Kigogo wa traffic Temeke akithiri kwa rushwa;ni edward balele,. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo wa traffic Temeke akithiri kwa rushwa;ni edward balele,.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 27, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  TRAFFIC WASEMA TUMEMCHOKA KABISA

  MAKAMANDA wa polisi wa kanda ya Dar es salaam na taifa leo wanatarajia kumuweka kiti moto mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Temeke, Edward Balele kutokana na tuhuma kwamba operesheni ya kukamata magari yanayokiuka sheria imegeuzwa kuwa mradi binafsi.

  Makamanda wanaotarajiwa kumuweka kiti moto mwenzao ni kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Kanda, Mohamed Mpinga; kamanda wa polisi Dar es salaam, Suleiman Kova na kamanda wa polisi wa Temeke, David Msiime.

  Kamanda Mpinga aliliambia Mwananchi kuwa leo watakuwa na kikao cha Balele kwa nia ya kusikiliza maelezo yake dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

  “Hizo ni tuhuma nzito ambazo hatutarajii zingekuwepo... mimi nafanya juhudi ya kuondoa rushwa katika Jeshi la Polisi, halafu mtu mwingine anageuza mradi... hii ni aibu kwa jeshi hivyo leo mimi na Kamanda Kova, na RPC wa Temeke pamoja na msaidizi wa trafiki wa Temeke tutakutana na kumwita anayetuhumiwa ili atueleze mkasa wote,’’ alisema Kamanda Mpinga
  Mpinga alisema ameshaagiza makamanda mbalimbali waliopo juu ya kamanda huyo anayetuhumiwa, wampe taarifa kuhusu tuhuma ahizo anazodai kulichafua jeshi hilo kama zitakutwa kuwa na ukweli ndani yake.

  “Nimeshaagiza RPC wa Temeke, na msaidizi wa Balele waniletee taarifa kuhusu tuhuma hizo kwa kutumia utaalam wao wa kuzungumza na askari na naamini watatumia mbinu mbalimbali za kuchunguza na watanipa taarifa na leo baada ya kumuhoji anayetuhumiwa nitatoa taarifa kamili juu ya tuhuma hizo,’’ alisema Kamanda Mpinga.

  Juzi baadhi ya maaskari kitengo cha usalama barabarani wa Temeke waliiambia Mwananchi kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini kuwa wamekerwa na vitendo vya udhalilishaji dhidi yao wanavyofanyiwa na wameamua kuweka mambo hadharani.

  Walidai kuwa hutakiwa kupeleka kituoni magari matano kila mmoja na baadaye wenye magari hayo hutoa rushwa ya kuanzia Sh150,000 hadi 260,000 kulingana na makosa yao, lakini kadri siku zinavyokwenda wamekuwa wakidharauliwa na madereva kila wanapoowakamata, na wakati mwingine hudharauliwa kwa sababu mabosi wao huwaachia.

  Walisema kiongozi mmoja wa juu wa Temeke amekuwa akiwalazimisha askari wa kikosi chake hicho kila askari kukamata magari matano kwa siku na anayeshindwa kufanya hivyo humweka ndani kwa muda wa wiki, akimtuhumu kwa uzembe huku wengine akiwatishia kuwafukuza kazi.

  “Kuna askari wenzetu kama wawili wameshawahi kukumbwa na mkasa wa kufungwa walitakiwa kupeleka ela za magari matano hawakuweza kufikisha hivyo wakawekwa ndani kwa muda wa wiki moja jambo linalodhalilisha taaluma yetu, kwa kweli tumechoshwa na vitendo hivyo,’’ alisema mmoja wa askari hao.

  Vituo ambavyo vinatuhumiwa kutumika na maaskari hao katika ukamataji wa magari kutokana na amri ya mkubwa wao ni pamoja na Tazara, Veta, Mtongani, Tandika, Mabagala na Chang’ombe.

  “Tunachoshangaa madereva wanatakiwa kufikishwa katika mahakama za wilaya zinazohusika ili watozwe faini, lakini yeye anawafiksha mahakama ya jiji ambapo hutozwa faini ya Sh 20,000 ambapo si mahakama sahii kutokana na makosa waliyokamatwa nayo,’’ alisema

  Askari hao walifafanua kuwa Ijumaa iliyopita magari 10 yalikamatwa kutokana na makosa ya usalama barabarani na kupelekwa kituo cha Chang’ombe, lakini ni madereva wawili tu kati ya 10 ndiyo waliofikishwa mahakamani na wengine waliachiwa huru baada ya kutoa rushwa.

  Akizungumzia tuhuma hizo, Kamanda Balele alisema: “Tuhuma zinaweza kuwa sahii kwa kuwa kila mtu ana uhuru wa kuzungumza kulingana na upeo wake, lakini wee njoo ofisini tuzungumze nitakueleza yote; siwezi kuzungumza kwenye simu wewe unaweza kuwa ni mmoja wao au ni mpigadebe tu wa Mtoni Mtongani, hivyo njoo ofisini tuzungumze,’’ alisema Kamanda Balelel ambaye hata hivyo hakuweza kupaytikana ofisini kwake.
   
 2. k

  kidumeso Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Balele mimi namjua,ana magari mengi tu,ukilinganisha na siku alizoingia polisi siyo rahisi kupata mali hizo alizo nazo,kama nikitakiwa kutoausahhidi wa haya ninayo yasema,nitakuwa tayari,sio vizuri watu wachache kutuharibia jeshi letu zuri.
   
Loading...