Taifa teule na mataifa

Israel ndio inajulikana kama taifa teule la Mungu na kuna ushahidi mwingi mitandaoni kuwa dunia ilianzia mashariki ya kati....

Mengi yanayoandikwa kuhusu hizi dini mbili zinazomtambua Mungu mmoja... Yana asili na mashariki ya kati... Mitume manabii masinagogi, historia na kumbukumbu nyingi za ulimwengu wa imani na kwa sehemu historia chimbuko lake ni mashariki ya kati....

Rejea mada ya Je dunia ilianzia mashariki ya kati? ... Kuanzia maisha ya Eden mpaka gharika ya Nuhu na kuangamizwa kwa sodoma na gomora... Haya yote hayatoki nje ya hapo

Unapoendelea kusoma historia ya dunia kiimani na vitabu vya dini.. Kuna kaliba inapewa nafasi ya 'wa mataifa'.... Yaani kwa tafsiri rahisi wale wa nje ya mashariki ya kati...! Nje ya Israel!

Tuna hizi dini tulizoletewa Afrika na wazungu na waarabu.. Uislam bado una asili na mashariki ya kati... Ukristo ulifikaje ulaya kwa wageni wa dunia (wazungu)? Kisha pengine wakauchakachua kishapo ndio wakatuletea sisi? Hili hojaji linahitaji mjadala wake tofauti?

Lakini kwa sasa kuna maswali yanahitaji majibu ili kujiridhisha na hizi imani zetu

. Je wale wote walio nje ya mashariki ya kati ndio wa mataifa?

. Je kwanini kwenye Biblia takatifu China inatajwa kipekee? Katika kitabu cha mithali kwenye kutafuta maarifa watu wanaaswa wafike hata China?

. Je mpango mkakati wa Injili kwa watu wote (wa mataifa) ya kuwahubiria neno la Mungu watubu na kuokoka... Tafsiri yake ni ipi? Je hawa hawakuwa sehemu ya uumbaji wake?

. Je wapagani wanaohitaji kuhubiriwa injili.. Si wakazi wa dunia hii?
Historia ya Israel...

Nguvu waliyo nayo utabiri wa kurejea nyumbani... Namna yao ya kuabudu nakuamini tofauti na imani nyingine ni kama vile inatoa picha kuwa hata wazungu ni watu wa mataifa na si sehemu ya taifa teule! ?
Nimesoma kwa umakini sana post yako mshana jr, ila kuna jambo pia naomba niulize na najua litakuwa nje ya maada kuhusu israel ningependa niulize humu.

Kule instagram kuna page ya state of israel naifollow Israel (@stateofisrael) • Instagram photos and videos

iko verified na ig ila nilichoshangaa sana ni kuwa wanapromote sana ushoga, kiasi kuwa baadhi ya followers wake toka nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakihoji kuhusu kitendo cha taifa teule kama israel kupromote ushoga kiasi hicho tena kwa kuandika SHABBAT SHALOM

Sasa kama taifa teule linafanya hivyo, ni wapi tunaelekea, ni kwanini wanafanya hivyo ili hali nchi mbalimbali za kikristo zinaliheshimu sana taifa hilo kuwa ni taifa teule la Mungu.
 
30 Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;

31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.

32 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.

33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
 
Ilikuwaje miungu ya Tanzania ishindwe na Mungu wa israel? Si tungetambika kupitia miungu yetu na kupata uwezo wa kuitwala dunia na miungu yetu ikaabudiwa na wanadamu wengine wote duniani. Hilo tu la Bismack ungetakiwa ujiulize nani kalaani miungu yetu na sisi wenyewe. Nimependa huu mchango wako wa vikoba...imependeza.

inawezekana waisrael wangemkubali Kristo dunia au watu wa mataifa wasingemjua kwa nafasi aliyo nayo.
dini kwa ujumla wake kwa kadri ya mapokeo ina mambo mengi kwa kadri ya anayetupokelesha kwa kuwa huwa pia inaweza kubeba maslahi binafsi kwa wapokeaji.
lakini ninachojifunza kwa watu hawa ni mambo makubwa mawili.
  1. utuzaji wao wa taarifa- inawezekana hakuna taifa litunzalo taarifa kwa umakini kama hawa jamaa kwa kadri ya vizazi vyao toka ibrahimu mpaka sasa na wamefanikiwa kuyaweka kwenye maandishi yakisomwa dunia nzima. pamoja maandishi yalizinduliwa misri ambako hawa jamaa walikuwa watumwa, lakini walitumia fursa vizuri kuzidi wa misri wenyewe.
  2. kiingine shida na kutumikishwa kwa muda mrefu na wamisri (kama tunavyoona baadhi ya kazi zao za ujenzi) zimewafanya kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na mazingira wakitumia resource chache kuleta mafanikio makubwa. iko mifano mingi lakini wengi tunajua taifa hili lilivyo na mvua chache lakini linaongoza kwa kilimo cha matunda na mbogamboga wakitumia zaidi kwa uangalifu mvua chache zinazonyesha ka kukinga maji na sehemu zingine za milima zinatumika kama matenki ya kuhifadhia maji na kushuka bondeni(kwa kadri ya simulizi).
naogopa sana kuwachambua kwa kuwa wanahusika na imani nilionayo na muda si mrefu nimetoka kwenye jumuiya na somo la leo limetoka 2timotheo 4:1-8 nikitutaka tuwaubirie watu wa mataifa injili.
hivyo kwangu mimi cha kujifunza ni kwamba:-
  1. katika shida zetu na masumbufu yetu tujitahidi kutafuta njia ya kuyatatua kwa urahisi na kwa akili zote. ( mfano mzuri VICOBA ilianzia niger baada ya shida za kinamama kutelekezwa na waume zao kwa ulevi na pengine na umalaya kulisababisha wao kuanzisha vikundi hivi, lakini leo wazungu walishavichukua vikawa vyao na jina la kibantu la vikundi hivi likapotezwa na sasa ni wao na hawakumbuki hata kuwalipa haki miliki kwa waanzishaji.)
  2. tujifunze kutunza kumbukumbu zetu vizuri ili siku zijazo tuweze kuzielezea vizuri haiingii akilini eti ziwa victoria pamoja na mlima wake wa bismarock eti ulivumbuliwa na mzungu waswahili walikuwa hawauoni?
  3. tutumie muda na maarifa kutambulisha kile tulichonacho na tulichofanya badala ya muda mwingi kuzungumzia udhaifu mfano hakuna ubishi mpaka sasa binadamu wa kwanza aliishi tanzania hvyo tungeweza kusema taifa la tanania ni taifa teule na wale wengine ni watu wa mataifa.
yapo mengi na inawezekana nimetoka nje ya mada lakini nimeona mchango huu waweza faa kwa kadri nilivyoona leo yafaa kuchangia.
 
Mkuu Zitto Junior, naomba nikurekebishe mahali

Ahadi za Mungu kwa wana wa Israeli hazifutiki kamwe mpaka mwisho wa dahari, hilo ni agano la MUNGU na Ibrahimu hili ni agano la milele na milele

YEREMIA - SURA YA 31
1 Wakati huo, asema Bwana, nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu.
2 Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha.
3 Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.

Kuhusu Waisraeli kuwakataa mitume na Manabii mtume Paulo alishasema sababu na chanzo chao

25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. (isaya 27:9) kuijua hiyo ahadi
28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
soma warumi 11 sura nzima

Kwa maelezo zaidi juu ya hawa watu

soma Isaya na Yeremia
Nashukuru mkuu kwa kunirekebisha hapo kwa mistari iliyoshiba kabisa ila mimi hoja yangu sio kupinga kuwa Israel haina ahadi za Abraham ila nachosema ni kuwa ule UTEULE sio wa kwao tu tena kama hapo zamani ila sasa UTEULE umekuwa kwa wote wanaomcha Mungu ikimaanisha waisrael wamekuwa sawa na mataifa mengine yote as long as yakimfuata Mungu wa kweli

Wagalatia 3
6
Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa
.

..........

29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Je hapa Biblia haikumaanisha Uteule wote wa Abraham na baraka zake zimeshakwenda kwa mataifa yote ambayo yatamkubali kristo ikiwemo Tanzania na mataifa mengineyo??? Hivyo kama wote tumerithi hizo baraka uteule wa israel si umekomea hapo au labda niseme uteule wa israel umeongezwa wafuasi hivyo nikimaanisha waliomfuata MUNGU wa kweli wote wamehakuwa sehemu ya taifa teule hivyo hakuna special tena kuhusu ISRAEL

Labda unieleweshe vzuri maana nakiri bado najifunza kuhusiana na maandiko

Cc tikakami wa lopelope
 
Ila pia kuna sehemu Yesu alikuwa anaombwa na mama fulani amponye binti yake na Yesu kwakujua siyo myahudi alikuwa anampotezea mpaka wanafunzi wake wakamwambia mtimizie haja yake huyu mama ila yeye akajibu kuwa HUWEZI KUMPA MBWA CHAKULA CHA WATOTO naye mama hakajibu kuwa hata mbwa wanakula makombo ya bwana zao chini ya meza, naye kwakuona imani ya yule mama akamtimizia haja zake za kumponya binti yake kwakusema sijapata ona mtu mwenye imani kama wewe

hapo unaona kuwa anasema ametuma kwa taifa la wayahudi sio kwawote ingawa pia kuna mifano mingine ile ya harusi na waalikwa kukusanywa katika njia panda inakuwa contradicted na maneno aliyosema hapo juu, hapo ndio unaona biblia ni msitu mnene
 
Nabii Issa ni Mtume wa Mungu alyezaliwa na Maryam Bint Imran ..Nabii Issa hakuzaliwa hana Baba na huu ndo Muujiza mkubwa juu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu..Nabii Issa alikuja na ujumbe wa kumuabudu Mungu aliye mmoja , kusali na kutoa zaka pamoja na kufanya yaliyo mema hakuuliwa wala hakusulubiwa kwa mujibu wa imani yangu ya Uislam.

Naomba nieleweshe juu ya Yesu.
Yesu alisema "yeye ni njia ya kweli na uzima" yesu alibatizwa vipi issa nae alipatizwa? Yesu alisulubiwa msalabani na kufa siku ya tatu alifufuka. Yesu alizaliwa kwenye hori la ng'ombe Issa alizaliwa chini ya mtende!! Kwakifupi Issa siyo Yesu. "Kweli itakuweka huru".
 
Naomba nieleweshe Yesu alizaliwa vp na mama yake ni nani
 
Biblia ni historia ya waisrael na Mungu wao. kila sehemu wana mungu wao na jinsi ya kumwabudu. issue inakuja jee Mungu ni mmoja wa wakristo,waislam, africa...
 
Alikufa au hakufa? Na kama alikufa alifufuka au hakufufuka. Kama hakufufuka yuko wapi? Maana wafu wako kaburini wakisubiria ile siku ya mwisho wa dunia yaani siku ya hukumu. Kiranja wa hiyo siku ni Bwana Yesu mwenyewe.

Bwana Yesu aliteswa, alisulubiwa, akafa, akazikwa na siku ya tatu akafufuka. Ameshinda kifo na dhambi, hatimaye akapaa akishudiwa na watu kwenda mbinguni.

Hakufa na wala hakusulubiwa...Mwenyezi Mungu alimpaisha na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu...jambo unaloliona wewe ni gumu na haliingii akilini basi kwake ni kitu chepesi mno.
 
Mkuu zitto jr asante ni mara ya pili una ni mention. Hili suala nita hitaji muda kulifuatia ilinije na mistari ya Biblia kusurpport hayo nitakayo ya leta hapa. Mistari mingine tayari imo humu kwenye hii thread. Ila agano la Mungu na Abraham na mjukuu wake Jacob/Israel lita simama milele. Ni kiamini kwa msaada wa Mungu tunaendelea kukomaa katika hii mijadala ya kiimani humu jF.

Nashukuru mkuu kwa kunirekebisha hapo kwa mistari iliyoshiba kabisa ila mimi hoja yangu sio kupinga kuwa Israel haina ahadi za Abraham ila nachosema ni kuwa ule UTEULE sio wa kwao tu tena kama hapo zamani ila sasa UTEULE umekuwa kwa wote wanaomcha Mungu ikimaanisha waisrael wamekuwa sawa na mataifa mengine yote as long as yakimfuata Mungu wa kweli

Wagalatia 3
6
Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa
.

..........

29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Je hapa Biblia haikumaanisha Uteule wote wa Abraham na baraka zake zimeshakwenda kwa mataifa yote ambayo yatamkubali kristo ikiwemo Tanzania na mataifa mengineyo??? Hivyo kama wote tumerithi hizo baraka uteule wa israel si umekomea hapo au labda niseme uteule wa israel umeongezwa wafuasi hivyo nikimaanisha waliomfuata MUNGU wa kweli wote wamehakuwa sehemu ya taifa teule hivyo hakuna special tena kuhusu ISRAEL

Labda unieleweshe vzuri maana nakiri bado najifunza kuhusiana na maandiko

Cc tikakami wa lopelope
 
Hakufa na wala hakusulubiwa...Mwenyezi Mungu alimpaisha na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu...jambo unaloliona wewe ni gumu na haliingii akilini basi kwake ni kitu chepesi mno.

Unaona sasa siku zote na jua kuwa Makka au Madina kuna kaburi la Mtume SAW. Naomba basi nielezee siku zake za mwisho hapa duniani zilivyo kuwa na mashuhuda walio zishudia pengine na kwa faida ya wengine humu.

Siku ya hukumu ya mwisho yeye atakuwa wapi? Maana kwa mujibu wa Biblia siku ya hukumu ni shurti kila goti la mwanadamu lipigwe mbele yake kwa ajili ya hukumu ya haki. Sasa sitaki kuamini kuwa Mtume Muhamed SAW si mwanadamu aliye umbwa Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote (Bwana Yesu).
 
Ukiangalia kwa undani zaidi haya masuala utagundua kuna watu wametuzidi kete sisi weusi kwenye kuandika haya mambo maana kitaalamu its the one with pen who control the story.

Waliopata fursa ya kuandika juu ya haya mambo wamewamba sana hii ngoma kuvutia kwao.

Ila when you check it in your sense unagundua hata Dunia ilivyo watu walioanza walikuwa weusi then watu weupe wakapatikana kutokana na environment factors... Wazungu wamekuwa wazungu kwa kukaa sehemu yenye baridi sana. But probably walikuwa weusi mwanzoni then kutokana na kusafiri zaidi na kufika Europe wakajikuta wako weak in melanin and hair.

Ndio maana watu wa afrika wana nywele ngumu na ngozi ngumu ili kuzuia jua kuwadhuru. Thus maisha yalianzia afrika then watu walipotawanyika wakaadapt kulingana na environmental reasons.

Kuna mengi sana hatuyajui kwenye hii Dunia. Sema waliopata nafasi ya kuandika ndio wametu control kwa maandishi yao.
Vp zile pua za kizungu na wahindi?
 
Mkuu nakuunga mkono but Issa siyo yesu jaribu kuelewa.
Mkuu hata mimi nakuunga mkono yesu sio Issa bin Maryam kwa kuwa yesu alisulubiwa na Issa A.S hakusulubiwa na pia inawezekana yesu alikuja na kitabu cha biblia lakini Issa alikuja na kitabu cha Injili you are correct
 
Nimesoma kwa umakini sana post yako mshana jr, ila kuna jambo pia naomba niulize na najua litakuwa nje ya maada kuhusu israel ningependa niulize humu.

Kule instagram kuna page ya state of israel naifollow Israel (@stateofisrael) • Instagram photos and videos

iko verified na ig ila nilichoshangaa sana ni kuwa wanapromote sana ushoga, kiasi kuwa baadhi ya followers wake toka nchi mbalimbali duniani wamekuwa wakihoji kuhusu kitendo cha taifa teule kama israel kupromote ushoga kiasi hicho tena kwa kuandika SHABBAT SHALOM

Sasa kama taifa teule linafanya hivyo, ni wapi tunaelekea, ni kwanini wanafanya hivyo ili hali nchi mbalimbali za kikristo zinaliheshimu sana taifa hilo kuwa ni taifa teule la Mungu.
Kuna mambo mengi yanachanganya sana kuhusu Israel
Mema na mabaya
Mazuri na ya kutisha
Ya msaada na ya ukatili
Ya akili nyingi na ya ujinga pia
 
28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.

Bibilia haijasaza kitu
hii kitu hujaweka vizuri mstari wake nimeipenda hii
 
hi
Ikuwaje miungu ya Tanzania ishindwe na Mungu wa israel? Si tungetambika kupitia miungu yetu na kupata uwezo wa kuitwala dunia na miungu yetu ikaabudiwa na wanadamu wengine wote duniani. Hilo tu la Bismack ungetakiwa ujiulize nani kalaani miungu yetu na sisi wenyewe. Nimependa huu mchango wako wa vikoba...imependeza.
hilo jina tanzania tu ni la miungu ya kigeni sina uhakika na tanzania ni muhindi mmoja ndo alishinda hilo shindano la kutafuta jina.
hivyo mwisho wa siku tuendelee kukubali MUNGU wao wanayemtegemea wayahudi ni wakweli nasi tumekubali kumpokea na kufuata kwa kuwa ziko shuhuda mbalimbali kwao na mifano iko mingi daniel 6:16, 2wafalme6:18 na nyingine nyingi.
ila hii haiondoi uhalali wa kutetea yaliyo mazuri yetu ikiwa ni pamoja na historia zetu.
 
Back
Top Bottom