Uchaguzi 2020 Kwanini tunasema Magufuli mitano tena? Kwanini tunasema CCM mitano tena? 2020-2025

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Na: Giantist McWenceslaus
09/09/2020.
Dodoma.

Habari za leo, ndugu wanabodi wenzangu... Tangu uhuru hata sasa, Tanzania imeendelea kuwa salama, kwa sababu ya kuwepo kwa viongozi wazalendo na wenye kuwajali watanzania wenzao wote. Na usalama huo wa Tanzania, imesababishwa kwa kuwepo kwa haki na uhuru kwa watu wote waliopo ndani ya mipaka ya Tanzania. Na hiyo haikuja kwa sababu tulistahili ila ni kwa sababu viongozi wetu wote wa serikali chini ya CCM wamekuwa wakitoa haki na uhuru kwa watu wake. CCM na wanaCCM wote wanafahamu kuwa uhuru na haki ni mbegu ya amani na utulivu kwa nchi.

Tanzania imewahi kushiriki vita mbili moja kwa moja na ikashinda, ni ile vita ya Uganda na vita ya Msumbiji. Lakini Tanzania imeendelea pia kushiriki vita ambayo ilitangazwa rasmi katika azimio la Arusha 1967, na mpaka sasa Tanzania ipo katika uelekeo mzuri wa kushinda vita hiyo. Ni vita dhidi ya maadui ujinga, umasikini na maradhi. Siku chache nyuma niliwahi kusema humu namna ambavyo Tanzania imeweza kupambana na adui ujinga kupitia Sekta ya elimu. Hivyo basi leo nitaeleza namna ambavyo Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na adui maradhi. Na hii itaelezwa vizuri kupitia sekta ya afya.

Kama ilivyo kawaida ya vita, kuna wakati mnaweza mkarudi nyuma kidogo kwa lengo la kujipanga ama kushambulia huku mkiwa mnasonga mbele. Lengo ni moja, kumshinda adui. Kupitia Sekta ya afya kuna nyakati ambapo ilionekana kama adui maradhi anataka kutuzidi hivi. Lakini pongezi kwa serikali ya CCM na Jemedari wa vita Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuweka mikakati madhubuti ambayo imeisaidia Tanzania kupata uelekeo sahihi wa kummaliza kabisa adui huyu maradhi katika siku chache zijazo.

Ndugu zangu mtaji wa kwanza na wa muhimu katika kufanikisha jambo lo lote lile la Mwanadamu, ni afya njema. Afya njema ndio mtaji wa kwanza na wa msingi kabla ya mitaji mengine. Afya ya watu ni uzima na ndio afya ya Taifa, Taifa lenye watu wasio kuwa na afya bora, ni Taifa dhaifu. Hivyo basi leo nitawaeleza mafanikio yaliyopatikana kwa miaka Mitano katika vita dhidi ya maradhi, chini ya ilani ya CCM na kiongozi imara Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia mwaka 2015 hadi mwezi Julai, 2020. Kwa uchache zaidi, nitaanza kama ifuatavyo.

Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Dkt John Magufuli, imetekeleza mambo yafuatayo kwa maelekezo ya ilani ya CCM, katika mapambano dhidi ya adui maradhi.

Mosi, ujenzi wa Zahanati na vituo vya afya vya kutosheleza wananchi katika kutoa huduma za afya. Inajulikana kuwa hapo awali zahanati zilikuwa ni chache sana kwa idadi katika meneo mengi nchini. Kwa mfano, unakuta kata moja yenye vijiji vitatu na zaidi wakati mwingine, kuna zahanati moja tu ambayo inawahudumia wananchi zaidi Elfu moja!

Vivyo hivyo wilayani, wilaya nyingi nchini zilikuwa na hospitali chache ambazo zilikuwa hazina vitendea kazi, lakini wakati mwingine kulikuwa na wilaya ambazo zilikuwa hazina kabisa hospitali. Na kwa vile wilaya zilikuwa na hospitali moja tu, hivyo zikajikuta zikielemewa katika kutoa huduma kwa wananchi. Ikiwa ni pamoja na huduma ya uzazi kwa wakina mama na watoto n.k. Lakini hivi sasa chini ya uongozi wa Dkt. John P. Magufuli, serikali imeweza kuongeza na kujenga zahanati na vituo vipya vya afya katika kata na vijiji, pamoja na kuzikarabati hospitali kongwe za wilaya. Lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na huduma zingine kama afya kwa wazazi na watoto, kulaza wagonjwa, huduma za mochwari n.k rejea hospitali ya Makole, Mkonze, Kigogo n.k

Pili, upatikanaji wa dawa za kutosha pamoja na vifaa tiba za kutosha katika hospitali, zahanati pamoja na vituo vya afya vya umma. Inafahamika adha iliyokuwapo kwa wananchi katika utafutaji wa dawa, ilihitajika pesa nyingi ili kuweza kupata hata Panadol ama dawa za kawaida za kutuliza maumivu! Kutokana na ukosefu wa dawa ilipelekea hata baadhi ya wahudumu kuuza dawa kwa pesa nyingi. Ninahakika kuwa wananchi wengi wamekumbana na adha hii na bado hawajasahau.

Lakini hivi sasa, Dkt. Magufuli ameweza kurahisisha upatikanaji wa dawa na vifaa Tina vya kutosha kuwahudumia wananchi. Sasa hivi, dawa zinaoatikana bila usumbufu, kwamba ni miaka mitano sasa watanzania wameishi passport kugharamia pesa nyingi katika kupata dawa. Dawa zimekuwa na gharama nafuu kwa sababu zipo za kutosha katika mahospitali, lakini pia upo udhibiti madhubuti katika kuhakikisha hakuna urasimu utakaofanyika katika upatikanaji wa dawa.

Ninahakika jambo hili limepata kushuhudiwa na kila mtanzania ndani ya miaka mitano ya uongozi wa ilani ya CCM chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika suala hili la dawa, ni dhahiri kuwa lipo pamoja na suala la vifaa tiba kama ambavyo nimeshasema hapo mwanzo. Kipindi cha nyuma ilichukua muda mwingi kwa wagonjwa kuweza kuhudumiwa kutokana na ukosefu wa vifaa vya kupima magonjwa, lakini pia kukosekana na vitanda vya kutosha na mashuka katika hospitali nyingi. Na kwa jinsi hiyo, idadi ya vifo ilikuwa ikiongezekana, kwani wagonjwa walikufa kwa sababu hawakupimwa, na kama uwezekano wa kuwapima ulikuwepo basi hakuhudimiwa kwa kukosa pesa ya matibabu. Kwa hiyo kutokana na ukosefu wa vifaa tiba, kulisababisha gharama za huduma za aftya kuwa juu mno.

Lakini sasa, serikali chini ya Dkt. John Magufuli imejitahidi kuhakikisha Hospital zetu zote zinapata Vifaa tiba. Na kwamba wagonjwa watapimwa kwa haraka, na kupata matibabu kwa haraka kwa gharama nafuu. Na hiyo imesaidia katika kupunguza safari za wagonjwa wengi kwenda kutibiwa nje ya nchi, na hivyo kuokoa pesa nyingi sana. Lakini hiyo haitoshi, serikali imeenda mbele zaidi katika kuhakikisha vifaa tiba vya kupimia magonjwa makubwa, kama vile Xr-rays Mashine, CT-Scan, MRI, n.k. Ndio kusema katika juhudi hizo serikali ya CCM chini ya Dkt. JPM imeweza kuokoa maisha ya watanzania wengi na kufanikiwa kupunguza idadi ya vifo.

Tatu, uboreshwaji wa huduma ya afya kwa mama na mtoto. Adui maradhi amechukua maisha ya mama zetu wengi kutoka na mambo ya uzazi lakini pia amechukua maisha ya watoto wetu wengi went umri chini ya miaka mitano. Ilani ya CCM ya 2015 chini ya kiongozi wake Dkt. John Pombe Magufuli, ilijidhatiti kwa dhati kabisa katika kuyaokoa maisha ya mama na mtoto. Kwa kufanikisha uboreshwaji wa huduma ya afya kwa mama wajawazito, imesadia kupunguza vifo vya kina mama, kwa sasa huduma ya ulkuongezwa damu kwa mama anayejifungua ni bure! Miaka ya nyuma wakina mama wengi walikufa kutokana na kuishiwa damu nyingi wakati wa kujifungua.

Lakini pia kuanzishwa kwa vituo maalum vya kuwahudumia wakina mama na watoto tangu ujauzito na hata baada ya kujifungua mpaka mtoto anapofikisha miakata mitano na kuendelea. Hivi leo tunashuhudia kupungua kwa kasi kubwa vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito kutokana na huduma bora wanazopewa ambapo mama huhudumiwa tangu mimba ikiwa na mwezi mmoja!

Nne, uimarishaji na udhibiti wa huduma zinazotolewa idara ya uhifadhi wa madawa, inayofahamika kama Bohari kuu ya Dawa (MSD). Kwa miaka mitano mfululizo serikali imeweza kumudu vita dhidi ya maradhi kutokana na utendaji kazi mzuri ambayo imekuwa ikisaidiwa na Bohari kuu ya madawa nchini. Rais Dkt. John P. Magufuli, amefanikiwa katika kuiongezea weredi na Uzalendo watendaji wa Bohari hii, ili kwamba nguvu inaongezeka katika kumshinda adui maradhi. Tangu uongozi wake ni aghalabu kusikia ucheleweshaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vituo mbalimbali vya afya.

Tano, serikali ya CCM chini Dkt. John P. Magufuli kwa miaka mitano imeweza kupambana na maradhi ya TB, Malaria, UKIMWI, Kisukari, Kiarusi, Selinundu n.k kwa kuweka utaratibu wakutoa huduma za afya kwa wagonjwa wa magonjwa hayo, kwa gharama nafuu pamoja na kupewa uangalizi mkubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mfano TACAIDS. Lakini pia kwa kuajiri watalaamu wengi zaidi katika kada ya afya ili kuhakikisha maisha ya watanzania yanakuwa salama. Ndio kusema kwa miaka mitano vifo dhidi ya malaria imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, ambapo kipindi cha nyuma vifo vingi vilisababishwa na malaria! Kwa sasa vifo vinavyotokana na malaria ni vichache sana. Hata hivyo kwa baadhi ya magonjwa serikali ya CCM imeweza kuondoa gharama kabisa, mfano kwa wagonjwa wa TB wanapata matibabu bure; vivyo kwa dawa za kufubaza VVU, dawa zake hutolewa bure bila malipo kuanzia kwa watoto mpaka kwa watu wazima. Hiyo ndiyo CCM na huyo ndiye Dkt. John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya maradhi! Lakini pia kupunguzwa kwa kodi ya vifaa vya kutibu magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari, Kiarusi, saratani n.k ikiwa ni sehemu ya kuongeza na kuimarisha mapambano dhidi ya adui maradhi.

Nilisema kuwa "Bunduki ni silaha ya ulinzi, Elimu ni silaha ya kuleta maendeleo ya mtu na taifa kwa jumla." Na leo nasema hivi "kumekuwepo na rasilimali watu, rasilimali fedha na rasilimali vifaa ili kuwezesha shughuli ama biashara za watu kwa ajili ya kuleta maendeleo ya watu na ya Taifa kwa jumla, lakini bila afya ya watu kuwa bora vyote hivyo ni ubatili mtupu!"

Mwanzoni mwa mwaka huu, Tanzania na Dunia ilipata pigo kwa watu wake wengi kushambuliwa na adui ugonjwa wa Covid-19. Kwa kweli uchumi wa watu na wa Taifa umeyumbishiwa kwa kiasi kikubwa, na watu wengi walipoteza maisha. Ugonjwa huo ulisababisha hata baadhi ya shughuli kufungwa na mwishowe Dunia yote ilijawa na hofu si kwa wakubwa wala watoto, masikini wala tajiri. Tanzania chini ya Jemedari Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imetumia njia ya maombi na ya kumtimizia Mungu katika kupambana na ugonjwa huo, hakika Mungu amesikia maombi ya watanzania. Ndio kusema Tanzania chini ya CCM imeweza kuwa ni nchi ya mfano kwa mataifa mengine Duniani katika kutekeleza mapambano yake dhidi ya adui maradhi.

NINAHAKIKA TUTAISHINDA VITA DHIDI YA MARADHI, KAMA TULIVYOISHINDA COVID-19 KATIKA NAMNA AMBAYO DUNIA HAIKUTEGEMEA. WATANZANIA WANAOWAJIBU WA KUICHAGUA TENA CCM NA KUMCHAGUA TENA MAGUFULI KATIKA KUYAENDELEZA MAPAMBANO HAYO KWA MIAKA MITANO MENGINE.

Kifo ni wajibu wa kila kiumbe chenye uhai, lakini mapenzi ya Mungu kwa watu wake waishi maisha marefu ikiwa tu watawaheshimu wazazi wao. Lakini vifo vya maradhi ni umasikini, ninahakika watanzania wanaweza wakaishi maisha marefu zaidi ikiwa tu tunaishinda vuta dhidi ya maradhi. Leo hii umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 65, tofauti na miaka mitano iliyopita ambapo ulikuwa ni miaka 55!

Sauti ya Mdodomia
Dodoma

CHAGUA CCM
CHAGUA MAGUFULI
MITANO TENA

ILI KUBORESHA HUDUMA YA AFYA YA WATU NA TAIFA KWA JUMLA. BIMA YA AFYA KWA WATANZANIA WOTE INAKUJA!

TUKUTANE OKTOBA 28 KURA ZOTE KWA MAGUFULI
 
Kwa mtu mwenye akili Timamu hawezi kumchagua Magufuli Oktober 28.

Tumeshuhudi Kwa kipindi kifupi cha mkaka mitano kukiwa na sintofahamu Nyingi sana.

: Tumekuwa na mpasuko mkubwa wa kitaifa.
: Kuvunjwa kwa Utengamano wa Kitaifa.
: Kuvujwa kwa Diplomasia yetu.
: Matendo mengi ya kikatili na kinyama.
: Kukurupuka kwa Huyu kiongozi katika maamuzi mengi.
: Udini Ukabira na ukanda.

Inatosha kwa sasa
 
Mkuu kama kweli upo Dodoma naomba unisaidie haya machache tu.

1. Mwaka 2017 Rais alisitisha sherehe za uhuru akasema fedha itakwenda kwwnye ujenzi wa Hospital ya uhuru Dodoma je Hospita ya uhuru leo 2020 Imekamilika????

2. Rais na Mfalme wa Moroco walituahidi ujwnzi wa Uwanja Mkubwa wa Michezo Dosodma tangu mwaka 2017. Je umeanzwa hata kujengwa?

3. Rais 2016 alituahidi kuwa fedha zipo na Anataka kuanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato je ujenzi umeanza?

4. Vipi kuhusu ahadi ya Ujenzi wa Barabara ya pete kuzunguka mji Ring road Imekamilika?

5. Hivi unajua Dododma Jiji halina hata stand kituo cha mabasi chenye Lami?
Ukiondoa jamatini palipofutwa?

Ukinijibia haya tu nitamuunga mkono JPM.
 
Back
Top Bottom