.....Siku zote jifunze toka kwa waliofanikiwa sio toka kwa walioshindwa......
Mkuu naomba ruhusa nipingane na wewe mubashara.
Haijalishi mnafanya shughuli inayofanana, kila mtu anapata changamoto yake.
Wakulima wa tikiti mpo wilaya moja but still kila mtu anapata changamoto tofauti.
Usiwapuuze waliofeli kisa walifeli, hapo pia kuna somo tena kubwa.
Katika kilimo, hali ya hewa, aina ya mbegu, kanuni bora za kilimo, magonjwa, wafanyakazi, na soko ni vitu vinavyodetermine faida.
Kuna watu waliuza nyumba, wakanunua gari/tax. Biashara ya tax ikaenda ndivyo sivyo. Mpaka sasa wanaishi maisha magumu sana. Hapo kuna somo kubwa sana.
Kuna watu walichukua mikopo kwa dhamana ya nyumba, biashara zikaenda vibaya, nyumba zikapigwa mnada wakawa masikini. wakati kuna wengine wanachukua mkopo na anaulipa na faida juu.
Aliyefeli akikweleza utajifunza pale. Hivi mtu anapokwambia "kantangaze"/tuta absoluter imesababisha nitoke patupu hakupi somo au mpaka likukute mwenyewe upate ukichaa ndo upate somo?
Au Mfuga kuku anakwambia vifaranga 600 vimekufa vyote hakupi somo??
Wewe unaloliita somo ni pale mtu akikwambia nimeuza nyanya nikawa tajiri,
Ama nimefuga kuku nikawa tajiri!!
Tujitafakari, tusidandie kitu kwa sababu fulani alifanya na akafanikiwa.