FONT="]Mh Zitto, argument yangu: why make a mountain out of a mole hill? Sasa uliikingia kifua Dowans wakati ni wizi mkubwa zaidi, sababu gani? Na ilikuwa ni matumizi mabaya ya pesa za umma, lakini uko hapa kama msemaji wa Takukuru na Hosea kuhusu posho.... kwa kweli you fail to convince me as a true fighter for the people, hapa naona ni political maneuvering.... sorry if I am wrong....[/FONT]


Hivi wizi ulifanywa na DOWANS ama RICHMOND? Kwani ni wapi Zitto aliwahi kupinga kuchukuliwa hatua kwa waliohusika na RICHMOND? Kwani kama hao tuliowapa UMASIHA wanashindwa nini kufanya kweli kuhusu RICHMOND?

Yaani watanzania tumeishiwa kiasi hiki mpaka tunafikia kuhalalisha UOZO wa posho tunazozipigia kelele hapa kila siku just kwa sababu tunadhani kuwa kufanya hivyo kutawaumiza MASIHA FEKI wetu....Credability haijengwi na tunayoyasema majukwaani bali matendo yetu ndiyo nguzo muhimu ya uaminifu kwa wananchi. Tuache uvivu wa kimatumaini na tuamini kuwa tunaweza kuwa na harakati za kweli zitakazoongozwa na watu walio wasafi na wenye kuamini kwa dhati yale wanayoyatetea na sio kuangalia umaarufu na nafasi zao kisiasa tu....

Tunahitaji KUJISAHIHISHA kama wazalendo wa kweli na kama Taifa kabla ya kufikia mahala hali ikawa mbaya zaidi na kushindwa kujinasua katika majanga yanayotujongea....Tuanze na hili la wabunge wetu tuliowapa imani ya kutuongoza katika utakaso huo

omarilyas
 
Duh,

Naona sasa JF imekuwa kama michezo ya kidali poh. Yaani mkuu waberoya umeamua kuongea utumbo kiasi hiki. Kwamba unaleta michezo ya kitoto ya kutaka kuonekana nani popular vile. Yaani mambo yale ya high school kind of.

Mf:

Waberoya -- baba yangu anamzidi baba yako
Zitto -- no, baba yangu ni bora kuliko baba yako
mwanajf mwingine -- baba yangu ni askari polisi wakati baba yako ni mlinzi

waberoya -- baba yangu akitoka kuoga nyumba yote inajaa moshi
Zitto -- nyie hamnijui mimi kuwa ni mbunge kwa hiyo baba yangu ni mdosi.

mwanajf mwingine -- acha hizo wewe, ndio maana una koti la njano.
waberoya -- nyie wote na baba zenu mkichanganywa na maji mnabaki maji tu
kengele inagongwa na watoto wanakimbia kurudi darasani.




Haya ya umbea na jinsia za kiume na kike sijui yameingia vipi hapa? Au ndio kuishiwa huku?




wakati huo huo wakati wakiwa darasani ***

waberoya -- unajua ukoo wetu ni mkubwa kuliko wa mwalimu sayi?
Zitto -- acha hizo wewe, ukoo wangu unazidi wa kwako na mwl Sayi.

*** Mwl Sayi -- hivi nyie hapo si mnyamaze?



Waberoya -- sawa mwl tutanyamaza baada ya huyu chakubanga hapa
mwanajf mwingine -- unamwita nani chakubanga?
waberoya -- wewe hapo na baba yako polisi

*** Mwl Sayi -- nyie watoto acheni bange zenu




Waberoya -- hapana mwl, siyo bange, ni bangi
Mwl Sayi - what.......ever!!!!!!!!



Waberoya (huku akimgeukia Zitto) -- au wewe unasemaje?
Zitto -- je kwenye nini?
Waberoya -- ni bange au bangi?
Zitto -- ni bange



Waberoya -- wewe nawe sasa unaniangusha

Flap flap flap flap (mwl Sayi anasogea taratibu)

*** Hivi nyie mna matatizo gani?

Zitto -- sio mimi mwl, ni hawa wachagga (huku akinyoosha kidole)
Mwanajf mwingine -- mimi sio mchaga, mimi ni msukuma

Waberoya -- si ulisema wewe mnyaki?

***** makelele kibao hata hawaeleweki ...

Zitto -- Nani kasema yeye mnyaki?

Waberoya -- sio wewe mheshimiwa zitto, ni huyu mtoto wa polisi!
Zitto -- ah haaa



Mwl Sayi -- Zitto na waberoya, wachaga wamewakosea nini?
waberoya -- simu yangu imeishiwa chaja

Mwl Sayi -- simu ya nini sasa hapa?

Waberoya -- sio lazima ujibiwe..... message sent.

Asante sana
 
- Kwa njia za kisheria, sio kwa kupigiana simu majumbani toka lini sheria za jamhuri zikawa enforced kwa kutumia simu?

Respect.

FMEs!

Simu isitumike kwa kiwango gani?

Ukipigiwa simu na polisi na kutakiwa ufike polisi utasema sheria haiwi enforced kwa simu?

Una uhakika alichiponga Mwanakijiji ni simu na sio chombo chenyewe?

Salaam!!
 
Kaka unajua Mramba alihojiwa na kufikishwa mahakamani akiwa Mbunge? Unajua stori ya yule mbunge wa Morogoro aliyeburuzwa na Landrover la Polisi kwa madai ya Maji? Hawa nani alikuja hapa kuwatetea na kusema tawi la utendaji lisiingilie Bunge?

Nakupata vizuri; kama wabunge wenyewe hawasimami kujitetea nani atawatetea? Kama wabunge wanaridhika na uovu au dhulma dhidi yao mtu wa kulaumiwa ni wao wenyewe. Hata hivyo hilo halizuii kutoa utetezi wa jumla wa wabunge pale inapobidi.

Kuna tatizo la msingi katika Taifa letu na katika mfumo wa Bunge. Fanya tafiti zako, ni Bunge la Tanzania tu duniani ndilo halina utaratibu wa kudhibiti mienendo ya Wabunge

Hili bado ni tatizo la wabunge wenyewe. Kama wabunge wanaliona hili au hawalioni sijui inakuwaje. Nadhani kwa maneno mengine wabunge wetu siyo makini mno.

.
Nchi nyingine wana mtu anaitwa Kamishna wa mienendo (Office of the Commissioner for standards). Huyu huchunguza mienendo na ile ambayo ni ya kijinai huenda katika jinai na ile ya kimaadili (hili la posho ninadhani ni la kimaadili) linakwenda kamati ya Maadili na kisha Bunge kutoa adhabu.

nyinyi ndio wabunge; kama mnaona ipo haja ya kuwa na kitu cha namna hiyo tungeni sheria. Ukiona wanagoma ongoza maandamano Dodoma na sehemu mbalimbali nchini hadi wabunge wengine wakuunge mkono. Watanzania watakuwa nyuma yako. We know what is needed but who will lead us into getting it?

Mwaka 2004 Sheria ya maadili ilirekebishwa ili Bunge lipitishe 'code of conduct' kwa wabunge. Mpaka leo hatujapitisha. Mwaka 2008 niliwasilisha muswada binafsi ili kuunda code na kisha kuunda ofisi ya Kamishna huyu. Mpaka leo Ofisi ya Spika imekalia muswada huu na kukataa kuupeleka kuwa gazzetted ili ujadiliwe Bungeni.


Hakuna msukumo wa kisiasa toka upinzani au ndani ya Bunge zima. Ni hoja za kisomi za kujaribu kutuonesha kitu ambacho kinajulikana. Sheria ya maadili ilivyo na yale mapendekezo uliyatoa nyuma hujaongoza watanzania kuona umuhimu wake. Wekeni shinikizo la kisiasa; tokeni bungeni, shikeni mabango ikulu.. by any legal means necessary. Vinginevyo, hapa unanihubiria mwanakwaya wako.

Hivi MwanaKijiji unajua wabunge wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?

Kama hili ni kweli, ulitakiwa kutoa hii charge ndani ya Bunge na vithibitisho. Wabunge wanaofanya hivyo wapigiwe kelele waondolewe Bungeni, na unaweza kufungua kesi mahakamani. Haya wabunge wanafanya yanafanywa na watumishi wengi wa umma kwa muda mrefu tu. Tumejifunza sisi sote kuishi ndani ya mfumo wa kifisadi, kustawi ndani yake na kuvuna matunda yake haramu; wenyewe tunaita "kuula"!

Tunafanya makosa, halafu hakuna code wala mamlaka ya kutuchunguza halafu tuachiwe. Hapana. Mwanakijiji wewe kwa heshima yako hupaswi kutetea uvunjifu wa maadili.

Sijatetea uvunjaji wa maadili; ninatetea kanuni. Hatuwezi kukubali kanuni zivunjwe kwa ajili ya kujifurahisha. tukikubali kuvunja kanuni kubwa kwenye jambo dogo, basi jambo dogo litatufanya tuvunje kanuni kubwa huko mbeleni!

Waache TAKUKURU wafanye kazi yao. Lazima Wabunge tujue kuwa hatupo juu ya sheria na kwamba tupo accountable na answerable kwa vitendo vyetu (for actions and inactions).

Maana ya kuwa juu ya sheria siyo kwamba mwingine yupo juu ya sheria. Takukuru wanaposema kuwa wabunge "hawako juu ya sheria" wasimaanishe kuwa wao (takukuru)j wako juu ya sheria. sheria zinawafunga wote sawa.
 
Hakuna yeyote ambaye yuko juu ya Sheria, kama Dr. Mwakyembe na wabunge wengine walivunja sheria katika upataji wa malipo na ikathibitishwa kuwa walifanya hilo jambo kinyume cha sheria, nadhani ni sahihi kabisa kwa wao kuchunguzwa, kuhojiwa na hata kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

point nzuri hii geeque; tatizo langu haliko kwenye nani anachunguzwa au nini kinachunguzwa; tatizo liko katika utaratibu wa kuchunguza. Wabunge wa nchi yetu hawawezi kufanya kazi kwa huruma ya vyombo vya dola. Kwamba chombo cha dola kikiona au kikiagizwa na kiongozi wa juu serikalini kufanya uchunguzi juu ya mbunge au wabunge basi wanajiendea abitrarirly. hili kwangu ni la kanuni zaidi.
 
Mbunge Ole Sendeka atishia kumharibia Rais Kikwete
broken-heart.jpg


*Ataka serikali iwakamate kwanza nafisadu badala ya kuibua hoja ya 'posho mbili'
Daniel Mjema, Dodoma

SUALA la wabunge kuhojiwa na Takukuru, juzi lilichukua sura mpya baada ya Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka kugeuka msumari wa moto kwa serikali akitaka iwakamate kwanza wabunge mafisadi wanaohusika na kashfa za Kagoda na Deep Green Finance kabla ya kuwaandama wabunge.

Katika kashfa hizo, Kampuni ya Kagoda Agriculture inadaiwa kuchota kifisadi Sh40bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wakati Deep Green Finance inadaiwa kukwapua Sh9 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka ndani ya kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika mjini Dodoma,inaelezwa kuwa Sendeka alihoji kama kweli agizo la kuwahoji wabunge lilitolewa na Ikulu.

Huku akishangiliwa na wabunge wengine, Sendeka aliibana serikali akitaka kujua iwapo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah ametumiwa na mafisadi au kweli katumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwadhalilisha wabunge.

Sendeka alitoa kauli hiyo juzi usiku mjini Dodoma katika kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa chini ya Katibu wa Kamati ya Wabunge wa chama hicho, Ali Ameir na taarifa zake kulifikia gazeti hili.

“Kuna mambo mawili ambayo tunayaona katika suala hili; ama Dk Hoseah anatumiwa na mafisadi au ametumwa na rais kuwadhalilisha wabunge kwa sababu Takukuru siyo taasisi inayojitegemea bali iko chini ya rais,” chanzo chetu kilimkariri Sendeka akisema ndani ya kikao hicho.

Alisema hawaelewi na hawaamini kama rais ndiye ameagiza wabunge wadhalilishwe, lakini kama ndivyo awaeleze ili nao waende majimboni kwa wananchi kuwaeleza mabaya ya serikali wanayoyafahamu.

Huku akipigiwa makofi na wabunge karibu wote waliohudhuria kikao hicho, Ole Sendeka alisema baada ya kuwaeleza wananchi, wao ndio watapima ni nani wasafi kati ya wabunge, serikali na Takukuru.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zimedokeza kuwa Sendeka alitaka Rais Kikwete azungumze na Mkurugenzi wa Takukuru kabla mambo hayajaenda kombo.

Kikao hicho kilikuwa mahususi kwa kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kutoa taarifa ya ujio wa kamati ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, lakini Ole Sendeka akakitumia kuibua suala la uchunguzi huo wa Takukuru.

“Tunafahamu Hoseah anajua humu ndani wapo wanaohusika na kashfa za Kagoda, Meremeta na Deep Green Finance awakamate kwanza, tuone kama kweli anakerwa kwa dhati na tatizo la rushwa,”alikaririwa Ole Sendeka.

Mbunge huyo machachari alisema endapo suala ni malipo ya posho kwa wabunge, iundwe tume huru ya pamoja kuchunguza na uchunguzi huo ufanyike kwa mihimili yote mitatu ya dola kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali.

Chanzo hicho cha habari kimedokeza kuwa Ole Sendeka alisema endapo uchunguzi huo utabaini wabunge wamekula fedha haramu, wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali.

Alidai kuwa hata yeye Hoseah na taasisi yake (Takukuru) ilipokuwa inataka Bunge lipitishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Rushwa, aliandaa semina kwa wabunge na kuwalipa posho kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

Ole Sendeka alimtaka Dk Hoseah kama ana hoja ya msingi katika uchunguzi wake asubiri kwanza Bunge limalizane na suala la Richmond wiki ijayo, ndio waendelee na uchunguzi wao.

“Baada ya uchunguzi wao watupigie mahesabu kama kuna fedha haramu tumekula, tupo tayari kuzirejesha lakini uchunguzi huo uendelee pia kwa mihimili mingine ya dola ambayo ni serikali na mahakama," alikaririwa Sendeka.

Katika kikao hicho Ole Sendeka alihoji ni mkuu wa mkoa gani au waziri anayesafiri kwenda wilayani au mikoani ambaye hata kama amelipwa posho stahiki, husafiri na chakula chake bila kukirimiwa na halmashauri anakokwenda.

Habari kutoka katika kikao hicho, zimezidi kueleza kuwa Ole Sendeka aliitaka serikali kuwasiliana na Spika wa Bunge au katibu wake ili kupata ufafanuzi wa posho hizo vinginevyo iwaite wabunge wote na kuwahoji.

Wakati mvutano huo ukiendelea, zipo taarifa kuwa Takukuru imekuwa ikijiandaa kuwakamata baadhi ya wabunge siku moja au siku ya mjadala wa Richmond ikiwa ni mbinu ya kudhoofisha mjadala huo.

Habari zilizowakariri baadhi ya wabunge zinadai kuwa mpango huo umeandaliwa mahususi na wapo wabunge kwa majina ambao wanaandaliwa mpango wa kuwakamata, ila wanasubiri kwa hamu hilo litokee.

Wiki hii, Mbunge wa Kyela, Mwakyembe alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hatua hiyo ya Takukuru kutaka kuwahoji wabunge sasa, ina lengo la kuwafunga midomo wasijadili kashfa ya Richmond.

Alhamisi wiki hii, Spika wa Bunge,Samuel Sitta alisema wabunge wataendelea kupokea posho kwa kuwa ni halali na serikali ilileta bajeti zake bungeni na zikapitishwa na kuitaka Takukuru ishughulikie mambo ya msingi.

Msuguano huo kati ya Serikali na Bunge umekuja wakati wiki hii Bunge linatarajiwa kujadili ripoti ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayoitaka serikali kutekeleza maazimio yote bila kusitasita.

Miongoni mwa maazimio hayo ya Bunge ni kuwajibishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Hoseah kwa namna alivyoficha ukweli kuhusu Richmond hadi kamati ya Bunge ilipogundua uozo mkubwa.

Kashfa ya Richmond ndiyo iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu akifuatiwa na mawaziri wengine wawili, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao waliitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa mchakato wa zabuni iliyoipa ushindi kampuni hiyo.

Pamoja na kujiuzulu huko maazimio ya Bunge yalitaka pia kuwajibishwa kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika na katibu mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria.

Wabunge wanataka suala la utekelezaji wa maazimio hayo ya Bunge limalizike katika Bunge hili la 17, lakini hadi jana kulikuwa na usiri mkubwa wa lini ripoti hiyo ya serikali ya wa maazimio hayo itawasilishwa bungeni.



Source: Mwananji
 
Mzee MwanaKijiji,


... There is absolutely no doubt that some of this outcry by the MPs is intended to conceal some of their own shortcomings in the character and integrity department. In order to even begin to scratch the surface on the endemic problem of corruption that our nation is currently facing, we need to begin by cleaning up Parliament so that our Parliamentarians will have both the credibility and moral authority to wage an effective all-out war on corruption and not be viewed as self-righteous hypocrites.

well said. If you read my original post on this issue.. I did not deal with the question of "posho mbilli". That to me is not an issue. The issue is the process of investigating member of parliaments, questioning them at will and even possible remanding without following procedures. That to me, will set a very dangerous precedent.
 
Mzee Mwkjj, naona na wewe unaelekea huko huko. Nadhani ni muhimu kwanza tuweke vitu in perspective na tuzungmzie mihimili ya dola then tuchambue kazi of each. Na pia ni lazima tukubali kuwa hakuna ambaye yuko juu ya mwenzake. Kila mhimili ina kazi yake, kwa mfano ya mahakama ni interpretation ya sheria, Bunge ni upitishaji wa sheria. I think tatizo ni kwamba mpaka leo haijawekwa clear vyombo vya dola iko chini ya mhimili upi na kwa njia gani. Hii ni kutokana na kwamba imekaa kisani, hata hiyo TAKUKURU, I believe they do not have the same power like police, bali wanashirikiana na mwanasheria mkuu kuleta prosecution. Nadhani tutakapoanza kuchambua suala hili basi tutakuja kuona kuwa Pinda ameongea kitu ambacho kinahatarisha democrasia na ni haki ya kusema kuwa ajiuzulu: Amesema hawawezi kuacha kuhoji wabunge kwa kuwa Rais ameamuru, kwa hiyo Rais amevuka mipaka, kwa sababu kikatiba, Rais hawezi kumchunguza mbunge au wabunge. Inaonekana PInda amekiri kuwa TAKUKURU ni remote arm ya Rais na uchunguzi unaendeshwa at the whims of the President. Very big mistake and serious legal problem. Mi nadhani ni vyema Pinda angekaa tu kimya lakini he has opened Pandora's box....

tatizo ni kama zitto alivyosema mahali fulani kuwa Rais yuko juu ya mhimiili yote mitatu. Mawazo ya namna hiyo yanamgeuza rais wetu kuwa mfalme. ndio maana wabunge kama wanajua wajibu wao wangefanyia mabadiliiko taasisi ya PCCB na kuitoa mikononi mwa rais na kuiweka nje yake, kama vile wangefanya kwenye usalama wa taifa ili vyombo hivyo visitumike kisiasa.
 
Fundi Mchundo,
Mkuu, Nafikiri wabunge sio waajiriwa wa serikali kwa hiyo baadhi ya taratibu za serikalini zitakuwa haziwahusu. Kwa hiyo Posho ya kujazilia inaweza ikawa inaruhusiwa kila wanapotoka nje ya bunge. Lakini kwa vile ni jambo linaloikera serikali, basi serikali wangepeleka mswada bungeni kulipinga hilo na sio kuja na misemo isio na msingi na kuiita rushwa. Watanzania wanajua tofauti zake.

Sawa, Mkuu. Labda tuwaite ni watumishi wa umma. Malipo yao yanatokana na kodi ya wananchi kwa hiyo wanaongozwa na taratibu na maadili ya mtumishi yeyote wa umma. Kunachogomba hapa ni morals na ethics za hawa waheshimiwa. Hizo kamati zinapotembelea hayo mashirika na idara za serikali ni kwa madhumuni ya kuzikagua na kupata ukweli kuhusu mwenendo wao. Ndiyo maana Ofisi ya Bunge inawagharimia na kuwapa posho za kutosha ili waweze kutimiza majukumu yao with total impartiality. Unapokuta wakarimiwa na hao wanaoenda kuwachunguza, matokeo yake ndiyo tuliyoyaona kuwa wanakuwa mstari wa mbele kutetea uzembe wao. Tukambuke jinsi wabunge walivyoipamba Benki Kuu kuwa ni moja ya Benki Kuu bora Afrika joto la Epa lilipoanza. Hiki ndicho kinachochefua. Mtu yeyote mwenye integrity yake anapoenda kumkagua mtu na huyo jamaa akim-ofa takrima anajua wajibu wake ni kukataa.Tofauti ya hivyo, hawa waheshimiwa wanatanguliza kutembeza kibakuli! Kingine anacholalamikia Zitto ni tabia ya kudanganya ili wapate pesa za ziada. Ingawa tunaona ni kitu kidogo lakini ni dalili mbaya ikiwa kiongozi mwenye hadhi ya ubunge anapodanganya kuwa alitumia gari lake wakati alipanda basi. Kama kwa madogo anakosa uaminifu itakuwaje kwa makubwa? Ni hivi vitabia vya kwapukwapu ndizo zilizotufikisha hapa tulipo. Tuliowapa majukumu ya kulinda maslahi yetu wanatanguliza zaidi tamaa ya vijisenti vya ovyo ovyo. Kwa kulipiwa tiketi ya ndege kwenda ughaibuni na kulipiwa malazi ya wiki moja wanashindwa kabisa kufanya due diligence kabla ya kuitumbikiza serikali kwenye mikataba ya dhulma!

Zitto yuko right. Ni lazima tuukoromee uovu wowote unaofanywa na hawa wawikilishi wetu bila kujali ukubwa wake. Gharama ya kuangalia pembeni ni kubwa mno.

Amandla.....
 

Zitto yuko right. Ni lazima tuukoromee uovu wowote unaofanywa na hawa wawikilishi wetu bila kujali ukubwa wake. Gharama ya kuangalia pembeni ni kubwa mno.

Amandla.....

- Mkuu Fundi, hatuwezi kukoroma tu for the sake of kukoroma ili tuonekane tunakoroma bila kujua sheria iliyovunjwa, kila mwananchi yuko innocent until proven otherwise na hakuna aliyejuu ya sheria wala aliye chini, ingawa that is not the case na taifa letu,

- Hili suala zima linachekesha kwa sababu hatuambiwi ukweli wote, sheria iliyovunjwa haihitaji haya yote tunayoyaona yanatendekea, na ukizingatia kwamba Hosea anatakiwa kuwajibishwa kutokana na ushauri wa ripoti ya wabunge hao hao anaowaandama sasa kuhusu posho!

- Sasa hapo inakuwa sio kukoromeana tu bali wote tunashuka hadhi as a nation.

Ahsante.

William.
 
Kumbuka kuwa fedha zilizokuwa zikichotwa kwa makosa na waheshimiwa Wabunge ni fedha za Serikali na si fedha za Bunge. Kwa hali hiyo Serikali ina kila sababu ya kushinikiza wabunge waache kuomba/kudai pesa wanapokwenda kuhoji wizara na taasisi zake.

Kwa nini hiyo serikali isiweke utaratibu kwa vyombo vyake kutotoa hizo fedha hata wakiombwa? Kwangu mimi ningewachunguiza wale wanaotoa fedha hizo kwanza kwani they are the enablers of corruption. Kama vyombo vya serikali vingekuwa havitoi hizo fedha hakuna mbunge au mtu mwingine ambaye angekuwa na ujasiri wa kuomba.

Sasa angalia ustaarabu uliofanywa na Serikali. Kwanza ilitumia njia ya kisiasa kwa Waziri Mkuu kumuandikia Spika ikashindikana. Baadae ikatumia njia ya kiutawala kwa Katibu Mkuu Kiongozi kuzungumza na Katibu wa Bunge.

Kuna barua yoyote au maelekezo yoyote toka ofisi ya waziri mkuu au kwa Rais kwenda kwenye vyombo vya serikali kuvitaka kuacha kutoa posho hizo?

Serikali kwa upande wake ingeweza tu kuyaagiza Wizara, Taasisi na Mashirika ya Umma yasitowe chochote kwa Wabunge watakaoomba. Lakini kwa kuwa inajuwa vizuri tabia za waheshimiwa Wabunge wetu walivyokuwa vindictive, wangewapa taabu sana viongozi wa Wizara, taasisi na mashirika yao.

Ingeweza? Ndio maana Pinda na Hosea walitakiwa wajiuzulu kwa uzembe na kuchangia kuendeleza vitendo vyenye mrengo wa kifisadi vyenye malengo ya kupindisha uhuru wa bunge na wabunge. Hiyo sababu ya kwanini WM hakuviagiza vyombo vyake kutotoa fedha kunanifanya nipige kelele Pinda afungashe virago vyake.!

Kwa hiyo kuliko kuwagonganisha Wabunge na Wizara, Taasisi na Mashirika yake serikali ikaamua ku tackle problem hii at national level kwa ku involve Spika na Ofisi yake kisiasa na kiutawala.

hicho ni kisingizio dhaifu kuliko vyote cha kujaribu kufafanua uzembe na kutokuwajibika.


Hivi sasa kwa upande wa serikali wao problem yao is now solved maana sioni namna ambayo wizara, taasisi na Mashirika ya Serikali yataendelea kutowa posho hizi hapo baadaye.

kama hawakatazwi nini kitawazuia? Je ina maana taasisi hizo hazitatoa posho kwa watumishi wake mbalimbali na watu wengine ambao si wabunge wanaohudhuria warsha, tamasha, kongamano, semina, mikutano, n.k?
 
FIELDMASHALL TUACHE USHABIKI KTIK HILI MWAKYEMBE IS WRONG
1. Slaa kamwambia leo, kwanini wenzake wote, yeye slaa, shelukindo, na wabunge wenzake wamekubali kuhojiwa yeye akatae?

Ukiona wenzako wanaruka kwenye genge kwa sababu fulani kawaambie waruke na wewe utaruka?
2. We unajenga hoja kwamba Mwakyembe yuko sahihi kukataa kuhojiwa kwa simu...hiyo sio hoja....TAKUKURU hawakutaka kumuhoji kwa simu. walimpa taarifa ili wakamuhoji...usicheze na maneno kubadilisha mantiki jamani.

Hawana nguvu ya kufanya hivyo; na wabunge waliokubali ni wale wasiojua nguvu yao ya kisheria. Haijalishi kama aliyewaomba ni Katibu wa Bunge..!
 
Nimezisoma hoja na michango ya watu wote kwenye thread hii na nimewajibu pale inapopaswa. Naombe niweke nukuu hii kutoka kwenye sheria ya Haki, Wajibu na Madaraka ya Bunge

11. Notwithstanding anything to the contrary, no summons issued by

any Court of the United Republic or outside the United Republic in the

exercise Of its civil jurisdiction shall be served or executed within the

precinct of the Assembly while the Assembly is sitting, or through the

Speaker or any officer of the Assembly, nor shall any member be arrested

on civil process, save by the Leave of the Speaker first obtained, while
he is within the precincts of the Assembly and while the Assembly is







sitting.

Na vile vile:


5.

No civil or criminal proceedings may be instituted against any


member for words spoken before, or written in a report to the Assembly

or a committee, or by reason of any matter or thing brought bv him
therein by petition, bill, or motion or otherwise or for words spoken or
act done in bona fide pursuance of a decision or proceeding of the
Assembly or a committee.
6. No member shall be liable for arrest for any civil debt except for

a debt the contraction of which constitutes a criminal offence.


 
Back
Top Bottom