Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,921
Kibri cha Marekani na Uiengereza kuyaona mataifa mengine duniani hasa mashariki ya kati yanakaliwa na watu wajinga kinazidi kupata vikwazo katika awamu hizi.
Juhudi za kuwashawishi viongozi wa mataifa hayo ya mashariki ya kati kuwapokea wapalestina wa Gaza zilikwama mapema sana.Juhudi hizo ziliambatana na hongo kwa Misri lakini wote kwa pamoja
wakagoma.Mataifa hayo yakaamua wawaachie Israel wenyewe wapambane na Hmas mpaka kieleweke.
Wanamgambo wa Houth nao wamekuwa mwiba kwa mataifa hayo kutokana na wanamgambo hao kuvuruga safari za meli zinazoelekea Israel kupitia mlango wa Suez.
Msimamo wa Houth na vitendo vyao vimeonesha kuwa na athari sana katika kuangusha uchumi na mtindo wa maisha wa waisrael.Jambo hilo limewatia hasira washirika wakubwa wa Israel ambao ni Marekani na Uiengereza.
Hata pamoja na hasira na nia za kuisaidia Israel iliyobanwa na Hamas na Hizbollah lakini bado mataifa hayo daima hayapendi kuingia vitani peke yao.Hupendelea sana kukokota mataifa mengine ili yawe pamoja nao,
Viongozi mbali mbali wa Marekani wamekuwa wakifanya ziara zisizosita mashariki ya kati ili kutafuta uungwaji mkono wa mikakati yake ya kivita na kuipa muda Israel kupiga wapalestina.
Ziara ya mwisho ya Blinken ilianza na Uturuki halafu akaelekea Qattar,Saudi Arabia, UAE na Misri.
Katika mazungumzo yake ilikuwa ni kuwashawishi wajiunge na muungano wa kuilinda bahari ya Red Sea Ili kuwazuia Houth wasizipige meli za Israel.Ombi hilo kama yale ya mwanzo ya kuwahamisha wapalestina nalo lilikataliwa na viongozi wa mataifa hayo.
Kwa vile nia ya kuipiga Houth ilikuwepo zamani,hata baada ya kukataliwa ushirikiano Marekani ikashirikiana na Uiengereza kupiga maeneo kadhaa ya Yemen.Siku moja baada ya mashambulio ya mwanzo Marekani ikazidi kujikashifu nia zake mbaya kwa kufanya mashambulia mara ya pili peke yake bila kuishirikisha Uiengereza.