DOKEZO TAKUKURU mbona hamuwakamati trafiki wanaochukua rushwa hadharani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
9,792
14,873
Muda huu saa sita kamili mchana hapa Stendi ya Morroco (Dar es Salaam) kuna askari watatu wanakusanya hela hadharani kwa kila Daladala inayosimama kituoni.

TAKUKURU tokeni maofisini muwakamate hawa majambazi katika nguo nyeupe.

Ninachojiuliza mbona wanaofanya hivyo hadharani hawachukuliwi hatua?
 
Ajabu ni kwamba mambo haya yako wazi sana siku hizi,Yani askari wala sio waoga kuomba rushwa ,mama yetu ana kazi kubwa sana ya kufaya reform jeshi la polisi upande wa traffic
 
ukiona rushwa za traffic zinakuuma,ujue bado hujakomaa kiakili.

pata gari kwanza ndil utajua ile sio rushwa ni bakshishi.
rushwa ziko mahospitalini huko unaombwa kama huna mgonjwa anakufa.
 
Mda huu saa sita kamili mchana hapa stendi ya Morroco kuna askari watatu wanakusanya hela hadharani kwa kila daladala inayosimama kituoni.

Takukuru tokeni maofisini muwakamate hawa majambazi katika nguo nyeupe.
Ni mfumo umerasimisha hilo ili viatu viwake
 
Ajabu ni kwamba mambo haya yako wazi sana siku hizi,Yani askari wala sio waoga kuomba rushwa ,mama yetu ana kazi kubwa sana ya kufaya reform jeshi la polisi upande wa traffic
Kama alishindwa report za CAG kuwachukulia hatua ndio traffic ataweza.
Hii nchi mifumo ilishakufa usiwaonee wivu wenzio
 
Hivi traffic wakifata Sheria kuna gari itatembea barabarani kweli.
Ni kusaidiana kitanzania Tanzania tu
Wakifuata sheria zipi hizo? Wewe bhana kama ni mmoja wao, kubali tu mnazingua. Maana mna njaa mpaka mnaboa. I wish ningekuwa Rais.

Hakika ningewatimua wote barabarani, halafu ningefunga camera tu za cctv kwenye maeneo yote muhimu. Dereva atakaye kiuka sheria za usalama barabarani kwenye hayo maeneo, ndiyo atahukumiwa sasa kutokana na makosa yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom