TAKUKURU, Kawe kuna mteja wenu mzuri sana wakati wa usiku

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Wakuu amani iwe kwenu!

Leo sina mengi ila nataka niwaombe wajomba zangu wa TAKUKURU kwamba kuna wateja wao Kawe tena wateja wakubwa sana. Leo usiku wateja hao walikuwa wanapita nyumba kwa nyumba na kila mwenye kitambulisho cha kura alikuwa anakula pesa halali za kitanzania kati ya 30000/= na 40000/= Familia ya mjomba wangu wanaoishi nyumba moja watu 6 wenye vitambulisho walikula sh 180000/=

Mimi nimewapa taarifa kazi ya kujua hiyo rushwa inatolewa na nani ni kazi yenu, fanyeni ziara Kawe usiku kuanzia saa tatu kuendelea. Nawashukuru kwa imani kwamba mtalifuatilia hili nina imani kwamba huu ni muda wa TAKUKURU kufanya kazi usiku na mchana ili tupate viongozi wanaotokana na kura na si rushwa. kwa pamoja tutokomeze rushwa ya uchaguzi.

Kindi.
 
Kuleni Pesa zao ni zenu hizo wala msiwaonee huruma ,kura pigeni panapo stahili.Hao Takukuru hawana Meno mbele ya Chama Tawala.Yupo anae gombea nafasi ya Ubunge na alisha wekwa korokoroni kwa Kosa la Uhujumu Uchumi na sasa yupo Huru uraiani.
 
Askofu anatoa rushwa? Katukana Sana Islam huyu hakujua siku moja angewahitaji, Islam wa Kawe msimpe Kura, hela zake kuleni kura mpeni mwingine, pamoja nakuishabikia kijani kwa kawe ningempa mwingine
 
Anaomba takukuru wasiende waache huyoanaetowa rushwa andelee kuwapa nipesa zao zimewatesa miaka 5 leo wanaletewa ilanawaomba wasimpe kura huyo anaetoa rushwa kwani akifika atatamani kurudisha alichotoa nafaida hiyondiokanuni
 
Siku za mwisho watakuja manabii wengi was uongo, watawadanganya wengi na wengi watadanganyika.
 
Kuleni Pesa zao ni zenu hizo wala msiwaonee huruma ,kura pigeni panapo stahili.Hao Takukuru hawana Meno mbele ya Chama Tawala.Yupo anae gombea nafasi ya Ubunge na alisha wekwa korokoroni kwa Kosa la Uhujumu Uchumi na sasa yupo Huru uraiani.
Njombe moja hiyoooo.
 
Back
Top Bottom