bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,697
- 4,107
Nimesoma kwa umakini sana post yako mshana jr, ila kuna jambo pia naomba niulize na najua litakuwa nje ya maada kuhusu israel ningependa niulize humu.Israel ndio inajulikana kama taifa teule la Mungu na kuna ushahidi mwingi mitandaoni kuwa dunia ilianzia mashariki ya kati....
Mengi yanayoandikwa kuhusu hizi dini mbili zinazomtambua Mungu mmoja... Yana asili na mashariki ya kati... Mitume manabii masinagogi, historia na kumbukumbu nyingi za ulimwengu wa imani na kwa sehemu historia chimbuko lake ni mashariki ya kati....
Rejea mada ya Je dunia ilianzia mashariki ya kati? ... Kuanzia maisha ya Eden mpaka gharika ya Nuhu na kuangamizwa kwa sodoma na gomora... Haya yote hayatoki nje ya hapo
Unapoendelea kusoma historia ya dunia kiimani na vitabu vya dini.. Kuna kaliba inapewa nafasi ya 'wa mataifa'.... Yaani kwa tafsiri rahisi wale wa nje ya mashariki ya kati...! Nje ya Israel!
Tuna hizi dini tulizoletewa Afrika na wazungu na waarabu.. Uislam bado una asili na mashariki ya kati... Ukristo ulifikaje ulaya kwa wageni wa dunia (wazungu)? Kisha pengine wakauchakachua kishapo ndio wakatuletea sisi? Hili hojaji linahitaji mjadala wake tofauti?
Lakini kwa sasa kuna maswali yanahitaji majibu ili kujiridhisha na hizi imani zetu
. Je wale wote walio nje ya mashariki ya kati ndio wa mataifa?
. Je kwanini kwenye Biblia takatifu China inatajwa kipekee? Katika kitabu cha mithali kwenye kutafuta maarifa watu wanaaswa wafike hata China?
. Je mpango mkakati wa Injili kwa watu wote (wa mataifa) ya kuwahubiria neno la Mungu watubu na kuokoka... Tafsiri yake ni ipi? Je hawa hawakuwa sehemu ya uumbaji wake?
. Je wapagani wanaohitaji kuhubiriwa injili.. Si wakazi wa dunia hii?
Historia ya Israel...
Nguvu waliyo nayo utabiri wa kurejea nyumbani... Namna yao ya kuabudu nakuamini tofauti na imani nyingine ni kama vile inatoa picha kuwa hata wazungu ni watu wa mataifa na si sehemu ya taifa teule! ?
Kule instagram kuna page ya state of israel naifollow Israel (@stateofisrael) • Instagram photos and videos
iko verified na ig ila nilichoshangaa sana ni kuwa wanapromote sana ushoga, kiasi kuwa baadhi ya followers wake toka nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakihoji kuhusu kitendo cha taifa teule kama israel kupromote ushoga kiasi hicho tena kwa kuandika SHABBAT SHALOM
Sasa kama taifa teule linafanya hivyo, ni wapi tunaelekea, ni kwanini wanafanya hivyo ili hali nchi mbalimbali za kikristo zinaliheshimu sana taifa hilo kuwa ni taifa teule la Mungu.