TAJA - Mzee Mengi haheshimu viongozi wa Zanzibar?

Enigma

Senior Member
Feb 29, 2008
109
62
Kwa mara nyingine malalamiko yametolewa dhidi ya Mmiliki wa vyombo vya habari vya IPP Bw. Reginald Mengi. Huko nyuma amewahi kulalamikiwa na Mbunge wa Mkuranga Mhe. Adam Malima na muda si mrefu uliopita amelalamikiwa na mfanyabiashara mwingine Bw. Yusuph Manji.

Hata hivyo safari hii analalamikiwa na chombo cha TAJA (Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania). Katika barua ifuatayo ambayo nakala yake ametumiwa Rais Kikwete watu wataja wanatoa madai mazito na yenye utata dhidi ya mzee Mengi. Hata hivyo kwa yeyote atakayesoma kwa macho huru ataona kitu kingine kilichofichika.

Amueni wenyewe uzito, ukweli, na mantiki ya madai haya.
 
Attachments

 • picture 001.jpg
  picture 001.jpg
  451.8 KB · Views: 244
 • picture 002.jpg
  picture 002.jpg
  537.3 KB · Views: 198
 • picture 003.jpg
  picture 003.jpg
  392.6 KB · Views: 158
Mhhh

This doesnt look good. Mengi kashindwa vipi kununua influence huko TAJA? Maana wao at most wanaonekana ni ma Obsolete tuu hawana jipya

hivi zile pesa za UN AIDS ambazo alidai kaibiwa CRDB ziliishia wapi?
 
Kwa mara nyingine malalamiko yametolewa dhidi ya Mmiliki wa vyombo vya habari vya IPP Bw. Reginald Mengi. Huko nyuma amewahi kulalamikiwa na Mbunge wa Mkuranga Mhe. Adam Malima na muda si mrefu uliopita amelalamikiwa na mfanyabiashara mwingine Bw. Yusuph Manji.

Hata hivyo safari hii analalamikiwa na chombo cha TAJA (Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania). Katika barua ifuatayo ambayo nakala yake ametumiwa Rais Kikwete watu wataja wanatoa madai mazito na yenye utata dhidi ya mzee Mengi. Hata hivyo kwa yeyote atakayesoma kwa macho huru ataona kitu kingine kilichofichika.

Amueni wenyewe uzito, ukweli, na mantiki ya madai haya.

Ahaaa, sijui kwanini...! Lakini lazima kuna jambo hapo ....!
 
tusubiri ukweli si mida utakuja njee wacha tufatilie huko jikoni?

lkn mbona SMZ wenyewe wako kimya au wao wamelichukulia vipi?

nnashindwa kuunganisha mistari isije kuwa ni vita vya wengine hutumiwa wengine kuwa muhanga kufanikisha yao
 
I have a big doubt over this Association. Who are members of this association? Mh! Let's go thru these allegations and dig up the truth
 
Kwa mara nyingine.. watu wanakubali kubebeshwa mabomu.... Kazi kweli kweli!!!!!
 
TAJA, hawaonekani popote kwenye maslahi ya waandishi wa habari, kimekua kikundi cha watu wachache kwa maslahi binafsi, si chombo cha waandishi wa habari. Angalia TAMWA (Ananilea Nkya), MISA-Tan (Ayubu Rioba) ambavyo vimekua mstari wa mbele kupambana na serikali na ukiukwaji wowote wa maslahi ya wanahabari... JF tusikubali kutumika. Kama kweli ni wana habari mbona hawajafanya Press Conference? Wanahabari wana vyombo vya habari kwanini waje JF? ama kwa sababu wanaona hakuna Editor? nadhani Invisible ni editor, ondoa huu uchafu
 
Labda pia wangefanya uchunguzi wa matangazo ya vifo Radio One kutawaliwa na watu wa sehemu moja
 
TAJA, hawaonekani popote kwenye maslahi ya waandishi wa habari, kimekua kikundi cha watu wachache kwa maslahi binafsi, si chombo cha waandishi wa habari. Angalia TAMWA (Ananilea Nkya), MISA-Tan (Ayubu Rioba) ambavyo vimekua mstari wa mbele kupambana na serikali na ukiukwaji wowote wa maslahi ya wanahabari... JF tusikubali kutumika. Kama kweli ni wana habari mbona hawajafanya Press Conference? Wanahabari wana vyombo vya habari kwanini waje JF? ama kwa sababu wanaona hakuna Editor? nadhani Invisible ni editor, ondoa huu uchafu

Naona hayo madai yao kwa kiasi kikubwa yanahusisha kwamba Mengi anatubagua waislamu, na kwamba kwa kuwa TAJA inaongozwa na Waislamu ndio maana habari zake hazitoki. Lakini mbona hivi karibuni nilisoma habari kwenye magazeti ya Mengi kuwa Baraza La Habari la Waislamu lilifanya press conference pale maelezo na kutangaza kuwa wananchi waichukie CCM kutokana ufisadi na kuwapongeza Dr Slaa na Zitto kwa kuibua ufisadi? Sasa kama Mengi anachukia waislamu kwanini hakuacha kuandika habari hii ya Baraza la Habari la Waislamu? Kwani TAJA ni chama cha wanahabari waislamu? Kwa kweli TAJA mmeidhalilisha SMZ kwa barua yetu. Kama wao ndio waliwatuma basi wote mmejidhalilisha.

Asha
 
duh..!! kilichonishinda mimi ni hiyo lugha iliyotumika. Yaani, kama hawa ndio waandishi na ndio wanajaribu kujenga hoja basi tumekwisha. Zaidi ya yote, kwanini ni wao walalamike? Kama kuna unfair treatment ni serikali ya Zanzibar ndio wangekuwa na sababu ya kulalamika? Je, vyombo vya Zanzibar vinawataja vipi viongozi wa muungano au watu maarufu? Je vyombo vingine vya habari viliripoti kwa kina kiasi gani suala la Shamuhuna?

Wao wenyewe wanaituhumu MCT kuwa ni maswahiba wa Mengi, sasa kwanini wanapeleka malalamiko yao kwake? Hivi wakikataliwa si watasema "tulijua" na wakikubaliwa watasema "tumeogopwa"?

Sidhani kama kuna sababu ya kuondoa; lakinin ni vizuri watu waone na wapime kwa sababu hatuwezi kujua mawazo ya kijinga tusipoyaona.
 
Viongozi wa TAJA ni wakina nani? Wanataaluma gani? na wafanyakazi vyombo vipi vya habari?

Isije ikawa ni chama cha waandishi wa habari makanjanja Tanzania

Asha
 
Nadhani inachekesha,,, pale wanapomtaja, Manji, Basalehe na Malima, wanasahau Edward Lowassa, Andrew Chenge, Basil Mramba, Daudi Ballali, wote hao ni waislamu? Aibu tupu mheshimiwa Hamza KOndo kama kweli ni wewe, ila jamani huu naona ni Mkenge wa kuiondoa JF katika hoja za msingi.... Kondo kama unataka demu karibu
 
Na hilo ndilo ninalolitaka kujua. I have a big doubt over these allegations. Hawa wanatumiwa? Na nani? Maswala yepi ya kitaifa wamekuwa kifua mbele kutetea? Nadhani TAJA kwa uandishi wa namna hii mmejichanganya! Pamoja na kuwa Mengi si Hero kwangu bado mmenifanya niamini huyu bwana mnamwandama kwa kutumiwa. Kwa kutumia taaluma zenu za kiuandishi angalia tuhuma zilivyo na mfikirie kwanini abebe Mengi! Mnampa "shavu" bure...
 
Asha Napenda Kukutaarifu Kwamba Baraza La Habari La Waisilamu Nalo Limepewa Onyo Kali Na Msajili Wa Vyama Vya Siasa Pamoja Na Katibu Wa Ccm Taifa Kuhusu Matamshi Yao Ya Juzi .

Pia Waisilamu Hawalitambui Baraza Hilo Pamoja Na Viongozi Wake
 
Nadhani inachekesha,,, pale wanapomtaja, Manji, Basalehe na Malima, wanasahau Edward Lowassa, Andrew Chenge, Basil Mramba, Daudi Ballali, wote hao ni waislamu? Aibu tupu mheshimiwa Hamza KOndo kama kweli ni wewe, ila jamani huu naona ni Mkenge wa kuiondoa JF katika hoja za msingi.... Kondo kama unataka demu karibu

HE TINA MJUKUU WANGU BADO HUJAPATA TU

KWELI KAZI UPO PAMOJA NA MAOMBI YOTE BADO WANAZUNGUKA MBUYU TU
 
Kweli ipo kazi.... nadhani mambo mengine yanahitaji "Ushauri wa daktari"
 
Naona Siku Hizi Imekuwa Dili Kila Mtu Akitaka Kuwa Maarufu Basi Anakaa Pale Mbele Anataja Mabaya Ya Ccm Na Viongozi Wake Kama Hao Baraza Wakiendelea Na Mtindo Huu Wa Uchonganishi Sidhani Kama Wanafika Hata Mwezi Mmoja Toka Jana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom