TAKUKURU, kwanini mnaivua tena nguo CCM? Tuacheni tupumue jamani!

Jana Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu akizungumza na gazeti hili, alisema sakata hilo linatakiwa liishe kwa kuwa linaumiza uchumi wa nchi kwa kuwa mtambo wa IPTL ni matatizo.

"Hili jambo kwa namna yoyote lazima liishe na kwamba mwisho wake ni bora tutaifishe ule mtambo na ufie mbali," alisema Mangungu.
Wewe unasemaje kuhusu undumila kuwili wa macc? achana na maoendekezo ya bunge wala sijui mbunge nani kasema nini!! nataka naoni yako wewe jingalao.
 
Tulisema fedha sio za serikali leo nini kitatokea kama sio upofu. Unaiba unasema sijaiba Je kama ni mahakani mtumiwa angefanyiwa nini basi kilichostahili inatakiwa tukipate sisi wanaccm ambao leo hii ni watuhumiwa. Hili hatuwezi kulipinga kiwepesiwepesi tukiwa kama watuhumiwa
 
Nimekupata RC!

Mzee Tupatupa

Loooo unaniita nani ha ha haaa

wewe ndio uko nae huko jikoni mnatuendeshea nchi. Vipi umeshapewa cheo chochote na Mkulu au upo ulipokuwa tangu enzi za Kikwete?

Naona siku hizi unakuwaga kama vile haupo nao, labda siku moja utatueleza nini kinajiri.
 
Mngechuna tu. CCM sasa itadhalilika tena. Kuhusu madini,ilitubidi makada tujikaushe na kuwa vigeugeu kuhusu kuyalinda madini. Sheria na mikataba ilipofanyika sirini,makada tuliunga mkono na kushangilia

Wapinzani waliotaka uwazi wa mikataba na usawa wa kisheria walikuwa maadui zetu. Tuliwaponda bila kuwapenda na tuliwataka viongozi wetu chamani waongeze mwendo wa jembe na nyundo. Wapinzani walisema kwa kuhema,tukawakebehi kama watu wa Bahi. Mambo yakawa yalivyo

Sasa,bila aibu hata chembe hata ukubwa wa wembe,tunamshangilia Rais na Mwenyekiti wetu kurekebisha Sheria na kuianika mikataba. Ile ile ya wakati ule. Kwa jambo hili,CCM tukavuliwa nguo na kudhalilika kiuhakika. Lakini,kisiasa inakubalika.

Sasa TAKUKURU mnalenga kutuvua tena nguo wanaCCM. Kuanzia Mwenyekiti wetu hadi kada wa shina,msimamo wetu ni kwamba Escrow haikuwa pesa ya umma. Waliosema za umma tuliwazodoa na kuwashambulia kwa hoja za haja. Tulisema waliochota Escrow wamechota pesa zao. Na waligawa zao.

Wamehujumu vipi pesa zao? Itakuwaje waliogawiwa wote wakiunganishwa nao kama Mushi alivyounganishwa na Melo? Wote ni makada. CCM si itatikisika kuliko miti wakati wa masika? TAKUKURU,mngetuacha tupumue jamani

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Watu kama wewe ndio mnaosababisha hata rais aamue kufumbia macho mambo haya yaliyopigiwa kelele bila hatua yoyote. Na ukweli akiamua kufumbia macho na kuendelea kama wenzake waliopita anaweza na hakuna lolote mtaifanya ccm na uchaguzi ukifika watashinda kwa kishindo. Tumuombee Mungu Rais bila kulete ushabiki wa kisiasa au upepo unaweza kumbadili tukajikuta hali imebaki ilivyokua.
 
Wewe unasemaje kuhusu undumila kuwili wa macc? achana na maoendekezo ya bunge wala sijui mbunge nani kasema nini!! nataka naoni yako wewe jingalao.
Nimeomba kuonyeshwa tamko la CCM kuhusu Esxrow.

Nimeomba kueleweshwa kwa nini Deo Filikunjombe mwanaccm alikesha kupambania suala la escrow...akiwa na wanakamati wengine ambao wengi wa ni wanaccm.

Nimekuletea quote ya mbunge wa kilwa alipohojiwa na gazeti la mwananchi kipindi kile cha escrow.

Wabunge wa CCM kwa wingi wao waliunga mkono azimio la bunge.

Sasa hicho mnachokiita undumilakwili kiko wapi?

Fuatilia posts zangu kuhusu escrow utaelewa msimamo wangu.

Mimi sio Kubene,Lissu au Mbowe waliosema lowasa ni fisadi halafu baadae wakabadilisha.
 
Hakuna mtu mnafiki na mzandiki Kama wewe kiumbe unayejiita Mzee Tupatupa wa Lumumba.
Kwanza kabisa unajulikana wewe ni Kada wa Chama gani. Pili, umejivisha Ukada wa Chama tawala ili kuhadaa watu. Hizo sarakasi na mauno unayokata mwisho ya siku yatakuvua wewe nguo kweupeeee mbele ya watoto na wakwe zako.
Za Mzandiki ni 20.....muda utakufichua. Umejaa Chuki na Visasi kama umeibiwa Mke na Dada yako na mtu mmoja. Pathetic.
Sijawahi kuchukia binadamu maishani, Ila sipendi viumbe Kama nyinyi mnaotujaza Chuki sisi walala hoi kwa manufaa yenu binafsi.
Ilhali ikifika wakati mnaenda kuchukua Posho na ruzuku kutoka Serikalini. AIBU YENU!
 
Mngechuna tu. CCM sasa itadhalilika tena. Kuhusu madini,ilitubidi makada tujikaushe na kuwa vigeugeu kuhusu kuyalinda madini. Sheria na mikataba ilipofanyika sirini,makada tuliunga mkono na kushangilia

Wapinzani waliotaka uwazi wa mikataba na usawa wa kisheria walikuwa maadui zetu. Tuliwaponda bila kuwapenda na tuliwataka viongozi wetu chamani waongeze mwendo wa jembe na nyundo. Wapinzani walisema kwa kuhema,tukawakebehi kama watu wa Bahi. Mambo yakawa yalivyo

Sasa,bila aibu hata chembe hata ukubwa wa wembe,tunamshangilia Rais na Mwenyekiti wetu kurekebisha Sheria na kuianika mikataba. Ile ile ya wakati ule. Kwa jambo hili,CCM tukavuliwa nguo na kudhalilika kiuhakika. Lakini,kisiasa inakubalika.

Sasa TAKUKURU mnalenga kutuvua tena nguo wanaCCM. Kuanzia Mwenyekiti wetu hadi kada wa shina,msimamo wetu ni kwamba Escrow haikuwa pesa ya umma. Waliosema za umma tuliwazodoa na kuwashambulia kwa hoja za haja. Tulisema waliochota Escrow wamechota pesa zao. Na waligawa zao.

Wamehujumu vipi pesa zao? Itakuwaje waliogawiwa wote wakiunganishwa nao kama Mushi alivyounganishwa na Melo? Wote ni makada. CCM si itatikisika kuliko miti wakati wa masika? TAKUKURU,mngetuacha tupumue jamani

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mjomba usiwe na wasiwasi,hiyo pia ITAPITA kama MAKINIKIA.!Hakuna cha Mla Rushwa wala Mla Ufisadi tunatafuta Front page tu
 
wewe ccm gani? acha wanaojua kusimamia rasilimaliza nchi wafanye kazi,uongozi ni inborn wengine walishindwa na huyu kwa kipindi kifupi ameweza,tumuunge mkono
 
Mim Kama mwana ccm nakijua chama changu vizuri..... Ngoja mtasikia kwa!ba takukuru imebaini kwamba pesa hazikuwa za uma au hatuna ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa
 
Back
Top Bottom