Taifa la kidemokrasia linapaswa kuepuka kwa nguvu zote desturi na mila ya mauaji ya siri; hakuna maendeleo yakudumu kwenye damu inayolia

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Nimejaribu kutafakari ni kwanini wauaji wengi ukamatwa kirahisi baada Tu yakufanya mauaji ila waalifu wengine uchukua muda?

Nimetafakari ni kwanini watu wengi wanaweza kukaa kimya pale wanaposikia ndugu Yao kauwawa lakini NI vigumu kusamehe likaisha?

Nimejiuliza kwanini MTU maarufu akiuwawa let say na dola maswali yakianza wauaji ufika msibani kutoa pole wakihubiri mwachieni Mungu?

Nimejiuliza ikiwa unajua walioua na ukakaa nalo moyoni na wao wakajua kabisa unajua kwamba wameua haipo siku wewe utataka kuwauwa walioua kwa kuogopa wasikuue au wewe ukauwawa na walioua wakihofia utatoa Siri?

Nimejiuliza aliyeua ana nafasi moyoni mwake yakupata Amani? Kama Hana Amani tunawezaje kumdhibiti asiendelee kuua?

Je, lini tutafunga mjadala WA mauaji ya Siri? Familia ngapi zitakuwa zimeathirika? Kati hao wanafamillia walioathirika wangapi watajaa chuki nakupanga malipizi? Je yakija malipizi wewe au familia yako itakuwa salama?

Ukitafakari haya Ndipo unapogundua uchumi uliojengwa njia ya mauaji ya Siri NI endelevu lakini uchumi uliojengwa kwenye mauaji ya Siri utegemea na muuaji anataka nini.

Demokrasia si kupiga Kura Kwa maana ya kuchagua na kuchaguliwa , demokrasia nikuruhusu hukumu ya wazi na haki Kwa wakosaji. Ukikosa Haki na uwazi ipo SIKU utaporomoka . Huu ndio uchumi. Uchumi endelevu NI Demokrasia

Tanzania tumeua uchumi na maendeleo kwa Sababu tumekosa majibu kuhusu wote waliohusika na mauaji ya uchumi. Kama ujaua uchumi basi unamjua aliyeua uchumi na unajiuliza ukimuuliza kwanini ameua uchumi upo uwezekano akakumaliza wakati huo aliyeua uchumi anajiuliza unaweza kumfichia Siri ya dhambi aliyotenda au akutangulize ili abaki huru?

Tuepuke sana dhana ya mauaji ya siri, yanawafanya waasi kujitaftia confot wanapotaka kutenda mabaya dhidi ya wale wanaodhani ni wabaya. Tumeletwa duniani kustarehe, siyo kutafuta umaarufu na nguvu ya kuondoa nguvu ya uchumi (starehe) za wengine.
 
Back
Top Bottom