Taifa kwanza: Rais na mawaziri 2015

- Mheshimiwa Sitta, anafaa kuwa Rais wa Jamhuri: msomi, haogopi kusimamia ukweli, anaheshimu sheria, ni mtendaji na mfuatiliaji na ni mkali sana.

Willie @ NYC, USA.
 
Sikujua kama hii nayo ni sifa muhimu kuwa Waziri Mkuu.
mkuu sio matakwa yetu kinchi, ni matakwa ya viranja wa Dunia kuhakikisha wakinamama wanapewa nafasi hata kama za kulazimishia kama viti maalumu
 
Mkuu@ NYC, USA, achana naye huyo. Anayefaa kuwa Rais ni John Jumanne Cigwiyemis Malecela. Hakuna mwingine

sio mbaya sana pia ni mawazo, ila huyu ungemtaja kwenye thread iliyoanzishwa na mtu mwingine, hapa inaweza ikaonekana ni kejeli km mimi ninavyohisi.
 
- Mheshimiwa Sitta, anafaa kuwa Rais wa Jamhuri: msomi, haogopi kusimamia ukweli, anaheshimu sheria, ni mtendaji na mfuatiliaji na ni mkali sana.

Willie @ NYC, USA.
Mkuu hapo tupo pamoja, ameonyesha angalau anuwezo wa kufanya ingawaje amebanwa na mfumo wa CCM.
Lakini vipi kama CDM ikishinda unadhani ni akina nani watatufaa kushikilia usukani wa uongozi toka CDM?
 
Kwani lazima kila issue ya urais lazima awemo huyu?
I can't be used to fight W. Malecela's battles in CCM. You might have noted that he has no Tanzanians' agenda at heart but CCM's. Anajua members wengi watamponda EL na yeye kupata nafasi ya kupendekeza ampendaye (tayari ameshapendekeza Mwakyembe).

Huwezi kumchukia EL bila kuichukia CCM maana anayofanya EL siyo mageni CCM na ndio maana EL alipokuwa anaongea bungeni, wabunge wote wa CCM(hata 6) walishangilia. Chenge anasafishwa, wabunge wa CCM wanashangilia. Wapenda mabadiliko wanavyopendekeza Dr. Slaa, anaponda kishabiki wakati hana ujasiri ya kuwaponda viongozi wa chama chake wanaolea rushwa na ufisadi nchini. EL anawafaa CCM maana anafanana nao na ni bora kuliko wengine wanafiki.
 
- Mheshimiwa Sitta, anafaa kuwa Rais wa Jamhuri: msomi, haogopi kusimamia ukweli, anaheshimu sheria, ni mtendaji na mfuatiliaji na ni mkali sana.

Willie @ NYC, USA.

mkuu nafikiri inabidi usimame na mmoja tu, mimi sijabadilisha, nimeshasema Dr.Slaa anafaa, kwa hiyo umeshindwa kuwashawishi watu kuhusu Dr.Mwakyembe au imekuaje? embu nipe sifa za mzee tarakimu kumlinganisha na Dr.Slaa.
 
Mkuu mwakyembe anaweza kua mzuri sana tena sana lakini ninamashaka kama ataweza kutumia uwezo wake wote kusimamia malengo na maslai ya taifa kwani yuko kwenye mfumo ambao hautamruhusu kufanya hivyo mfano mzuri nikushindwa kusimamia mapendekezo ya kamati yake ikiwa nipamoja nakutoweza kuwawajibisha wahusika wakuu kama hosea n.k. Licha yakwamba umesisistiza taifa kwanza chama badae ila hatuwezi kujadili mtu anaefaa pasipo kujua anatoka chama gani kwani katiba hairuhusu mgombea binafsi na kwamantiki hiyo tunapaswa kuangalia mtu na chama anachotoka je kitamruhusu kutekeleza maslai ya wananchi hata kama hayaendani na maazimio ya chama chake? Kwaupande wangu naona Dr Slaa anafaa kwani nimsomi, anauchungu na taifa lake anapenda haki na mfumo wa sheria tena zaidi ya mwakyembe ndio maana kapigania uundwaji wa katiba mpya na mwisho yuko kwenye chama kinacho mruhusu kutekeleza matakwa ya wananchi tofauti na vyama vingine chadema ni chama kinachozingatia maslai ya taifa kwanza tena kwavitendo sina haja yakueleza hili kwa undani naamini unaelewa isitoshe kuliko mimi.
Hoja za usomi hazina nafasi katika hili mkuu, huo usomi wake ni wa imani yake
 
- Mwalimu the greatest alitusaidia kutufanya huru, lakini the rest ni debatable, naomba unishawishi zaidi kwamba Dr. Slaa anafaa kuwa Rais wa kulisaidia hili taifa zaidi ya wengine, kwa mfano unasema ndiye aliyetufunua kuhusu mafisadi ambao mpaka leo hakuna aliyefikishwa kwenye sheria, Dr. Slaa anao ushahidi wa kutosha kwa nini asiwapeleke kwenye sheria kwa jina la wananchi? I mean Mch. Mtikila siamini kwamba ana uwezo wa kuwa Rais, lakini kwenye hili la kwenda kwenye sheria na ushahidi anaonekana kuwa na ubavu zaidi,

- Sasa je tutaendelezwa na Rais asiyesimama kuona sheria inatendeka?

Willie @ NYC, USA.

Kijana wa Cigwiyemisi, Unaziamini mahakama za Tanzania kwa kiwango ambacho Slaa anaweza kufungua kesi hizo na akashinda? Kama unaziamini hizi mahakama za huku kwa kiwango hicho nakusihi kwa unyenyekevu wote, fanya upya homework yako. Huyo Mtikila si unaona kesi zake zinavyochezewa mchezo mchafu? Ile kesi ya mgombea binafsi si umeona ilikoishia? Usijifanye huyajui magamba bana
 
mkuu sio matakwa yetu kinchi, ni matakwa ya viranja wa Dunia kuhakikisha wakinamama wanapewa nafasi hata kama za kulazimishia kama viti maalumu
Hadi kwenye uwaziri Mkuu? Mnataka kutufanya wenda wazimu sasa. Kwani nani alisema Makinda apewe Uspika kwa sasa ni Mwanamke? Ni hao viranja wa dunia? Au nini tulipewa na hao viranja wa dunia baada ya kumuweka Makinda?
 
- Well, kwanza ninaamini kwamba huenda by 2015 tukawa na wagombea binafsi, lakini pia ninasema hivi Mwakyembe ameshaonyesha kwamba ana uthubutu wa kuweza kusimama kidete kwenye mazingira tuliyonayo sasa, meaning kwamba akipewa nafasi ya Urais au Waziri Mkuu, kwa kweli tutasonga mbele kidogo, mchango wako mzito sana mkuu Agreed 100%!

Mkuu ikumbukwe kwamba mwaka 2005 jk alijigamba kama mpinga ufisadi akisifiwa kwakuto chukua nyumba za serikali zilizo uzwa na zaidi alisema atahakikisha zinarudishwa alivyo ingia chama kikamweleza huo sio utaratibu kampeni zimekwisha rudi kwanye misingi ya chama, sasa tunashuhudia hana makali tena kuweza kufanya kitu kwa mafisadi.

Hivyo hatuwezi kua na imani kwamba mwakyembe anaweza kupata nguvu yakuua mising ya chama na kufanya atakavyo akiweza kuhamia chama tofauti atafaa sana ikumbukwe pinda aliitwa mtoto wa mkulima aakaanza kwa kasi chama kikamwambia rudi kundini akasema kasha ya kagoda haigusiki.

Nadhani tutafute mtu sahihi aliye kwenye chama sahihi au awe mgombea binafsi kama tutafanikiwa kuunda katiba kwasasa nasisitiza hakuna zaidi ya Slaa.
 
Hadi kwenye uwaziri Mkuu? Mnataka kutufanya wenda wazimu sasa. Kwani nani alisema Makinda apewe Uspika kwa sasa ni Mwanamke? Ni hao viranja wa dunia? Au nini tulipewa na hao viranja wa dunia baada ya kumuweka Makinda?

na kwanini tuendelee kuwa na mawazo ya kitumwa? viranja wa dunia wamushushwa kutoka mbinguni kutawala mawazo yetu au?
 
I can't be used to fight W. Malecela's battles in CCM. You might have noted that he has no Tanzanians' agenda at heart but CCM's. Anajua members wengi watamponda EL na yeye kupata nafasi ya kupendekeza ampendaye (tayari ameshapendekeza Mwakyembe).

Huwezi kumchukia EL bila kuichukia CCM maana anayofanya EL siyo mageni CCM na ndio maana EL alipokuwa anaongea bungeni, wabunge wote wa CCM(hata 6) walishangilia. Chenge anasafishwa, wabunge wa CCM wanashangilia. Wapenda mabadiliko wanavyopendekeza Dr. Slaa, anaponda kishabiki wakati hana ujasiri ya kuwaponda viongozi wa chama chake wanaolea rushwa na ufisadi nchini. EL anawafaa CCM maana anafanana nao na ni bora kuliko wengine wanafiki.
Mkuu umenikosha sana, sichangii tena thread hii kwa heshima ya mchango wako huu. Ngoja niende kwenye maonesho ya Saba saba maana you have made my day.
 
dude are u serious ...?! wajuwa kuna watu hata wapige msuaki vipi kinywa kitaendelea kutoa harufu mbaya...! basi ndio lowasa katika ulingo wa siasa na swala zima la ufisadi
Ndugu Malecela anaona upinzani hakuna kichwa kinachofaa kuwa rais na ndo maana anasema japo anauthamini mchango wa Dr. Slaa kwa taifa, bado anaona hafai kuwa rais bali kiongozi wa upinzani! Sasa kama mtu wa kaliba ya Dr. Slaa hafai, maana yake ni kwamba EL anafaa. Huyu ndiye EL aliyekuwa anashangiliwa na wabunge wa CCM juzi. Hadi Samweli 6, anagonga meza kukiri kwamba anachosema ni kweli!

Kama EL ni mchafu, waliobaki CCM ni wasafi? Mbona hakuna mwanaCCM anayejitokeza kusema kwa uwazi kwamba EL, RA, AC hawafai na waachie nafasi zao serikalin na kwenye chama? Mbona hakuna mwanaCCM anayetaka kukiri kwamba serikali yake haina dhamira ya kweli ya kupambana na rushwa(kagoda, rada, n.k)? Malecela hatusaidii kupendekeza viongozi wazuri wajao, anataka tumsaidie kupambana na wabaya wake kwenye chama cha magamba!
 
Hadi kwenye uwaziri Mkuu? Mnataka kutufanya wenda wazimu sasa. Kwani nani alisema Makinda apewe Uspika kwa sasa ni Mwanamke? Ni hao viranja wa dunia? Au nini tulipewa na hao viranja wa dunia baada ya kumuweka Makinda?
mkuu taratibu, punguza munkari.
Viranja hawasemi nafasi ipi apewe mwanamke ila wana demand wanawake wapewe nafasi za juu pia,hata kama ni kwa upendeleo.
Sitetei uspika kupewa Mkinda hapana.
Anyway yale yalikuwa maoni yangu tu mkuu tusije toka nje ya mada ndio maana PM niliona anafaa Mdee kwa CDM
 
Mwingine ni Mhe. Samwel John Sitta(Mb),Waziri wa Uhusiano wa Afrika ya Mashariki...

Yeye ni Waziri wa zamani wa sheria na katiba,na pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji(TIC) na baadae kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....

Sifa zake nyingine hizi hapa chini...

- Mheshimiwa Sitta, anafaa kuwa Rais wa Jamhuri: msomi, haogopi kusimamia ukweli, anaheshimu sheria, ni mtendaji na mfuatiliaji na ni mkali sana
Willie @ NYC, USA.
 
Mkuu hapo tupo pamoja, ameonyesha angalau anuwezo wa kufanya ingawaje amebanwa na mfumo wa CCM.
Lakini vipi kama CDM ikishinda unadhani ni akina nani watatufaa kushikilia usukani wa uongozi toka CDM?

- Ushauri wangu siku zote ni kwamba Dr. Kitila na Mkulu wangu Mwanakijiji wapewe nafasi huko ya kujitayarisha kushika nafasi kubwa mbele ya safari, lakini kwa sasa level ya Uwaziri Zitto, Lissu, wanafaa sana isipokuwa ninatatizwa sana na Urais kwa waliopo sasa huko CDM na ni mawazo yangu tu!, sio lazima yawe sahihi, lakini ninatatizwa sana na kwenye Urais!

- I mean CDM hamjafanya collective serious thinking ya kumtayarisha Rais wa 2015 na sitaki kuamini kwamba mnategemea mabaki kutoka CCM, mkuu hili linanitatiza sana!, kwa sababu kwa walipo sasa CDM, CCM itashinda Urais bila tatizo sana!

Willie @ NYC, USA.
 
Nadhani mzee Malecela anafaa kuwa raisi,...kajitahidi mda mrefu sana kuutafuta
nadhani ni mda tumpe nafasi atuoneshe kwanini anahisi anafaa kuongoza Tanzania/Tanganyika
 
na kwanini tuendelee kuwa na mawazo ya kitumwa? viranja wa dunia wamushushwa kutoka mbinguni kutawala mawazo yetu au?
Nakuhakikishia hata CDM wakichukua nchi watafuata matakwa ya viranja asilimia 100.
Muulize Gadafi ndio anajua nini maana ya viranja wa dunia.
Hata hivyo yale yalikuwa maoni yangu tu mkuu
 
- Mheshimiwa Sitta, anafaa kuwa Rais wa Jamhuri: msomi, haogopi kusimamia ukweli, anaheshimu sheria, ni mtendaji na mfuatiliaji na ni mkali sana.

Willie @ NYC, USA.
Hapo umepotoka niko kwenye jimbo lake hapa anatesa wananchi na nidikteta mkubwa hapendi kupingwa hata kama amekosea pia hana mawazo endelevu hatuwezi mpa mtu nchi kwa kuangalia kwamba anajua kuangalia sheria wakati hana mawazo endelevu tukishapata katiba mpya na utawala bora tutahitaji mtu mwenye uwezo wa kimikakati ya maendeleo huyu bwana hajui hata umuhimu wa njia ya lami hajui haja ya vituo bora vya afya wala umuhimu wa viwanda nchini anachojua nikutukuzwa kama mungu na kutawala wajinga ambao hawata mhoji wala kumkosoa hapo ukichanganya na chama chake itakua kiama nimetumia maneno makali kwakua sio mtendaji kabisa
 
- Ushauri wangu siku zote ni kwamba Dr. Kitila na Mkulu wangu Mwanakijiji wapewe nafasi huko ya kujitayarisha kushika nafasi kubwa mbele ya safari, lakini kwa sasa level ya Uwaziri Zitto, Lissu, wanafaa sana isipokuwa ninatatizwa sana na Urais kwa waliopo sasa huko CDM na ni mawazo yangu tu!, sio lazima yawe sahihi, lakini ninatatizwa sana na kwenye Urais!

- I mean CDM hamjafanya collective serious thinking ya kumtayarisha Rais wa 2015 na sitaki kuamini kwamba mnategemea mabaki kutoka CCM, mkuu hili linanitatiza sana!, kwa sababu kwa walipo sasa CDM, CCM itashinda Urais bila tatizo sana!

Willie @ NYC, USA.
Mkuu be honest, unamashaka gani na DK Slaa kuwa hatufai kuwa rais wetu
 
Back
Top Bottom