Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Pinda?

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Zitto said:
#sahihi70 tumepata sahihi 62 mpaka sasa. Makao makuu CUF imetoa agizo kwamba wabunge wao waweke sahihi. Tutafanikiwa

#Sahihi70 ndugu Deo Filikunjombe amesaini. Huu ndio unaitwa ushujaa. Kuwa upande wa wananchi.

#sahihi70 ndugu Kangi Lugola amesaini tayari

Mh. Zitto Bungeni ametoa bomu kwamba wamiliki wa ndege iliyokodishwa kwa ATC wamepewa bandari ya Mtwara baada ya ATC kushindwa kulipa deni kwa Wallis Traders ya Lebanon....OMG.

Zitto kazini anatafuta kura za wabunge 71

Sababu bunge halina meno ya kuwawajibisha mawaziri ila wabunge wanauwezo wa kumwajibisha waziri mkuu

Swali:

Wakina Filikunjombe watatoa saini kumwajibisha wanaojiita mwanachama mwenzake?

Wananchi tuone wabunge wetu wapo kweli au ni kerere za chura
ZITTO kafyatuka "Kesho mchakato utafanyika kukusanya sahihi, zinahitajika sahihi 70 tu"

Kama yeye ameshindwa kuwajibisha mawaziri basi awajibishwe yeye!!!!

Halafu sasa wataamua nani abaki
Zitto Zuberi Kabwe on twitter:

#Sahihi70 mpaka sasa tumepata sahihi 52 kutoka kwa wabunge wa vyama vyote isipokuwa #UDP

Wabunge Walio Saini, Kwa Majina

1. Rashid Abdala CUF
2. Chiku Abwao CDM
3. Salum Barwany CUF
4. Salum Mbaruku CUF
5. Deo Filikunjombe CCM
6. Pauline Gekuli CDM
7. Asaa Hamad CUF
8. Prof Kahigi CDM
9. Naomi Kaihula CDM
10. Sylvester Kasulumbaya CDM
11. Raya Khamis CDM
12. Mkiwa Kiwanga CUF
13. Sazan Kiwanga CDM
14. Grace Kiwelu CDM
15. Kombo H Kombo CUF
16. Joshua S Nassari –CDM
17. Tundu A Lissu- CDM
18. Aphaxar K Lugola- CCM
19. Susan A Lyimo- CDM
20. Moses Machali – NCCR
21. John Shibuda Magalle CDM
22. Faki Haji Makame-CUF
23. Esther N Matiko-CDM
24. Joseph Mbilinyi- CDM
25. Freeman Mbowe- CDM
26. Kurudhum J. Mchuchuli – CDM
27. Halima Mdee-CDM
28. John Mnyika- CDM
29. Augustino L Mrema- TLP
30. Maryam S Msabaha- CDM
31. Peter Msingwa-CDM
32. Christowaja G Mtinda CDM
33. Philipa G Mturano- CDM
34. Christina L Mughwai- CDM
35. Joyce Mukya – CDM
36. Israel Y Natse – CDM
37. Philemon Ndesamburo- CDM
38. Ahmed Juma Ngwali-CUF
39. Vincent Nyerere- CDM
40. Rashid Ali Omar-CUF
41. Meshack J Opulukwa- CDM
42. Lucy Owenya- CDM
43. Rachel Mashishanga- CDM
44. Mhonga Ruhwanya – CDM
45.Conchesta Rwamlaza – CDM
46. Moza Abedi Saidy-CUF
47. Joseph R Selasini – CDM
48. David E Silinde-CDM
49. Rose Kamili - CDM
50. Cecilia Paresso- CDM
51.Kabwe Zuberi Zitto- CDM
52. Magdalena Sakaya – CUF
53. Rebecca Mngodo- CDM
54. Sabreena Sungura -CDM

Majina mengine yatakuja muda si mrefu...

MHE KABWE Z. ZITTO – MWENYEKITI WA KAMATI YA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA

Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote ambao wamechangia katika hoja hii na kutokana na muda sitoweza kuwataja majina wote kwa sababu inahitaji tupate muda wa kutosha kuweza kuzijibu hoja zote pamoja na majibu ambayo baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri wameyatoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jambo moja ambalo Waheshimiwa Wabunge wamependekeza tuboreshe mapendekezo ya Kamati, pendekezo namba 7.2.7 kuhusiana na ukodishaji wa ndege wa Air Bus ambao ulifanywa na ATCL tarehe 27 Oktoba, 2007 na baadae Serikali ikatoa guarantee kinyume na sheria ya mikopo mwezi Aprili 2008 walitoaguarantee baada ya kuwa mkataba umeshaingiwa. Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge watatu waliochangia kwa maneno na wanne waliochangia kwa maandishi wakapendekeza kwamba Bunge liunde Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza mazingira kwa kuingia mkataba huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunaendelea na michango nimepata taarifa, tulitoa taarifa kwanza Serikali haijaanza kulipa fedha zile kwenye Kampuni ya Wales Trading ya Lebanon. Lakini nimepata nyaraka ambazo zinaonyesha kwamba Serikali imeanza kulipa. Mpaka sasa tumeshawalipa shilingi bilioni 2.5, tumewatengenezea schedule ya malipo mpaka watakapokuwa wamekamilisha kuyalipa na ninayo hapa nitampatia Mheshimiwa Wazrri Mkuu aweze kuiona. Lakini linalonisikitisha ni kwamba tarehe 27 Machi, 2012 Maafisa wa Wizara ya Fedha walikutana na wawakilishi au wamiliki wa hii Kampuni Wales Trading ambayo walitukodishia ndege ambayo haikuruka na ambayo imetuingiza madeni makubwa sana na Waheshimiwa Wabunge na hasa Wabunge wa Mikoa ya Kusini naomba wanisikilize kwa makini watu hawa sasa katika nia ya kulipa deni hili wanapewa bandari ya Mtwara. Nina nyaraka hizi nitaziweka mezani na kuweza kumpatia Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa kutokana na mambo haya nakubaliana na mapendekezo ambayo Waheshimiwa Wabunge ambayo wameyatoa kwamba tuboreshe pendekezo namba 7.2.7 kwamba Bunge liunde Kamati Teule ili kuchunguza mazingira ya mkataba huu na mazongezonge mengine yote. Niwaambie tu kwamba Waziri wa Miundombinu aliishauri Wizara ya Fedha kwamba Wales wasilipwe, lakini Wizara ya Fedha imewalipa Wales hii inaonyesha mkanganyiko ambao uko Serikalini miongoni mwa Wizara. Kwa hiyo pendekezo hilo naomba lirekebishwe na litakuwa hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili Waheshimiwa Wabunge wamezungumzia kuhusiana na suala la special audit ya Consolidated Holdings. Special Audit ya Consolidated Holdings Corporation iko ndani ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwanza nimeshauriana na Wajumbe wenzangu wa Kamati tumekubaliana kwamba taarifa nzima ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ule ukaguzi maalum ufanyiwe kazi na Kamati na kwa ruhusa ya Wajumbe wa Kamati nimeunda timu ya Wajumbe watatu ambao watashughulikia suala hili ambaye ni Mheshimiwa Aliko Kibona, Mheshimiwa Esta Bulaya na Mheshimiwa Murtaza Mangungu na timu hii itaongozwa na Mheshimiwa Murtaza Mangungu na nitataka wamalize kazi hii ndani ya muda mfupi iwezekanavyo kwa ajili ya kuchukua hatua zinazostahili.

Katika hili ushauri wangu ni kwamba kwa Mawaziri wote namna ya kuendesha Mashirika ya Umma naomba tufanye eyes on hands off kwa sababu ya kuweza kuepuka kuingilia Mashirika haya. Mheshimiwa Nundu amesema kwamba yeye ataingilia tu hata chooni sisi tutamwambia hapana, kwa sababu ya kutaka kuhakikisha kwamba Mashirika yetu yanaendeshwa kwa misingi inayotakiwa. Lakini lazima iwe eyes on kwa sababu pasipokuwa na eyes on madudu ya Mashirika yatakuwa makubwa sana. Kwa hiyo lazima ku-balanceeyes on hands off msifanye micro managing, kwa sababu micro managing ndiyo ambayo inatuletea matatizo. Kuhusiana na Waziri wa Fedha ambaye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imemuonyesha dhahiri kwamba aliingilia na kufanya maamuzi kuhusiana na Shirika la CHC ajipime, ajione kama bado anastahili kuendelea kushikilia fedha za nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Bodi ya Pamba na maelezo Waziri wa Kilimo ameyazungumza na napenda nitofautiane naye Mheshimiwa Maghembe kwa sababu tarehe 17 jana nilisema tarehe 2, tarehe 17 Novemba, 2011 mmiliki mwenye Mashirika kwa niaba yetu Msajili wa Hazina aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya kuivunja Bodi ya Pamba ambayo ilikula fedha za wananchi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameshaonyesha kwamba fedha za wananchi zimeliwa. Waziri anasema kwamba anaomba mamlaka ya uteuzi iteue Mwenyekiti mwingine na hili ni kwa Mawaziri wote, tabia ya kumsingizia Mheshimiwa Rais katika kila jambo ambalo mnapaswa kulifanya ikome. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu Rais hayuko humu ndani ni rahisi sana kusema kwamba Rais hajafanya, Rais hajateua, suala la kuvunja Bodi ni mamlaka ya Waziri, uteuzi ni mamlaka ya Rais, Waziri anayo mamlaka ya kuweza kuvunja Bodi na kumtaarifu Mheshimiwa Rais ateue Mwenyekiti mwingine na ateue Wajumbe wengine na hatua zingine ziweze kuchukuliwa. Kwa maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Prof. Jumanne Maghembe ameyazungumza ni maelezo ambayo si sahihi. Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati sijayakubali na Bunge lichukulie tu kwamba yalikuwa yanapita tu kwa sababu ilikuwa ni lazima Wizara ichukue hatua, fedha za wakulima zimeliwa na tusifanye mchezo kabisa na hawa wananchi wa kawaida wa chini kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la TBS limezungumzwa kwa kina sana. Lakini majibu hayajatosheleza. Hayajatosheleza kwa sababu kuna hatua ambazo ni lazima zichukuliwe. Sisi tulitoa taarifa tukampelekea Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Spika akatoa taarifa akampelekea Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa sisi hatufahamu kama Ofisi ya Waziri Mkuu haikupeleka taarifa ile kwa Waziri wa Viwanda na Biashara. Maana Waziri wa Viwanda na Biashara anasema kwamba hakuwa na taarifa. Kwa hiyo anachokisema ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu anachokisema Ofisi ya Waziri Mkuu haikumpelekea taarifa na nyaraka zote ziko hapa kwa Spika. Kwamba baada ya taarifa yetu imekwenda na tulishauri kwenye uchunguzi Mkurugenzi Mkuu wa TBS asimamishe, apishe uchunguzi. Mbona ilikuwa ni rahisi sana kwa Mkurugenzi Mkuu wa CHC kusimamishwa tena bila kufuata taratibu. Lakini inakuwa ni vigumu sana kwa Mkurugenzi ​Mkuu wa TBS anayewafanya wakulima wetu watumie mbolea ambayo haina ubora, anayewalisha watoto wetu Blue bandambazo ni fake, anayeingiza matairi nchini ambayo yanasababisha ajari, inakuwa ngumu sana, lakini inakuwa rahisi kwa watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilichokuwa nakiomba ni kwamba, maelekezo ya Mheshimiwa Spika, kwa Waziri Mkuu kuhusiana na TBS yatekelezwe na yatolewe taarifa Bungeni kwa sababu maelezo haya Mheshimiwa Spika ameshayatoa muda mrefu sana na ni zaidi ya miezi miwili sasa imepita toka Mheshimiwa Spika, ayatoe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho. Tatizo kubwa la Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutokutekelezwa ni ukosefu wa uwajibikaji; na kama nchi hii tunataka tuendelee, kama tunataka tupigane kwa dhati kabisa dhidi ya ubadhirifu, dhidi ya udokozi, dhidi ya uzembe, dhidi ya uvivu ni kuhakikisha tuna misingi sahihi ya uwajibikaji.Accountability, niliwahi kuwaambia vijana fulani kwamba kama kutakuwa kuna neno moja linalotakiwa liandikwe kwenye Katiba mpya, neno moja; ni ‘accountability,' uwajibikaji na ndicho kinachokosekana. Taarifa hizi zinatolewa kila mwaka, nashukuru sana safari hii Wabunge mmekuwa wakali sana. Lakini bila kuhakikisha Executive inawajibika katika haya mwaka kesho tutarudia haya haya na tutakuwa wakali hivi hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa taarifa kwamba; mimi na Bunge hili halina mamlaka ya Mkurugenzi wa Shirika, Katibu Mkuu wa Wizara au Mkurugenzi wa Halmashauri. Mawaziri ambao wametajwa kwa njia moja au nyingine kutokuwajibika ipasavyo na kuliingizia hasara taifa wamekuwa wagumu sana kuwajibika, wanampa kazi Rais ya kuwafukuza.

Lakini sisi hatuwezi kuwaazimia hapa ila sisi tuna mamlaka na mtu mmoja tu humu ndani ya Bunge; na naomba mnisikilize kwa makini sana. Tuna mamlaka na mtu mmoja tu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bila kumwajibisha Waziri Mkuu hawa Mawaziri waliotajwa hawatatoka na wasipotoka madudu haya yatarudia. Kwa hiyo Mbunge yoyote mwenye uchungu na ubadhirifu, Mbunge yoyote ambaye anakereka na watoto kwenye Jimbo lake kukaa chini, Mbunge yoyote anayekereka na madawa kuharibiwa na MSD na MSD kushindwa kupeleka madawa kwenye vijiji vyetu, nampa taarifa kwamba kuanzia kesho tunakusanya sahihi za Wabunge 70, ili siku ya Jumatatu tutoe hoja hapa Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na kipindi hiki tunakitoa Mawaziri wote ambao wapo implicated kwenye taarifa hizi waweze kuona ama wao, au wamtoe rehani Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wabunge wote wenye uchungu kuanzia kesho tutakuwa pale mlangoni, sahihi zinazohitajika ni 70 tu, kwa ajili ya kuleta hapa Bungeni na Wabunge wanahitajika kupitisha hilo azimio ni nusu tu ya Wabunge, 50 plus one. Tukifanya hivyo tutakuwa tumewapa heshima wananchi wetu, wataona kweli tumewatendea haki badala ya kupiga kelele bila ya kuchukua action. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Wenyeviti wenzangu wote, Mheshimiwa Cheyo na Mheshimiwa Mrema nitoe hoja sasa kwamba Bunge lako lipokee taarifa za Kamati zote hizi tatu na mapendekezo yake na kuweza kuyapitisha. Naomba kutoa Hoja. (Makofi)
 
aise kumbe mawaziri wetu wanaitafuna nchi kiac hiki mkullo itakuwa kma balali yan bongo ni zaidi uijuavyo inatia uchungu sna madawa hakuna hospitali dah inauma
 
Halafu hiyo ndege haikuruka then wakapewa zawadi bandari ya WATZ? kama vile mtu anamgawia mtu pipi kutoka mfukoni mwake. Hili ni tusi kwa waTZ.
 
Nchi inaongozwa Kishie******nzi
Niko tayari nipig:amen::frusty::amen:
 
Zito kwa kweli wewe kidume manake umeongea kwa ushupavu haswa kumwambia huyu Jambazi sugu WAZIRI WA FEDHA ajipime kama anafaa kwendelea kushikilia fedha zetu.

'Msako wa nyani ngedere haponi safari hii'
 
Mh. Zitto Bungeni ametoa bomu kwamba wamiliki wa ndege iliyokodishwa kwa ATC wamepewa bandari ya Mtwara baada ya ATC kushindwa kulipa deni kwa Wallis Traders ya Lebanon....OMG.

Waziri wa uchukuzi bado yupo kitini au anawasilisha barua ya kujiuzulu? toba rabi
 
Zito kwa kweli wewe kidume manake umeongea kwa ushupavu haswa kumwambia huyu Jambazi sugu WAZIRI WA FEDHA ajipime kama anafaa kwendelea kushikilia fedha zetu.

'Msako wa nyani ngedere haponi safari hii'

Hafai hata kidogo. Yuko pale kutekeleza matakwa ya wachache na ndiyo maana alirudishwa pale. Hana lolote huyu. Hata TRA taasisi iko chini yake ameshindwa kuibana kupata mapato ya kutosha. Futilia mbali huyu.
 
ZITTO kafyatuka;Kesho mchakato utafanyika kukusanya sahihi, zinahitajika sahihi 70 tu.
Kama yeye ameshindwa kuwajibisha mawaziri basi awajibishwe yeye!!!!
Halafu sasa wataamua nani abaki
 
Ama Mawaziri au Waziri Mkuu, mmoja wao lazima ajiuzuru. Pinda sasa kazi unayo.

Itakuwa heri Mawaziri wajiuzuru mapema maana itawezesha kuinusuru Serikali.
 
Zitto kuongoza kumpigia Waziri mkuu kura ya kutokuwa na Imani naye kesho? Pinda anataka kulia. Naona kama anajuta kilichomponza hadi akubali uwaziri mkuu.
 
Zinahitajika sahihi za wabunge 70 tu kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Zitto amekuwa noma
 
Back
Top Bottom