TAHADHARI: Wahafidhina wapo toka zamani, Kisa cha Abneli mwana wa Neri na Generali Yoabu

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,020
Kwanza nitoe Pongezi zangu Nyingi kwa Viongozi wa Kitaifa akiwemo Mh Rais Samia Suluhu Hassan, rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania.

Pongezi zingine ziwaendee viongozi wakuu wa vyama vya siasa Mh Freeman Mbowe na Mh Zitto Zuberi Kabwe. Bila kuwasahau na wananchi wote wenye Mapenzi Mema.

Tatu sitaweza kuwasahau pia viongozi hawa kwa upekee kabisa Askofu Emaus Mwamakula na Lecturer Dr Lwaitama kwa Nasaha zao za kila siku kuhusu Amani, umoja na haki ktk Taifa letu la Tanzania.

Hivi Karibuni niliandika kuhusu Generali mmoja wa Jeshi la Israeli anaitwa Yoabu. Huyu alikuwa kiongozi wa juu majeshi yote ya falme hiyo wakati wa Utawala wa Mfalme Daudi Kusini mwa Israeli yaani Hebroni.

Ktk makala ile ilikuwa kwa mfumo wa Swali, Je Tanzania kuna Yoabu? Pengine kutokana na uwasilishaji wangu( mimi sio mwandishi) kuna baadhi ya wasomaji hatukuelewana. Sio kosa!

Sisi wengine wenye imani nyingi za hapa na pale kila jambo huwa tunalipima na kulitazama kwa mujibu wa imani zetu. Elimu ya dini tunaitumia kama reference kwenye mazingira yetu ya sasa.

Juzi Tarehe 8 Machi Mh Rais Suluhu alihutubia Taifa akiwa kwenye Jukwaa la wanachama wa Chadema, baraza kuu la wanawake lenye heshima afrika mashariki na kati.

Ktk hotuba yake aligusia uwepo w watu conservatives yaani wenye misimamo isiyobadilika hata kwenye jambo lenye Maslahi ya Kitaifa. Hawa watu sometimes ni watu hatari. Alisema wapo CCM na Wapo Chadema.

Abneli Mwana wa Neli alikuwa ni Mkuu w Jeshi la Mfalme Sauli Yerusalem. Yeye alikuwa coordinator wa shughuli zote za ulinzi na maslahi ya ufalme wa Saul kipindi ambacho Mfalme Sauli alikuwa na migogoro ya kiutawala dhidi ya Mfalme Daudi.

Hofu ya Sauli ni kuhusu Daudi anayetaka kuchukua ufalme wa Israel yote yaani Hebroni na Yudea( Yerusalem).
Kulipiganwa vita mbali mbali kati ya Daudi na Sauli na kati ya Daudi na Wafilisti( waparestina).

Kutokana na uhasama kuwa mkubwa upande wa Sauli ulianza kushindwa kuhimili mapambano. Watu wa Sauli walikufa wengi, na wengine kubaki walemavu.

Jemedali Abneli mwana wa Neli akatumwa Mission kwenda kwa Mfalme Daudi kukaa kwa amani na kuridhiana ili suluhu ipatikane bila kuumiza wananchi wao.

Ugeni kwa upande mmoja ukiongozwa na Abneli na upande wa pili akiongozwa Mfalme Daudi Mwenyewe katika Ikulu yake.

Kitendo kile cha kufanya mazungumzo ya amani hakikumfurahisha General Yoabu. Alianza kuona Abneli anaweza kuwa Royal kwa Daudi na hivyo kuna uwezekano Abneli anaweza kuchukua nafasi ya Yoabu.

Ikawa walipomaliza maridhiano Daudi alisindikia msafara wa Abneli baadae akarudi Ikulu.

Wakati huo huo Mwanajeshi Katiri aoiyekuwa na roho mbaya kuwahi kutajwa katk Biblia Yoabu alikuwa ametoka kuongoza Vita huko Gathi kwa wafilisti na wa Amaleki.

Alipofika Ikulu akadokezwa kuwa muda mfupi uliopita Abneli alikiwa Ikulu akifanya mazungumzo na Mfalme.

Basi akapiga mbio kuwafata akina Abneli.

Kwa kuwa Abneli aliamini ni wakati wa amani na yakale yamekwisha si ndweli alisimamishwa na Yoabu akimwambia anataka wasalimiane na kukumbatiana.

2samweli 3: 24-25

Raraabii!! Abneli akaamini akamkumbatia Yoabu. Kumbe Yoabu alikuwa anaongozwa na Hila. Alikuwa ameficha kisu Mfukoni kwa nyuma. Wakati wakisalimia kwa amani Yoabu akamchoma Kisu tumboni. Abneli mwana wa Neli akafariki palepale.

Taarifa za Kifo cha Abneli zilisambaa kwa kasi sana. Nchi nzima ya Israel ikaingia kwenye majonzi makubwa. Hofu na vilio vikatawala. Nchi nzima wakafunga na kusali kwa siku Tatu wakiomboleza.

Mfalme Daudi alisikia habari zile zikamsikitisha sana. Akalia na kuomboleza mbele ya Raia wake. Hata ushindi waliopata kule Amaleki ukaingia doa.

Daudi analia mbele ya Kaburi la Abneli akisema imekuwaja Abneli umekufa kizembe hivyo? Kwani ulifungwa miguu na mikono?

Kosa la Daudi ni kusahau kukumbuka kuwa ndani ya Utawala wale kuna Wahafidhina wasiopenda utengamano. Wasiopenda amani kwa wengine. Yaani kwao bora vita na mateso kuliko umoja na mshikamano.

Yoabu alitumia vita na vurugu kujinufaisha na kupata umaarufu kwa kuwa alijua kupigana na siraha za kutosha aliweza kuzitumia vyema. Hivyo alibaki kuwa ni kipenzi cha Mfalme.

Kwa lugha nyingine nje ya vita na uhasama Yoabu alikuwa hana sifa nyingine. Hana cha kumuonesha Mfalme. Hana maana na hana kazi. Hivyo migogoro kwake ilikuwa na Advantage kubwa bila kujali Mfalme alikuwa akichukizwa na hali ile. Ilifikia hatua Yoabu akamuua Mtoto wa Daudi kwa kumchoma Mkuki moyoni na mfalme akabaki analia tu asimfanye kitu Yoabu kwa kuwa alijua bila Yoabu vita nyingi vya maaduni asingetoboa. Hivyo mfalme alibaki kufadhaika moyoni tu.

Kwa Upande wa Viongozi wetu wa Kitaifa wameligundua hilo. Ni muhimu sana kuongeza umakini dhidi ya wahafidhina wasije wakavuruga hii mipango mizuri.

Na Mwenyezi Mungu awasimamie na kuwabariki sana.

Nimesikia kuna vikao vinaendelea kwa maslahi ya Taifa. Mungu awajali mkafanikishe jambo hili mweze kuwatumikia Wana wa Mungu wa Tanzania kwa mafanikio makubwa.

Asalam Aleykum.

2Samwel3: 20-39.

Sikiliza pia video hii ya Bahati Bukuku akifanya reference ya Yoabu, Abneli, Daudi na Ithbosheti kwa upande wa Sauli.
 
Ktk clipi hii pia utajifinza busara anazotoa Mwimbaji huyu.

Wimbo huu wenye melody na Rhythm ya Reggae
" usijaribu kuua nzi aliyetua Kichwani mwa mtu kwa kutumia nyundo utamuua na kumwachia jeraha kubwa"

" kama huwezi kutumia busara basi usitumie nguvu kitatua matatizo.

Nisikuchoshe ndugu msomaji. Kazi kwako.
 
Na wako pande zote.

FqsVdVaWIAAapSB.jpg
 
Kosa kubwa ni ku define watu wahafidhina na uhafidhina ni kitu kibaya. Hata mfano uliochagua hauna mahusiano na uhafidhina labda huelewi maana yake.

Unajua hata kupinga ushoga unaonekana mhafidhina? Sasa hebu nielimishe Chadema na CCM wanatafuta maridhiano yapi? Hapo wananchi tushangilie nini?

Utawala wa CCM umesigina Katiba na kutesa wapinzani toka enzi na enzi. Kama ni mauaji ya wapinzani, kuteswa na makesi yapo kitambo! Tukisema tuweke list ya matukio mabaya hapa zipo awamu zilikuwa worse kuliko hata hiyo awamu ya tano mnayo i lebal ubaya wote.

Kama kuna watu wanapinga mwenendo wa chama ndani Chadema nawaunga mkono na kama huo ndio uhafidhina basi wawe wahafidhina extremists kabisa ili upinzani upone.

Mambo ya CCM watajua wenyewe maana wamelea kansa wenyewe na sasa kila dawa kwao wanaona ni adui. Labda unabii wa Nyerere wa upinzani wa kweli kutokea CCM utimie haraka ili tujenge Taifa lenye manufaa kwa wengi.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza nitoe Pongezi zangu Nyingi kwa Viongozi wa Kitaifa akiwemo Mh Rais Samia Suluhu Hassan, rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania.
Mkuu umetoa mfano bora kabisa na ubarikiwe, ni kweli wako watu wasiotaka amani wala utangamano wala upendo na hao ndo wanamvuruga sana mama lakini Samia na Mbowe walianza na "MUNGU" watamaliza na "MUNGU".
 
Wahafidhina wa Tz ni watu wenye sifa zifuatazo;
1. Ni watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri!
2. Ni watu wenye ukosefu wa hekima na busara vichwani (walinyimwa hekima na Mola)
3. Ni watu wenye elimu duni na wasio na hofu ya Mwenyezi Mungu hata kidogo.
4. Ni watu waoga, waongo na wanafiki kupindukia.
5. Ni washirikina!
 
Wahafidhina wasipewe nafasi maana wao wapo kwa ajili ya maslahi yao na familia zao tu na wala hawako kwa ajili ya maslahi ya Taifa !!
 
Wahafidhina wa Tz ni watu wenye sifa zifuatazo;
1. Ni watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri!
2. Ni watu wenye ukosefu wa hekima na busara vichwani (walinyimwa hekima na Mola)
3. Ni watu wenye elimu duni na wasio na hofu ya Mwenyezi Mungu hata kidogo.
4. Ni watu waoga, waongo na wanafiki kupindukia.
5. Ni washirikina!
101% Truth !! Umenena kweli kabisa kabisa !! Tena tunamuomba Mungu awateremshie laana hao watu 🙏🙏
 
Wahafidhina wa Tz ni watu wenye sifa zifuatazo;
1. Ni watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri!
2. Ni watu wenye ukosefu wa hekima na busara vichwani (walinyimwa hekima na Mola)
3. Ni watu wenye elimu duni na wasio na hofu ya Mwenyezi Mungu hata kidogo.
4. Ni watu waoga, waongo na wanafiki kupindukia.
5. Ni washirikina!
 
Bibilia Ni Neno la Mungu linaloishi.

WAKUJUE MUNGU WA PEKEE WA KWELI NA YESU KRISTU ULIYEMTUMA.
YOHANA 17:3.

Mungu akubariki kwa Reference nzuri.
 
Mkuu umetoa mfano bora kabisa na ubarikiwe, ni kweli wako watu wasiotaka amani wala utangamano wala upendo na hao ndo wanamvuruga sana mama lakini Samia na Mbowe walianza na "MUNGU" watamaliza na "MUNGU".
Ameeni na Mwenyezi Mungu awasimamie tunaamini katika Yeye atutiae nguvu.

Barikiwa sana ndugu msomaji AirMax
 
Wahafidhina wa Tz ni watu wenye sifa zifuatazo;
1. Ni watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri!
2. Ni watu wenye ukosefu wa hekima na busara vichwani (walinyimwa hekima na Mola)
3. Ni watu wenye elimu duni na wasio na hofu ya Mwenyezi Mungu hata kidogo.
4. Ni watu waoga, waongo na wanafiki kupindukia.
5. Ni washirikina!
Unaposema ni watu wenye Elimu duni mi nadhani sio kweli.

Yoabu alikuwa Kamanda aliyebobea kwenye vita aliheshimika ndani na nje ya Nchi.
Ispokuwa tu alitumia cheo chake kujimwambafai mbele ya Mfalme kwa ajili ya Favor
 
Kosa kubwa ni ku define watu wahafidhina na uhafidhina ni kitu kibaya. Hata mfano uliochagua hauna mahusiano na uhafidhina labda huelewi maana yake.
Uhafidhina sio kitu kibaya kwa maana ya lugha ya uhafidhina. Lakini kwa mazingira yetu na linavyotumika ni kuwa Mhafidhina ni mtu mbinafsi, mtu mnafiki na asiyependa kusikiliza maoni ya watu wengine. Ni mtu wa kujipenda mwenyewe na kudanya anavyotaka.

Hii ndio maana aliyomanisha Mh Rais.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom