Taifa Stars kuonywesha duniani kote

Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
9,413
6,452
Kuna taarifa za uhakika kuwa Taifa Stars itaonyeshwa duniani kote hapo kesho katika mechi yake dhidi ya Misri.

Kwa walio nje ya Tanzania, Stars wataonyeshwa kupitia channel ya BeIn Sports both Spanish and English services. Check your local cable services.

Kwa wachezaji wetu, tafadhali acheni uchawi na ushamba kwani huu ndiyo muda wenu kujitangaza kimataifa.

Na kwa sie tunaopanga kwenda kuiona Stars hapo kesho, tafadhali tusilete mifuko ya rambo iliyojaa vinyesi ama chupa za maji zenye mikojo.

Ahsanteni!
 
Una muda gani huendi taifa mkuu?
 
Inaweza kuonyeshwa duniani kote lakini bado mtanzania asiione maana asilimia kubwa ya wabongo wanategemea local channels....nilidhani kuna channel ya bongo itaonyesha, azam vp itaonyesha?
 
Bein sport lazima waonyeshe kwa sababu wao wanahaki ya kuonyesha matangazo afrika ya kaskazini kwahiyo Egypt Ndio sababu ya kuonyesha mechi hiyo,
Na mtangazaji atakuwa akiitakia Egypt tu ushindi hutamsikia akisifia Tz

Ndugu yangu acha ubaguzi na ndio maana timu yetu haisongi mbele..bein sport kitu kingine na wala haibagui ksma unavyodhani, hayo ni maneno yako tu
 
Ubaguzi uko Wapi hapo? Bein sport kwanini haionyeshi mechi za Taifa star ila mpaka icheze na timu za afrika ya kaskazini? Kwa sababu ina mikataba ya kuonyesha timu za mataifa yote ambayo inarusha matangazo yake, na lazima studio yao siku ya mechi atakuwepo mtangazaji kutoka nchi husika, subiri mechi ya Taifa star kesho studio atakuwepo mtangazaji toka Egypt, ungekuwa unasikia lugha wala usingeleta ligi hapa
 
TBC jamani msituchinjie baharini! naandika kwa uchungu mpaka nataka kulia........
LIVE ni marufuku TBC... ila kama una harusi ni ruksa kuoneshwa live hiyo ni TV ya biashara utawala huu... MAmbo ya Taifa yanaleta hasara tu lipeni kodi alla
 
Ubaguzi uko Wapi hapo? Bein sport kwanini haionyeshi mechi za Taifa star ila mpaka icheze na timu za afrika ya kaskazini? Kwa sababu ina mikataba ya kuonyesha timu za mataifa yote ambayo inarusha matangazo yake, na lazima studio yao siku ya mechi atakuwepo mtangazaji kutoka nchi husika, subiri mechi ya Taifa star kesho studio atakuwepo mtangazaji toka Egypt, ungekuwa unasikia lugha wala usingeleta ligi hapa

Hakuna anaeleta ligi hapa sote tunaelimishana! Kwaiyo Sasa wewe unataka taifa stars na yenyewe ionyeshwe? Mi naona Bora hata wasiionyeshe mpaka pale kiwango chao kitakapokua juu like Algeria,ivory cost,Tunis nk hapo sawa! Ni hivyo mkuu
 
Hapana mechi itaoneshwa Bein sport chanel 1 tu ambayo ni kiarabu na sio duniani. Lazima ujuwe Egypt ni part ya MENA na beinsport wana customers wengi sana kwa hiyo mechi hasa inalengwa wa Misri waione.
 
Ndugu yangu acha ubaguzi na ndio maana timu yetu haisongi mbele..bein sport kitu kingine na wala haibagui ksma unavyodhani, hayo ni maneno yako tu
Ndugu yangu huo ndio ukweli lazima wataipa support Egypt sasa unadhani Tanzania acheze mechi yoyote hapo Bein watakuja? Kwa lipi?. Ni normal mtangazaji kupendelea kwao kama vile mtangazaji wa Tz atapendelea Tz. No wazungu tu peke yao hata kama wanapendelea lakini wana weledi mkubwa hawaoneshi wazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom