TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia

Meditation :ni kitendo cha uzingativu wa akili kuwa sehemu moja
Faida za meditation:
1.meditation ina ongeza uwezo wa akili ikiwa inafanywa kila siku
2. Meditation ina ongeza furaha na amani ndani ya nafsi
3.pia meditation endapo ikifanywa kila siku ,inafungua natural power za mtu anaye fanyaa
4. Meditation ina saidia katika mfumo wa upumuaji
5. Meditation ina kupa uwezo wa kuongea na nafsi yako
6.meditation ujianini kuongea mbele za watu ,mfano kwenye mikutano ,siasa,nk.
7. Meditation inakupa nafasi na kuheshimu kila kitu chenye uhai

Mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya meditation
1.taafuta sehemu tulivu isiyo na makelele

2.Oga ,vaa nguo nyepesi na zisizo bana,hii inasaidia kuondoa nuwasho kwenye mwili .
3. Imani ya kuwa unaweza kufanya meditation
4. Vuta punzi ndefu na kutoa taratibu hii inakusaidia kuondoa uwoga na kuweza u bongo upate oxygen ya kutosha.
5.Kaa mfumo wa budhaa ,au lala chali,au kaa kwenye stuli hakiki haumii sehemu yoyote 5.legeza misuli na mwili kiujumla
6. Weka akili yako kwenye pumzi inayo ingia na kutoka
7. Hakikisha unafanya meditation ndani muda wa dakika 10 hadi 15
8. Hakikisha usifikilie chochote za ya punziiii
Asante mkuu, ila hapo kwenye kulala hapo utakuwa Sio Meditation hapo utakuwa unaitafuta astral projection.
Kulala ni Astra projection kukaa ndio una-meditate
 
Mkuu Pasco,

Ufunuo au kupata insight kwa mkristo kupo kwenye Biblia na mtu hahitaji kufanya meditation ili aweze kufunuliwa, bali kwa kusikia Neno kwa usahihi, kulisoma na kwa kuomba ili Roho wa Mungu amwongoze katika kulielewa na kulitenda. Neno meditation kama lilivyotumika kwenye Biblia lina maana ya kutafakari kwa makini au kwa kina kuhusu jambo fulani "to think, conteplate, devise, ponder" sometimes to "sigh or murmur", Biblia haiwaambii watu wafanye practices kama alivyoonyesha Mtambuzi.

Yesu hakufanya meditation (kwa jinsi mlivyoielezea) na wala hakuhitaji kwa sababu Yeye ni AllMighty: Omnipotence - All powerful, Omnipresence - He is not limited by time and space, He is everywhere at all times, Ominiscience - All Knowing.

Kwa mjibu wako au wengine meditation lengo lake ni kumpa mtu focus, insights na powers, Yesu ni Mungu na Nguvu, uwezo, mamlaka, insights zote zatoka kwake, na ni designer wa foci, sasa afanye meditation ili iweje? Ili nani ampe uwezo gani? He is infinite God.

Biblia inaposema mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu unadhani maana yake ni kwamba anaweza kuwa na nguvu na uwezo kama Mungu? La hasha, nguvu za Mungu hata 1 over trillion mwanadamu hana. Mungu anaposema mwanadamu ameumbwa kwa mfano wake huhusianisha zaidi na mambo ya utakatifu - kwamba mwanadamu anaweza kuendelea kubadilika na kufanana naye kwa kuwa na utakatifu au ameumbwa na asili ya utakatifu kama alivyo Mungu na atakuwa mtakatifu kamili (kwa waliookoka) siku atakaponyakuliwa na kwenda mbinguni. Kwa habari ya nguvu Mungu amesema kila leo mwanadamu uwezo wake ni very limited.

Hauhitaji kufanya meditation kama ulivyoilezea ili kuijua kweli - Neno la Mungu ni kweli, and it's very apparent. Meditation ni imani, iwapo utaigeukia hiyo na kuacha imani ya Kikristo unamtumikia mungu mwingine na sio Mungu wa Biblia. Mtu anafunuliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu kupitia Neno la Mungu.

Na kuhusu habari ya kunena kwa lugha ni ishara ambazo zilifanywa wakati mitume wanasimika Neno la Mungu (wakati wanaweka msingi). Kwa sasa hizo huduma zimesitishwa, hazipo. Kunena kwa lugha sio kelele zisizokuwa na mpangilio wenye maana au kuongea lugha ambazo haziexist kama wafanyavyo watu siku hizi, bali ni mtu asiyejua lugha fulani kupata uwezo wa kuiongea kiufasaha na pia Biblia inasema katika kanisa wanaweza kunena wawili au watatu na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Mfano mzuri ni siku ya Pentekoste, watu walinena kilugha kwa maana ya kuongea lugha ambayo hapo awali hawakuwahi kujifunza wala kuijua na watu wengine waliweza kusikia na kuelewa walichokuwa wakisema na kushangaa. Unakuta watu wanalia kanisa zima halafu milio kama ya wanyama na ndege huku hakuna mfasiri hata mmoja! Hiyo sio kunena kilugha ni drama/movie.

Mtu anapata Roho mtakatifu pale tu anapompokea Kristo. Wokovu, kupokea Roho mtakatifu, kusamehewa dhambi; vyote vinatokea concurrently.

Kuijua kweli ni kupitia Neno la Mungu na si vinginevyo. Na Neno la Mungu linasema ukiwa na Imani ndogo tu kama punje ya haradali unaweza hata kuhamisha mlima (hiyo nguvu umeiongelea)! Unaona kwamba haya mambo yanafanyika kwa imani. Sawa imani inaweza kuwa ni ya giza au mwanga kama ulivyosema.

Meditation ni "cult", ni kitu kinachooshiria imani nyingine, inahusisha alteration of mind na kucreate scenes ya mambo ambayo hayapo, badala ya kumfanya mtu ajitambue inamfanya awe convoluted kwa sababu anakuwa subjected to an environment where he/she does not fit naturally.

Meditation ni dini/imani

"Meditation has been practiced since antiquity as a component of numerous religious traditions and beliefs.[SUP][6][/SUP]" - wiki.

"The history of meditation is intimately bound up with the religious context within which it was practiced." - wiki

Kuna references nyingi including vitabu vinavyoelezea how meditation the way you have stipulated is a religion/belief system. Kama nilivyosema, meditation, scientology, wicca, spell, magic, witchcraft ni intermingled practices in the sense that they borrow from each other!

Labda juve2012 na 2013 wana mchango wao kuhusu hili
Ukomo wa akili yko umefungwa na kitabu fulan
 
Meditation (uliyoilezea wewe) ina mchanganyiko wa vitu ambavyo vingine vinaweza kukubalika kwa imani ya kikristo, mfano to calm yourself, think deeply, sit in a quite place to read a Bible or pray, kutenga muda kila siku kumeditate with the God our Father. Katika ukristo kwa kifupi meditation ni kutenga muda katika hali ya utulivu "quite time" kwa nia ya kucommunicate na Mungu kupitia maandiko, maombi au tafakari ya aina yoyote kuhusu Mungu au Neno lake. Hii ndio meditation inayoelezewa kwenye Biblia.

Lakini meditation unayoielezea Wewe na Mtambuzi inaembrace na kuborrow a lot from paganism, in that sense the whole thing ni paganism, kwa sababu Neno la Mungu halitaki mchanganyiko.

CC Pasco
Issue ya upagan imekaa kisiasa Zaid hasa siasa za tawala za ulaya ya zamani ili kumaliza mfumo wa asili wa watu kumtafuta Mungu wao., Na kileta mfumo wao kiiman ili waweze kuwatawala watu kirahisi, kwa hlo neno mpagan kwa ww mtu ulie letewa din na wazungu umeliridhi bila kujua umelaaniwa kwa kumkataa Mungu wa baba zko na kufuata miungu ya kigeni ( meditation Ni Jambo la asili kabsa na Ni njia nzuri Zaid ya kuwasiliana na Mungu )
 
Yesu hakuwahi kuanzisha dini ya Aina yeyte yesu alihibir habar njema tu ambzo pia wahndu wa waislmu na wayahudi wanahubiriwa, ukristo ulianzishwa na tawala za Rumi Kama njia ya kuitawala dunia sema tu walimtumia yesu kma kigezo Ila Nia yao Ni nyingne
 
Pasco lakini mbona husemi ni wapi pameandikwa kuwa Yesu alifanya meditation?
Yesu alimwita Mungu pale msalaban amwepushe na kikombe hicho , then apo apo wewe una amini Yesu ndio Mungu mwenyewe dah wakristo tunadharaulika kwa kukosa maarifa , kwa taarfa yako ishara ya msalaba unayochorwa kwenye paji la uso wakati wakubatizwa Inahusu maswala ya jicho la tatu , yesu aponyi mtu kabsa yesu anachafanya nikufungua nguvu ya kiungu iliyo ndan yako kwa Iman then unapona , ndo maana alipenda kusema Iman yako imekuponya , yesu aliitambua tahajudi vizur na nguvu zilizopo ndan mwetu
 
Chimbuko/historia ya tahajudi:

Neno tahajudi limetokana na neno la kiingereza linaloitwa 'meditation' likiwa na maana ya kufikiri kwa uzingativu au kwa kujali. Neno meditation, nalo limetokana na neno la kilatini linaloitwa 'meditatio' likiwa na maana ya mazoezi ya mwili na akili.

Asili ya tahajudi ni dini za mashariki. Ilianzia huko Asia zaidi ya miaka 5,000 iliyopita. Kwa sasa tahajudi hufanywa zaidi huko magharibi (Ulaya na Marekani).

Tahajudi ya miaka hii (ya wakati huu), inazungumzia zaidi tahajudi ya kiyoga ambayo asili yake ni huko India.

Kwa ujumla, tahajudi inaelezwa kama njia za uzingativu katika jambo ambalo mawazo yamelinuia. Lakini pia inaweza kuelezwa kama ifuatavyo:

=> Ni hali ya uzingativu na utulivu katika hali halisi ya wakati wa sasa hivi.

=> Ni ile hali wakati mawazo yanapokuwa yameyeyushwa na kufikia mahali ambapo hakuna fikra yenye kuingia tena.

=> Ni ile hali ambayo, uzingativu, kwa makusudi kabisa umeachwa kuelekea kwenye nguvu kubwa zaidi ( Mungu? Nguvu kuu? ).

=> Ni ile hali ya kuweka mawazo na uzingativu katika kitu kimoja, mfano- sanamu ya kidini, pumzi au neno fulani unalotamka (mantra).

=> Wengine wanaielezea tahajudi kwamba, ni sala za usiku wa manane.

CouplePraying.jpg


Tahajudi na dini:


Kila dini ina aina yake ya uzingativu, ingawa ukiutazama kwa undani utagundua kwamba ni tahajudi halisi.

Dini ya kikristo wanatumia rozari, hii huwasaidia kujenga uzingativu. Waislamu wanatumia tasbihi ambayo huwasaidia kujenga uzingativu, lakini pia huwa wanakuwa na sala za usiku wa manane (tahajudi). Wabudha huwa wanafanya tahajudi kila siku kwani ndiyo nguzo yao kuu. Wabahai, hufanya tahajudi kila baada ya sala.

Faida za tahajudi:


Ili uweze kutambua faida za tahajudi, ni muhimu kuifanya kila siku, ikiwezekana asubuhi na jioni. Tahajudi ina faida nyingi sana, faida hizi utaziona tu kama utafanya tahajudi kila siku. Hivyo, tahajudi inahitaji nguvu kubwa sana ya kujituma (wheel power). Ina faida kubwa sana, hivyo ni vizuri ukajenga mazoea ya kuifanya kila siku. Nakushauri, kama huwezi kufanya tahajudi, basi ni afadhali ujifunze upendo ingawa, ni rahisi mara kumi kufanya tahajudi kuliko kuwa na upendo. baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo:

1. Husaidia kuongeza ubora wetu kiakili, kimwili pamoja na uwezo wetu kwa ujumla. Husaidia kuuburudisha mwili, pia husaidia kupumzisha akili na mwili.

2. Husaidia kujenga uzingativu na kukuwezesha kumudu kupata suluhu ya matatizo kirahisi.

3. Husaidia kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.

4. Husaidia pumzi pamoja na kurahisisha usagwaji wa chakula mwilini.

5. Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini.

6. Husaidia kuleta furaha ya nafsi.

7. Husaidia kuimarisha nguvu yako ya machale pamoja na nguvu zako za ziada.

8. Husaidia kutibu matatizo mengi ya kisaikolojia kwani hubadili hali ya mfumo wa fahamu na mawazo (endapo itafanywa kila siku).

9. tahajudi pia inaweza kutumika kuomba kitu unachohitaji, kama vile kazi au mahitaji mbalimbali, ingawa inashauriwa uwe mwangalifu badala ya kufanya kazi unaweza ukawa mtegemezi wa tahajudi. Mfano, unaweza ukatumia tahajudi kuomba shilingi laki moja na ukapata bila kufanya kazi yoyote au kwa kufanya kazi kidogo sana ambayo hailingani na malipo ya laki moja.

Je, tahajudi huleta utajiri?


Ni swali gumu kwa sababu, utajiri ni dhana pana sana, inategemea tu unazungumzia utajiri upi, wa kitu gani na wapi. Hata ule utajiri wa kimazoea, nao bado ni mgumu kuuelezea. Mfano, tajiri wa kijijini, akihamia mjini anaonekana ni mtu wa kawaida kabisa kwani kuna matajiri wengi sana wanaomzidi.

Lakini, swali la kujiuliza ni hili, unataka utajiri ili iweje au upate nini? Kama unataka utajiri ili uwe maarufu kwa kuandikwa na magazeti, ukweli ni kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuandikwa na magazeti ingawa siyo kwa utajiri ila kwa kubaka mtoto. Lakini pia kama unataka utajiri ili ukupe furaha na amani, ukweli utabaki palepale kwamba, hata kama utaupata huo utajiri, furaha au amani haitapatikana kwani utakuwa umevunja kanuni ya maisha kwani hukuja duniani kutafuta utajiri, bali kuishi kwa kufanya kazi unayoipenda sana, inayokupa furaha na amani bila kujali maslahi, heshima au umaarufu kutoka kwenye kazi hiyo.

Kwakuwa kazi hii unaipenda, utaifanya kwa ufanisi mkubwa sana, na ndipo utajiri utakapokuja. Kanuni ya maisha kuhusu utajiri inaanza na kufanya kazi inayokupa furaha na amani na ndipo utajiri unafuata, haianzi na utajiri na ndipo furaha na amani vipatikane. Kama huamini, wachunguze matajiri unaowafahamu, ambao walipata utajiri ili uwape furaha na amani, utagundua kwamba, hawana furaha wala amani. Kwa upande wa pili wa shilingi, wale matajiri ambao, utajiri wao ulikuja kupitia kwa kufanya kazi inayowapa furaha na amani, utagundua kwamba wana furaha na amani kubwa sana.


Swali lililoulizwa hapo juu linasema, je, tahajudi huleta utajiri? Kama utajiri ni kupata furaha na amani ya nafsi, jibu ni ndiyo. Hii ni kwa sababu, tahajudi hukusaidia au kukufundisha namna bora kabisa ya kupumzisha akili na mwili na hivyo kuwa mtu mwenye furaha na amani. Kumbuka, ukishakuwa mwenye furaha na amani, wewe tayari ni tajiri wa mali pia.


Tahajudi ina madhara yoyote?

Kwa watu wenye matatizo ya kifafa, matatizo makubwa ya moyo au wenye matatizo ya akili, tahajudi inaweza kuwaumiza wasipokuwa waangalifu, ingawa kwa upande mwingine, tahajudi ni tiba/dawa kwao. Hivyo, wanashauriwa wachague tahajudi ambayo haitawaletea matatizo.

Ni vizuri wakajaribu aina tofauti tofauti ya tahajudi, halafu wakaangalia ni ipi inawasumbua na ni ipi inawapa nafuu. Wakishapata inayowapa nafuu, ni vizuri wakaendelea kuifanya mara kwa mara. Baada ya muda, watagundua kwamba, matatizo yao ya akili, moyo au kifafa yamepungua kwa kiwango kikubwa sana au yameisha kabisa.

meditation-techniques.jpg


Jinsi ya kufanya tahajudi:

Mbinu za kufanya tahajudi hutofautiana kutokana na kiwango cha uzingativu, uwezo wa kujenga taswira na namna mtu anavyoweza kukabili mawazo yanayomwingilia wakati anafanya tahajudi yake.

Baadhi ya mbinu hizi, humfanya mtu apotelee kwenye kile anachozingatia na kutoingiliwa kabisa na wazo lolote. Mbinu hizi ni rahisi mtu kujifunza mwenyewe, ingawa kuna baadhi zinahitaji awepo mwongozaji.


Hatua zinazotakiwa wakati unajiandaa kufanya tahajudi ni kama ifuatavyo:

1. Tafuta sehemu iliyotulia, isiyo na makelele. Kaa kwenye kiti au chini, au lala kitandani. Hakikisha huumii mahali popote. Legeza mwili wako pamoja na misuli yote ya mwili wako kwa kadri utakavyoweza.

2. Sahau matatizo yako yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Sahau matatizo yako ya kazini au nyumbani. Jitahidi usifikirie chochote. kama kuna mawazo yataingia, usigombane nayo, usiyape muda na nafasi, wewe endelea na kile ulichoamua kukizingatia. Hakikisha uzingativu wako ni mkubwa. Pia kione hicho unachokizingatia kwa jicho lako la ndani, kijengee taswira kana kwamba unacho tayari au kana kwamba unakiona (unacho).

3. Ni muhimu sana kujali hisia zako wakati unafanya tahajudi. Kwa mfano, kama unafanya tahajudi ya kujenga nyumba. Hakikisha hiyo nyumba unaiona ilivyo, ingia ndani ya hiyo nyumba, sebuleni, chumbani, chooni, stoo, jikoni na sehemu ya kulia chakula (dining). Kila unapoingia, onyesha hisia zako, jione una furaha ndani mwako na ikiwezekana tabasamu, pia jione una amani ndani mwako. Ukweli ni kwamba, utakapokuja kujenga hiyo nyumba, zile hisia ulizokuwa unazionyesha wakati unafanya tahajudi, zitajitokeza au utaziona. Kama tahajudi yako ulikuwa unaifanya ukiwa na huzuni, hali hiyo itajitokeza baada ya kumaliza kujenga nyumba yako. Inaweza ikatokea baada tu ya kujenga nyumba yako, ndugu zako au wa mkeo wakajaa pale nyumbani, wakawa wanafanya vurugu ambazo zitakuletea huzuni na hivyo kuanza kujuta ni kwa nini umejenga hiyo nyumba.

Ukweli ni kwamba, tatizo siyo ndugu, tatizo ni wewe mwenyewe, ni hisia zako ulizokuwa unazionyesha wakati unafanya tahajudi yako ya kujenga nyumba. Na kama wakati unafanya tahajudi yako ulikuwa na hisia za furaha, hali hiyo pia itajitokeza baada ya kumaliza nyumba yako. Hata kama ndugu wa mkeo au mumeo watajaa pale nyumbani, vicheko, tabasamu na mambo mengine ambayo yatakupa furaha yatatamalaki pale nyumbani. Kwa hiyo, hisia ni muhimu sana wakati unafanya tahajudi.


4. Pumua kwa kuingiza pumzi ya kutosha mapafuni, halafu toa pumzi yote na kufanya kifua kiwe kama kitupu. Weka mawazo yako yote kwenye pumzi zako. Vuta pumzi kwa kina kiasi ili oksijeni iingie nyingi zaidi. Unapotoa pumzi unafanya msuli wa mapafu kujisafisha bila kukwazwa. Ni muhimu kuvuta na kutoa pumzi kwa kina angalau mara tatu kabla ya kuanza kufanya tahajudi yoyote.

5. Kila siku asubuhi baada tu ya kuamka na jioni au usiku baada ya watu wote kulala (au usiku wa manane), tenga dakika kumi na tano au zaidi kwa ajili ya kufanya tahajudi. Kuna wakati utakuta mwili hautaki, lakini jenga utashi mkubwa zaidi ya mwili hadi uzoee. Ukiahidiwa safari ya bure ya kwenda ulaya kutembea na ukaambiwa ndege itaondoka saa kumi usiku, nina uhakika ikifika saa saba utakuwa macho au yamkini unaweza usilale kabisa. Lakini pia ikitokea ukaahidiwa kutiwa au kumtia kila siku saa nane mchana na umpendaye sana, nina uhakika utafika kwenye eneo saa sita au saa saba mchana, hata chakula hutakumbuka. Ninakuomba ujenge utashi wa aina hii kwenye tahajudi.

6. Ukipata muda, kama huna kazi ya kufanya, ukiwa peke yako, ofisini, nyumbani, kwenye basi/daladala, kituoni, jaribu kufanya tahajudi. Mazoezi ya tahajudi hufanyika mahali popote.

7. kama ukifanya vizuri tahajudi, utahisi nafuu fulani kimwili au kiakili ama vyote. Utagundua kwamba, mwili hasa upande wa msukumo wa damu, utakuwa na mabadiliko.


Aina za tahajudi:

1. Tahajudi ya pumzi.

Ni kongwe zaidi. Ilianzia china na India. Ni tahajudi nzuri au muhimu kwa wale wanaoanza kujifunza.

Jinsi ya kuifanya: tafuta sehemu tulivu, kaa chini,kwenye kiti au lala kitandani (chali). Hakikisha mwili wako hauumii mahali popote, legeza misuli na viungo vyako vyote vya mwili, fumba macho yako. Vuta pumzi kwa kina halafu iruhusu itoke taratibu, wakati pumzi inatoka unaweza kutaja neno 'moja' au 'one' au neno lolote ambalo ni rahisi kwako. Usitaje neno hilo kwa mdomo, litaje kwa kulifikiri (kimoyomoyo) na baada ya muda utalizoea, litakuwa linakuja lenyewe.

Faida yake: husaidia kupumzisha mwili na akili.


2. Tahajudi ya mkono:

Hii inakuonyesha ni kwa jinsi gani mawazo yako yana nguvu zaidi kuliko mwili. Lakini pia inakuonyesha uhusiano uliopo kati ya mawazo yako na mwili wako.

Jinsi ya kuifanya: kaa kwenye kiti kisichokuwa na mkono. Miguu ikanyage chini na uweke mikono yako magotini (juu ya mapaja). Fumba macho, tulia, usiwaze kitu chochote, mawazo yakija usishindane nayo, usiyape nafasi wala muda, wewe endelea kutulia.

Ukiwa katika hali ya kupumzika na kufumba macho, chagua kati ya mkono wako wa kulia au kushoto na kupeleka mawazo (ufahamu) wako hapo. Peleka ufahamu wako kwenye mkono uliouchagua (mfano wa kulia). Fahamu kuwa sasa unaufahamu mkono wako wa kulia, yaani unauona kwa macho ya mawazo yako (kumbuka mawazo yetu yana macho, yanaweza kuona kitu hata kama hakipo mbele yetu).

Kwa kutumia macho ya mawazo yako, kitazame kiganja chako cha mkono wa kulia, kifahamu kabisa jinsi kilivyo huku ukiwa umefumba macho. Halafu kwa macho ya mawazo yako, itazame damu inavyozunguka kwenye mkono na kiganja chako, endelea kukitazama kiganja cha mkono huo wa kulia, kitazame kwa mbele na nyuma (ndani na nje). Halafu itazame damu inayotiririka ndani ya kiganja hicho. Wakati unaendelea kukitazama kiganja chako kwa macho ya mawazo yako, kuna mawazo yanapita kwenye ufahamu wako na kukuondoa kwenye uzingatifu wako. Usijaribu kushindana na mawazo hayo, yaache, bali endelea kuweka nguvu yako kwenye kiganja na damu inayotiririka ndani ya kiganja. Endelea kukitazama kiganja chako tena na tena na tena. Sasa hama kwenye kiganja na kitazame kidole gumba cha mkono wako, endelea kukitazama na baada ya muda, hamisha ufahamu wako na kukiona kidole cha pili, cha tatu, cha nne na cha tano yaani cha mwisho. Baada ya hapo, hamisha mawazo yako na kutazama katikati ya paji lako la uso, ni wazi unafahamu vizuri jinsi paji lako la uso lilivyo, endelea kulitazama kwa muda. Jaribu kukadiria umbali uliopo kati ya paji lako la uso na kiganja chako.

Baada ya hapo, endelea kukitazama kiganja chako kwa ndani, ione damu inayotiririka kwenye kiganja chako, tumia muda kidogo kuiangalia. Halafu angalia kiganja chako kwa juu(nje), kione vizuri jinsi kilivyo, peleka ufahamu wako kwenye kidole gumba, kidole kinachofuata, yaani cha pili, cha tatu, cha nne na cha tano. Peleka ufahamu wako kwenye paji lako la uso, endelea na zoezi hili kama ilivyoelezwa hapo juu. Baada ya muda, kama umejenga uzingativu wa kutosha kwa kufuata maelekezo, utaona mkono wako umeanza kupanda wenyewe. Na kama utaendelea kufanya zoezi hili, mkono wako utapanda na kugusa paji lako la uso. Na kama utaendelea kufanya, mkono utashuka wenyewe baada ya kugusa paji lako la uso na kutelemka chini mpaka kwenye paja lako na ukiendelea utapanda tena na kushuka tena.

Faida yake: husaidia kupumzisha mwili na akili, husaidia kutuliza maumivu ya mwili, husaidia kujenga uzingativu, n.k.

3. Tahajudi ya mshumaa.

Jinsi ya kuifanya: Tayarisha mshumaa na kiberiti. Kaa chini au kwenye stuli. Weka mshumaa wako mbele yako kwenye stuli au kitu chochote ili mradi uwe usawa wa macho yako. Uwashe na uanze kuuangalia kwa kuukazia macho bila kupepesa kope. Ukishindwa, pepesa kidogo halafu endelea kuuangalia bila kupepesa tena. Endelea kuuangalia kwa muda usiopungua dakika 10 au 30.

Pia, unaweza kutumia moto huu wa mshumaa kuchoma mambo ambayo uliambiwa huwezi. Mfano, uliambiwa huna akili, hivyo, chukua hili neno na lichome kwenye moto huu wa mshumaa. Kama utakuwa umezingatia sana, utaona moto wa mshumaa ukiongezeka au ukibadilika rangi.


Tahadhari: wakati unachoma, usije ukachoma yale mambo mazuri uliyoambiwa.

4. Tahajudi ya mtoto wa ndani:

Hii ni kwa ajili ya kufuta mambo ambayo uliambiwa huwezi. Huwa tunasema, ongea na mtoto wako wa ndani.

Jinsi ya kufanya: kaa chini, kwenye kiti au lala kitandani (chali). Jenga taswira ya picha yako ulipokuwa mtoto. Jione mahali ulipokuwa kama ni nyumbani au shuleni. Angalia yale maeneo ambayo unayakumbuka na ambayo uliambiwa huwezi. Kila unapofanya chagua eneo moja moja ambalo unakumbuka uliambiwa hufai. Baada ya kutengeneza taswira ya mtoto huyo ambaye ni wewe, rudi kwako sasa ukiwa mtu mzima. Anza kuongea na huyo mtoto ambaye ni wewe pia. Mwambie kwamba, uliambiwa huna akili (kama uliambiwa huna akili) na wewe ukaamini kwa sababu ya utoto, lakini sasa umekua, fahamu ukweli huu kwamba wewe una akili sana sawa na mtu yoyote. Endelea kurudiarudia hayo maneno kwa muda wa dakika tano au zaidi.


Unapoongea na mtoto wako wa ndani mara kwa mara, pamoja na kukupa faida zingine za tahajudi, itakusaidia pia kukuwezesha kujiamini katika hayo maeneo ambayo uliambiwa huwezi au hufai.

5. Tahajudi ya namba:

Hapa, unatakiwa kuhesabu namba kinyumenyume huku ukiwa umefumba macho. Unaweza ukaanzia 100, 99, 98, 97, 96, mpaka 1, au unaweza kuanzia 200, 198, 196, 194, 192, mpaka 2. hakikisha wakati unahesabu namba hizi hukosei, na ikitokea ukakosea namba yoyote hata kama umekaribia kumaliza, itakulazimu kuanza upya. Tahajudi hii ni nzuri sana kwa kurejesha kumbukumbu, ingawa pia ina faida nyingine.
225px-Maharishi_Huntsville_Jan_1978A  .JPG


6. Tahajudi ya maua:


Tafuta ua la rangi nyekundu, kijani, njano au nyeupe. Hapa usifumbe macho. Liweke mbele yako na uliangalie kwa kulikazia macho bila kupepesa kope. Hakikisha mawazo, fikra na uzingativu wako wote unaupeleka kwenye ua hilo. Lakini kama una bustani ya maua, unaweza kwenda kukaa bustanini na kuanza kuyaangalia maua hayo kwa kuyakazia macho huku mawazo na uzingativu wako wote ukiwa kwenye ua ulilolichagua.

7. Tahajudi ya rangi:

Hii hutumika kwa ajili ya kujiponya kwani kila rangi inatibu magonjwa fulani kwenye mwili wako kama utaiangalia kwa muda mrefu au kama utavaa nguo ya rangi hiyo. Unaweza ukatumia tunda lenye rangi husika, mfano matunda damu au nyanya kuwakilisha rangi nyekundu.

8. Tahajudi ya sauti:

Hii inahusisha kutaja neno kimoyomoyo ambalo ukishalizoea neno hili itafika mahali huhitaji kulitaja ila utalisikia neno hilo likijitaja lenyewe. Unaruhusiwa kuchagua neno lolote ambalo ndiyo litakuwa nguzo yako ya kujenga uzingativu. Mfano, amani, mungu, furaha n.k.

9. Tahajudi ya kusogea:

Hii huhusisha kuikabili ardhi kama kitovu cha nguvu, huhusisha kusogea kwa aina fulani. Watu wengi hupenda kuifanya usiku.

10. Tahajudi ya kujikagua:

Huhusisha kujikagua baadhi ya maeneo yako ya mwili kwa kutumia macho yako ya akili.

11. Tahajudi ya ukuaji:

Ni tahajudi ambayo imefanyiwa utafiti mwingi sana wa kisayansi na kuthibitishwa kwamba, tahajudi husaidia mwili, akili na hisia, pia ni rahisi kujifunza. Katika tahajudi hii, kila mmoja hupewa neno ambalo hatakiwi kumpa mtu mwingine. Neno unalifanyia kazi ili kujenga uzingativu.

Hizi ni baadhi tu ya tahajudi ambazo huwa zinatumika mara kwa mara. Unachotakiwa ni kuwa mbunifu ili na wewe ubuni tahajudi ya kwako (za kwako) na kuzipa majina yoyote unayotaka. Kwenye maisha hasahasa katika tahajudi, hutakiwi kuwa kasuku wa kutumia tahajudi zilizobuniwa na watu wengine, fanya kila uwezalo kubuni tahajudi yako hata kama ni ndogo kiasi gani ili mradi inakusaidia kukupa uzingativu. Kumbuka kwamba, tahajudi inaweza kufanywa muda wowote na mahali popote.

Usikubali mwili ukutawale kwa kukuambia umechoka na hivyo nenda kalale. Hivi, kuna kitu kinaitwa kuchoka ambako kutakufanya ushindwe kufanya tahajudi? Kama jibu ni ndiyo, jiulize swali hili: umetoka kazini, umechoka sana na unataka kwenda kulala hata kuoga huwezi, halafu kabla hujanyanyuka kwenda kulala, ukamuona nyoka anaingia ndani je, utaendelea kulala au utanyanyuka ili umpige nyoka huyo? Bila shaka, usingizi na uchovu wote utaisha. Unaonaje kama tahajudi itachukua nafasi ya nyoka? Inawezekana! Maelezo haya yanakuonyesha kwamba, hakuna kitu kinachoitwa kuchoka ila wewe unasemaje!

3 hours of Meditation Music




Kwa leo naishi hapa, kama kuna mwenye changamoto, namkaribisha ili tupate kuelimishana.....

Meditation is somethig very very powerful. Tuchangamkie fursa tujikomboe kiakili na kimwili pia
 
Kiislam, Tahajud ni salat ya kujitolea inayoswaliwa usiku wakati pametulizana.

Tumia google utafute neno "tahajud" utaielewa maana yake Kiislam.
Ustaadhat,hii tahajudi inayofundishwa humu ki-sharia ya kiislam inaruhusiwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom