Kizuri kinajiuza,kibaya kinajitembeza.Hili la Bandari CCM mnajitembeza.

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
943
1,988
Ukweli ni kwamba,
Kama kuna kitu kimewapa Hali ngumu CCM na Rais kwa ujumla basi ni hili Sakata la bandari.
CCM kwenye corridor nakutana nanyi na uzuri ni kwamba baadhi yenu mnakiri kabisa kwamba kwa hili tumeingia chaka na hatujui hatima yake hasa 2025. Baadhi mnakiri kabisa tuna wakati mgumu Sana kumsafisha mgombea wetu kuliko wakat wowote ule.
Uhalisia ni kwamba nchi nzima wasomi na wasio wasomi na matabaka mengine wanajua bandari imeuzwa.
Kuna ugumu Sana kuwabadilisha wananchi wa kawaida kutoka kuamini kuwa haijauzwa.
Mnafanya mikutano ya kisiasa kunadi uzuri wa mkataba wa uwekezaji wa bandari lakini maswali wanayoulizana wananchi ni;
1. Kwanini mnatumia nguvu na gharama kubwa kuitetea huu mkataba?
2. Ni kweli wananchi waamini mkataba ni mzuri kwa maneno ya wasira,ambaye Hana wasifu mzuri huko nyuma.
3. Kama hata Wana CCM wenyewe wamejitokeza hadharani na kuukataa mchana kweupe mfano,mama Tibaijuka ambaye ni msomi mkubwa amediliki kuuita ni zimwi na ameshangaa ulifikaje Ikulu, mzee warioba ameukataa,mzee Butiku ameukataa, Adamu Malima ameukataa,lakini pia wasomi wengine kama akina shivji pamoja na wengine wengi tu wameukataa.
Leo hii wasira na chongolo ndiyo waeleweke? Jamani hata aibu hamuoni.
Katibu MWENYEZI taifa wa CCM anasema eti "kama bandari imeuzwa mbona haijatiwa mfukoni na kuondoka,mbona Bado ipo hapa"
Ni mshangao kuona hoja za namna hii.
Namna mnavyoitusha mkutano na kunadi uwekezaji huo mbovu ndiyo wananchi wanadharau kweli na kama wanajaa ni kwasababu wanakuja kuona wasanii tu lakini hawatoki na hoja za bandari kuwa zinatija kwa nchi.
Najua mnajua na kama hamjui ni kwamba, wapo Wana CCM wasomi na wapo kwenye utawala hawajapendezwa kabisa na mkataba huu na badala ya wao kusema hadharani wanawatumia wananchi kulinda usalama wao ndani ya chama.
Mwisho.Huu mkataba utawamaliza CCM. Ki ukweli tunajiuliza wengi ilikuwaje ukasainiwa,hata Mimi nimeusoma kwa elimu niliyopata hapahapa nchini katika vyuo vyetu vinavyotambulika nimeshangaa kuona Rais wa nchi ametoka Baraka kwa waziri usainiwe,jamani kweli unaweza ukakabidhi nchi kwenye mkataba wa namna Ile,Duuuu! Rais aliusoma kweli??na kama aliusoma Nini kilimpata?waziri uliyesaini Nini kilikupata?nyie wote mliosaini na mnaozunguka nchi nzima kuunadi ni Watanzania Wenzetu kweli? Na kama ni Watanzania Nini hasa ajenda yenu?hamuoni aibu?
Hivi Watanzania wote Hawa wanaopinga ni wajinga?hawana akili? Nyinyi peke yenu ndiyo mna akili siyo?
Nilitegemea mtoe kauli moja tu kwamba, tumewasikia Watanzania na sasa tuna ufuta na kuanza majadiliano upya. Badala yake Bado mnakomaa nao tu. Leo tuna kesi nyingi tumeshindwa kwenye mikataba ya namna hii,tumeshindwa kwasababu ya vipengele vya namna hii hii .Bado Tena mnataka kule mbele tushindwe hivi hivi. Ndugu zangu nyie vipi?
Ni kichaa tu anaweza Saini mkataba wa namna Ile.✍️
Li mkataba limemporomosha Rais kukubalika kwake kwa wananchi na yeye pia kagundua hivyo na ana aibu usoni kwa kumuungalia tu.
Ufuteni plz,ufuteni plz msitumie gharama na fedha za wananchi kuzunguka nchi nzima kunadi kitanzi cha baadae,hizo fedha za mikutano zitumike mahala pengine kuleta maendeleo. Yaani hamuoni aibu. Pesa za Watanzania mnazitumia kuendeshea mikutano ya kutetea mkataba mbovu kama huu. Hii ni double dehumanization. Yaani mnawapiga kote kote.
Stop it okoa bandari zetu. Na wewe CDF ingilia hili plz hatutakuwa salama kimipaka Jamaa wakipewa kwa namna ulivyoandikwa kwasasa labda ubadilishwe.
Tanzania 🇹🇿 ni yetu sote.
 
CCM mmerighalimu sana Taifa hili kwa mikataba yenu mibovu na kuendekeza rushwa na ubinafsi ila hakuna marefu yasio na ncha, mwisho wenu utakuwa wa aibu na mchungu sana. LAANA ya kuwadhulumu na kuwanyanyasa WATANGANYIKA IKAWASHUKIE NYINYI NA VIZAZI VYENU kwa jina la mwenyezi Mungu. Amina
 
Back
Top Bottom