SoC02 Taifa hili litajengwa na nani?

Stories of Change - 2022 Competition

zephania5

JF-Expert Member
Aug 18, 2022
232
801
Hadi lini tutaendelea kubaki chini? mpaka lini tutaendelea kushuhudia mataifa mengine yakipiga hatua ya kimaendeleleo, ikiwemo, uchumi, viwanda, sayansi na teknolojia, diplomasia, afya, elimu pamoja na usalama wa watu wake? na ilihali sisi tukiendelea kubaki pale pale! Mataifa kama China, India pamoja na Thailand.Yalikuwa na uchumi ulioweza kulinganishwa na uchumi wa Tanganyika, mnamo miaka ya 1960. Lakini leo ni mataifa yaliyoendelea, waswahili wa siku hizi huuliza''Tunakwama wapi?''.

Kuanzia ngazi ya familia hadi taifa, hali sio shwari kabisa! walioko juu huwalaumu walioko chini, na walio chini hutupa mikono ya lawama kwa walio juu yao. Vijana wanapoona mambo yanaenda mrama, huishia kulaumu wazazi wao pamoja na wakubwa wao, wakidai ni kwa nini wameshindwa kuwatengenezea njia iliyo bora ya maisha! Utasikia watoto katika famlia zao wakisemezana wao kwa wao ''Laiti! Kama baba yetu angelisoma kama Mzee Shamte, tusingeliteseka namna hii''. Wazazi nao,lawama zao ni kwa watoto wao, na wengi wao kuishia kutoa laana kwa watoto wao! wazee hukilaumu kizazi hiki cha leo, kama ni elimu inapatikana kwa urahisi,miundombinu imeboreshwa, utandawazi unaongezeka kila kunapokucha, lakini ni kwa nini, hali inaendelea kubaki ile ile siku kwa siku?.

Mababu zetu
Wapo mababu zetu, kama akina mtemi Isike, mtwa Mkwawa, chifu Mangungo, bila kumsahau Kinjekitile Ngwale na wengineo, ambao hawakupenda kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe, walijitahidi kuhakikisha wanarejesha ardhi mikononi mwao, iliyotaka kuporwa na wakoloni wa kijerumani. walisimima kwa zamu yao, na kwa namna yao.Leo ni nani atasimama, kuirejesha haki iliyopotea miongoni mwa watanzania?

Wananchi na serikali yao
Wananchi nao, lawama zao, ni juu ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,pamoja na viongozi wake, hasa pale inaposhindwa kuleta maendeleo na mabadiliko kwa taifa., kama ilivyotarajiwa! Dhana hii ikanifanya nikumbuke sera ya mheshimiwa, raisi mustaafu, Jakaya Mrisho Kikwete, katika awamu yake ya nne(2005-2015), iliyosema ''Maisha bora kwa kila mtanzania'' au tuendelee kuweka matumaini katika ule mpango wa tatu wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano, uliozinduliwa na waziri mkuu Kassimu Majaliwa, mwaka 2021, mjini Dodoma?

Baba wa taifa anatuambia nini?
Hebu tukumbuke kidogo maneno na wosia wa baba yetu wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ''Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kwa paka kufungwa kengele shingoni, tabu ni kumpata panya wa kufanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana kwa kudhani paka watajifunga au kufungana kengele'' Suala la maendeleo kwa watanzania leo linafanishwa na panya, ambao kila siku huhojiana, ni nani atakayemfunga paka kengele?

Pamoja tunaweza!
Taifa haliwezi kujengwa kwa kuendelea kuilaumu na kuipa mzigo serikali yetu ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania. Taifa haliwezi kujengwa na wasomi au wenye ujuzi na fani mbalimbali peke yao. Taifa haliwezi kujengwa na wanasiasa pamoja na viongozi wa dini peke yao. Vile vile taifa haliwezi kujengwa kwa kuendelea kutegemea misaada kutoka katika mataifa yaliyoendelea kama Marekani, Uingereza,China na Canada, au mashirika ya kifedha duniani kama IMF(International Monetary Fund) pamoja na benki ya dunia (WB).

Hili ni taifa letu sote, hakuna mgeni atakayekuja kulijenga taifa hili, ikiwa wenyeji wao wenyewe wameshindwa! na wala mtu hatajenga na mwingine akaja akakaa,muda wetu ni huu na nafasi yetu ni hii. Hata kama hatukuanza vizuri, lakini tunayo nafasi ya kumaliza vyema, tukianzia hapa tulipo. Mambo yaliyowashinda mababu zetu, wajukuu wanaweza kuyaweza!

Daima nitaendelea kumkumbuka Baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa tayari kumkabili Iddi Amini. Aliposikika kwa maneno yake, tarehe 2 Novemba 1978, aliposema '' Tunayo kazi moja tu, watanzania sasa. Ni kumpiga. Uwezo wa kumpiga tunao. Sababu ya kumpiga tunayo. Na nia ya kumpiga tunayo. Tunataka dunia ielewe hivyo, kwamba hatuna kazi nyingine...'' Leo hatuna maadui wengine wa kupigana nao, isipokuwa njaa, umasikini, ujinga, maradhi pamoja na ufisadi, wanaendelea kututawala hadi hii leo. Kila mmoja anayo nafasi katika ujenzi wa taifa hili, maana mikono mingi kazi huenda haraka, na umoja iwe ndio nguvu yetu kama vile mwili mmoja ulivyojengwa kwa viungo mbalimbali.

Mkulima na aifanye kazi yake shambani kwa umaridadi na ubora wake, na wakati serikali ikimuunga mkono kwa pembejeo bora na za kisasa, ikiwa ni pamoja na mbolea, trekta pamoja na dawa za kuulia wadudu ama magugu. Maana ndio kiinua mgongo cha taifa letu tangu jadi, na hivyo hakiwezi kubaki nyuma.

Wafanyakakazi waliojiriwa katika taasisi za kiserikali, au mashirika binafsi, bila kuwasahau waliojiajiri wenyewe kama machinga na fundi seremala, wafanye kazi zao kwa bidii na kwa ufanisi, kwa muda na nafasi walizo nazo.

Wasomi wenye fani tofauti tofauti pamoja na ujuzi mbalimbali, waliokwisha kupata taaluma zao katika shule na vyuo mbalimbali, ndani na nje ya Tanzania, watumie fani zao na taaluma zao kwa manufaa ya nchi yao, na si vinginevyo. Ikiwa ni daktari, karani,mhandisi, mwalimu, muuguzi na maafisa mbalimbali, karibuni katika ujenzi wa taifa letu!

Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali nchini pia, wanayo sehemu katika kuleta maendeleo ya taifa letu, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha maadili, amani, upendano pamoja na mshikamano, miongoni mwa waumini wao, pamoja na mwamko wa kupenda kufanya kazi, kama maandiko ya vitabu vitakatifu vinavyoelekeza kuwa, asiyefanya kazi na asile! na vile vile asiwepo mtu atakayekwepa kulipa kodi, kwa ajili ya maendeleo ya taifa lake mwenyewe, akiwa kama raia mwema.

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania nayo ina wajibu wa kuhakikisha kuwa, maendeleleo katika nyanja zote, ikiwa ni utawala bora, ulinzi na usalama kwa raia wake, utoaji wa elimu bora na yenye manufaa kwa watu wake, kuboresha miundombinu iliyozorota na kuchakaa( reli, barabara na madaraja). Vile vile serikali inapaswa kuhakikisha afya bora kwa watu wake, maana afya ni msingi wa maendeleo pia.

Ungewaambia nini! kama ingetokea Hayati Julius Kambarage Nyerere, Mheshimiwa William Mkapa pamoja Hayati John Joseph Pombe Magufuli, wangefufuka leo? Je wangesema '' hii ndio Tanzania niliyokuwa ninaitarajia''? Hakika kwa pamoja tunaweza, majirani zetu, pamoja na mataifa mbalimbali ya dunia yasije kutudharau na kutucheka, kwa kuwa tulianza kujenga, lakini tukawa hatuna nguvu za kumaliza. Je! ni nani atalijenga taifa hili? Ni mimi, wewe na yule.
 
Tanzania tunaitaji taasisi ....imara ili kujenga watu bora ....
 
Umeelewka,kama kila mtu atafanya Wajibu wake kwa bidii na maarifa dhabit,pia na kuacha kutoa lawama mbali Mbali. Hii itaeleta maendeleo kwA mtu binafsi na TAIFA kwA ujumla.
 
Ni kweli kabisa, uwajibikaji ni muhimu katika kuleta maendeleo, na kuondoa lawama zisizo za lazima pia.
 
๐ญ๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š ๐ฒ๐ž๐ญ๐ฎ ๐ฌ๐จ๐ญ๐ž
 
Back
Top Bottom