Mbowe: Nitaongoza maandamano wakati taifa likiwa kwenye maombolezo

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ametangaza kuongoza maandamano ya taifa ya amani Jijini Mwanza.

" Kwa mapenzi ya Mungu, nitaongoza maandamano ya Taifa ya Amani Jijini Mwanza, Alhamisi 15 February 2024 Taifa likiwa katika maombolezo ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Lowassa aliamini sana katika kazi na alisisitiza salaam za Hongera kwa kazi badala ya pole kwa kazi.

Tunamuenzi kwa kuendeleza maombolezo pamoja na kazi …. aliyoijaribu kwa kuungana nasi 2015, akawa Mgombea wetu wa Urais na akawa mhanga wa wizi wa kura na mifumo isiyo ya haki katika uchaguzi.
Taifa bado linalilia Katiba mpya na mifumo huru na ya haki ya Uchaguzi.

Taifa lina vilio vingi. Watawala wanapaswa kulitambua hili. Ni wajibu wetu kwa pamoja tupaze sauti zetu usiku na mchana hadi wenye mamlaka watambue hali halisi ya hisia za Umma wa Watanzania.

Maumivu yetu makubwa ni umasikini unaotesa maelfu kwa maelfu ya Watanzania kunakosababishwa na kupanda kwa viwango visivyohimilika vya gharama za maisha ikiwemo chakula, pembejeo, nauli, mgao mkubwa usioelezeka wa umeme nk

Watanzania wote tukutane Mwanza tukaandike historia." - Freeman Mbowe

Written by Mjanja M1 ✍️
Screenshot_20240214_020743_X.jpg

Chanzo: Mtandao wa X
 
Ataandamana na wajinga,

Leo anaitisha maandamano kesho anaitwa mezani anafanya mazungumzo yenye masirahi kwake kisha anatufokea.

Waliopo madarakani wahuni, waliopo nje ya madaraka wahuni vilevile.
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ametangaza kuongoza maandamano ya taifa ya amani Jijini Mwanza.

" Kwa mapenzi ya Mungu, nitaongoza maandamano ya Taifa ya Amani Jijini Mwanza, Alhamisi 15 February 2024 Taifa likiwa katika maombolezo ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Lowassa aliamini sana katika kazi na alisisitiza salaam za Hongera kwa kazi badala ya pole kwa kazi.

Tunamuenzi kwa kuendeleza maombolezo pamoja na kazi …. aliyoijaribu kwa kuungana nasi 2015, akawa Mgombea wetu wa Urais na akawa mhanga wa wizi wa kura na mifumo isiyo ya haki katika uchaguzi.
Taifa bado linalilia Katiba mpya na mifumo huru na ya haki ya Uchaguzi.

Taifa lina vilio vingi. Watawala wanapaswa kulitambua hili. Ni wajibu wetu kwa pamoja tupaze sauti zetu usiku na mchana hadi wenye mamlaka watambue hali halisi ya hisia za Umma wa Watanzania.

Maumivu yetu makubwa ni umasikini unaotesa maelfu kwa maelfu ya Watanzania kunakosababishwa na kupanda kwa viwango visivyohimilika vya gharama za maisha ikiwemo chakula, pembejeo, nauli, mgao mkubwa usioelezeka wa umeme nk

Watanzania wote tukutane Mwanza tukaandike historia." - Freeman Mbowe

Written by Mjanja M1 ✍️
haina maana na wala si muhimu 🐒

ustaarabu, heshima na kufarijiana kwenye kipindi cha majonzi na kipindi kigumu zaidi kwa wengine ndio msingi wa utu na ubinadamu 🐒

kama amechagua kupuuza majonzi ya familia ya ENL na kuamua kuchagua kuiumiza zaidi familia ya ENL kwa style hiyo, basi yote kheri....

ENL mbele sie sote nyuma yake....

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ametangaza kuongoza maandamano ya taifa ya amani Jijini Mwanza.

" Kwa mapenzi ya Mungu, nitaongoza maandamano ya Taifa ya Amani Jijini Mwanza, Alhamisi 15 February 2024 Taifa likiwa katika maombolezo ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Lowassa aliamini sana katika kazi na alisisitiza salaam za Hongera kwa kazi badala ya pole kwa kazi.

Tunamuenzi kwa kuendeleza maombolezo pamoja na kazi …. aliyoijaribu kwa kuungana nasi 2015, akawa Mgombea wetu wa Urais na akawa mhanga wa wizi wa kura na mifumo isiyo ya haki katika uchaguzi.
Taifa bado linalilia Katiba mpya na mifumo huru na ya haki ya Uchaguzi.

Taifa lina vilio vingi. Watawala wanapaswa kulitambua hili. Ni wajibu wetu kwa pamoja tupaze sauti zetu usiku na mchana hadi wenye mamlaka watambue hali halisi ya hisia za Umma wa Watanzania.

Maumivu yetu makubwa ni umasikini unaotesa maelfu kwa maelfu ya Watanzania kunakosababishwa na kupanda kwa viwango visivyohimilika vya gharama za maisha ikiwemo chakula, pembejeo, nauli, mgao mkubwa usioelezeka wa umeme nk

Watanzania wote tukutane Mwanza tukaandike historia." - Freeman Mbowe

Written by Mjanja M1
Kweli CHADEMA wanadhani Watanzania wote ni mazuzu. Yaani Lowasa aliyekuwa namba moja kwenye LIST OF SHAME katika website ya CDM leo anaitwa alipenda maendeleo ya nchi. Jamani bado tupo WaTZ wenye kumbu kumbu
 
Ubinadamu kazi sana.....
Kama nimeelewa kwa usahihi ulichokiandika, basi maneno haya chini yakamilishe mtazamo huo.

Kwamba,

...yale yalikuwa ni machozi ya mamba.

...sasa ndio utajua uchu wa fisi.

Kwamba mda wote, lengo kuu limekuwa ni kupata nguvu na madaraka tu.

Kwamba, Unyambis unyambis tu
 
Back
Top Bottom