TAKUKURU Katavi, yawafikisha Watumishi saba kizimbani kwa ubadhilifu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Katavi imewafikisha mahakamani watumishi saba wa serikali kwa tuhuma za kujihusisha na ubadhilifu wa fedha za serikali zaidi ya shilingi bilioni 1.23

Akizungumzia ubadhilifu huo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Faustine Maijo amesema kufuatia uchunguzi waliofanya kwa muda wa zaidi ya wiki mbili uliowahusisha watumishi hao, walibaini kufujwa kwa fedha na watumishi hao kutoka Halmashauri ya Mpimbwe, Manispaa ya Mpanda na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katavi.

Maijo amesema fedha hizo ambazo zilikuwa kwenye akaunti ya halmashauri ya Mpimbwe zimefujwa na watumishi kwakudanganya kuwa walikua wakiwalipa wakandarasi waliofanya shughuli mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Amesema uchunguzi umethibitisha kuwa fedha hizo ambazo ni zaidi ya bilioni moja zililipwa kwa watu binafsi ambao hawakua na kazi zozote walizofanya katika halmashauri hiyo na walikuwa ni watu ambao wanafahamiana nao.

Kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2023 imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi Gway Sumaye na mwendesha mashtaka Gregory Mhangwa amesema watuhumiwa wanashitakiwa kwa makosa matatu kujihusisha na genge la uharifu, uhujumu uchumi na wizi.
 
Duuuh ,Hizo ni athari za kupanda ghafla kwa dola, wenyewe mirija yao ilikuwa inavuja.....ila wasihofu watatoka 🤔🤔
 
Mgao wa bil. 1.23 kwa watu 7 si haba, kwa mwendo huu wa kugawana pesa za umma maendeleo kwa wananchi itabaki kuwa ndoto. Nafikiri tumefikia hatua ambapo pesa ya umma haiogopwi tena kama ilivyokuwa enzi za mwalimu.
 
Hela wamekula na kesi watashinda na watarudishwa kazini na kulipwa.

Hii ni Tanzania.
Ndiyo maana mimi kuamini wala kufuatilia kesi zinazoibuliwa na hao Takakuru nilishaacha.

Hakuna kesi hata moja niliowahi kushuhudia wakishinda!

Nilishawaweka kwenye kundi la "genge maslahi".

Wanaoshindwa kufikia "bei" ama kwa maagizo ya wanasiasa ndiyo huburuzwa mahakamani na mwisho wa siku ambo huisha kimya kimya.
 
Ndiyo maana mimi kuamini wala kufuatilia kesi zinazoibuliwa na hao Takakuru nilishaacha.

Hakuna kesi hata moja niliowahi kushuhudia wakishinda!

Nilishawaweka kwenye kundi la "genge maslahi".

Wanaoshindwa kufikia "bei" ama kwa maagizo ya wanasiasa ndiyo huburuzwa mahakamani na mwisho wa siku ambo huisha kimya kimya.

Hakuna wala rushwa wakuu kwenye hizi kesi kama hao takukuru.
 
Back
Top Bottom