CCM wanajuana hakuna asiye mwizi huko. Hakuna anayewaza ya Kakoko. TAKUKURU fafanueni kuhusu tozo zinazotunyima usingizi mitaani

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Hakuna mwananchi asiyependa maendeleo lakini tozo zenu zimekuwa mwiba mkubwa kwa wananchi hilo mnalijua badala ya kupunguza matumizi makubwa Serikalini nyie mnazidi kuongeza mzigo kwa wananchi

Habari ya Kakoko kupelekwa TAKUKURU hayo ni mambo yenu kwani CCM hakuna aliyemsafi, mkisema mchunguzane kauli mbiu yenu ni chukua chako mapema kashifa za bandari na maeneo mengine zimetajwa na CAG hakuna sehemu hamkupoteza mapato tena kwa wizi.

Huko nyuma tumeshasema nyie ndio mnaoandaa kila kitu kuanzia sheria hadi mikataba hadi bajeti zote za nchi kwani walio wengi ndio hupewa kipaumbele kupitusha sheria mbovu na CCM ni nyie wenye sauti bungeni mkitofautiana mitazamo mnazikana mnaachiana nyie wenyewe. Tumeona kashfa za IPTL na ESCROW yupi aliyetiwa hatiani kwa kula fedha za umma? jibu ni hapana mnachofanya ni kudanganya wananchi kuwa mnachukua hatua kumbe huko mmetofautiana kimtazamo! Kuna msemo wengi wanaopenda kuutumia kuwa CCM ni ukoo wa panya hii ni kweli kabisa mkurugenzi anakuka kwa urefu ya kamba yake; DAS hivyo hivyo , RC, RAS, Mawaziri n.k. wanakula kwa urefu ya kamba yao.

Tunachokiomba fafanueni kuhusu tiozo hizo ambazo zimeleta taharuki kwenye jamii kukaa kimya Waziri wa Fedha bila kufafanua kunaketa sintofahamu kwenye jamii!

Masuala ya sensa na Kakoko hayawezi kutusahaulisha jambo hilo kwani hili kila siku linatuumiza, Kakoko na TAKUKURU hayo ni yenu mkitifautiana huko maana nyote ni wapigaji tu.
 
CCM walivyokuwa wajinga watakuja na movie moja Matata Sana ya kuwahamisha watanzania ili wasijadili tozo..nadhani Huko waliko wapo location wakitengeneza TUKIO LA KUFUNGIA MWAKA.
shida kubwa IPO Kwa wanaichi wengi ni mafala wa kupeperushwa na upepo,nahisi upepo wa safari hii utapitia Kwa vilabu hivi viwili vya Simba na yanga kwasababu huku Ndiko wajinga wamejaa wengi
 
Takukuru hawana cha kusema wala kufanya, kama maagizo ni ya kutoka juu...
 
CCM walivyokuwa wajinga watakuja na movie moja Matata Sana ya kuwahamisha watanzania ili wasijadili tozo..nadhani Huko waliko wapo location wakitengeneza TUKIO LA KUFUNGIA MWAKA.
shida kubwa IPO Kwa wanaichi wengi ni mafala wa kupeperushwa na upepo,nahisi upepo wa safari hii utapitia Kwa vilabu hivi viwili vya Simba na yanga kwasababu huku Ndiko wajinga wamejaa wengi
Watanzania ni watu makini sana mkuu, wanaweza wakawa wanahoji kuhusu ubadhilifu wa mali za umma hadi misuli ya shingo inawatoka.

Ghafla ikivuja video ya ngono,wote wanaacha kuhoji hutojua mzee ni yupi na kijana ni yupi, wote wanaanza kuhoji ilipo hiyo video na ni vipi wanaweza kuipata.

Watanzania ni watu makini sana.
 
Back
Top Bottom