TAKUKURU, kwanini mnaivua tena nguo CCM? Tuacheni tupumue jamani!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,047
2,000
Mngechuna tu. CCM sasa itadhalilika tena. Kuhusu madini,ilitubidi makada tujikaushe na kuwa vigeugeu kuhusu kuyalinda madini. Sheria na mikataba ilipofanyika sirini,makada tuliunga mkono na kushangilia

Wapinzani waliotaka uwazi wa mikataba na usawa wa kisheria walikuwa maadui zetu. Tuliwaponda bila kuwapenda na tuliwataka viongozi wetu chamani waongeze mwendo wa jembe na nyundo. Wapinzani walisema kwa kuhema,tukawakebehi kama watu wa Bahi. Mambo yakawa yalivyo

Sasa,bila aibu hata chembe hata ukubwa wa wembe,tunamshangilia Rais na Mwenyekiti wetu kurekebisha Sheria na kuianika mikataba. Ile ile ya wakati ule. Kwa jambo hili,CCM tukavuliwa nguo na kudhalilika kiuhakika. Lakini,kisiasa inakubalika.

Sasa TAKUKURU mnalenga kutuvua tena nguo wanaCCM. Kuanzia Mwenyekiti wetu hadi kada wa shina,msimamo wetu ni kwamba Escrow haikuwa pesa ya umma. Waliosema za umma tuliwazodoa na kuwashambulia kwa hoja za haja. Tulisema waliochota Escrow wamechota pesa zao. Na waligawa zao.

Wamehujumu vipi pesa zao? Itakuwaje waliogawiwa wote wakiunganishwa nao kama Mushi alivyounganishwa na Melo? Wote ni makada. CCM si itatikisika kuliko miti wakati wa masika? TAKUKURU,mngetuacha tupumue jamani

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,360
2,000
Mkuu VUTA-NKUVUTE,CCM haijavuliwa nguo na TAKUKURU leo wala jana,ilivuliwa nguo na nyinyi wenyewe wanachama wanafiki ambao hamuwezi kuwaeleza ukweli viongozi wenu kuwa wapo uchi zaidi ya kuwaambia nguo walizovaa zimewapendeza sana. Ni mpaka pale tu wanachama kwa umoja wenu mtakapoacha unafiki na kuwaeleza ukweli viongozi wenu kuwa wapo uchi na wao kujisitiri ndipo "uch." wa CCM hautaonekana tena. Inawezekana!?
 

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,211
2,000
Aisee ukisoma ile Hati ya Mashtaka ni hatari sana, ile inayosema kuwa, ..." Huku mkiwa si watumishi wa UMMA mkishirikiana na watumishi wa UMMA..." hapa lazima watumishi wa UMMA walioshirikiana na hawa jamaa waanze kuaga mitaani taratibu, halafu JPM mjanja, yeye kaamua kuanza na MAPAPA wenyewe maana wangekamatwa "vidagaa" tungelalamika...


Naona mpango uliopo mezani ni kuitupilia mbali IPTL na Mitambo yao, hongera sana JPM
 

Tarime one

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
2,248
2,000
JANA sisi CCM; hizo pesa za TEGETA-ESCROW sio pesa za umma, ni mali ya IPTL kabisa, wanawadai TANESCO hizo pesa, Rugemalira sio mtuhumiwa amelipa kodi yote., JK jembe, tunamuunga mkono kwa asilimia zote.

LEO sisi CCM; Safi, JPM jembe sana, safi sana, zile pesa za TEGETA-ESCROW ni mali ya umma, wakamatwe, IPTL hawafai, wametutia hasara sana, tunamuunga mkono JPM kwenye hili.., Rugemalira ni FISADI afungwe..

#My_Take; ukipewa akili za watu hawa wa CCM, basi tambua kabisa unaishi kwenye kundi la kuku ambao mchana wanakula mchele jioni wanaliwa kwa Wali.., Akili sawa na kifurushi cha Jaza Ujazwe!
 

Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,058
2,000
Sasa ccm kwa akili zao za makinikia unafikiri wanaweza kutambua kuwa wanajivua nguo kwa kila walifanyalo? Ila utafiti umeshatuambia aina za washabiki wa ccm (Maskini na wasio na elimu), ndio maana unaona wale waheshimiwa kutoka hicho chama chakavu cha makanikia kazi yao kuunga mkono kila hoja kwa kura ya ndiooooo pale bungeni, Lissu anawaita washangiliaji wa mfalme.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom