Ni lini Wafilisti/Wapalestina walianza rasmi kutahiriwa?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,162
22,684
Salaaaam, Shalom!

Uchokozi kati ya wafilisti na Waisraeli haukuanza leo, kupata ukweli hasa wa swali la mada hapo juu, inabidi tupitie maandiko.

Pia usomapo thread hii, uwe na uwezo kutofautisha, PAGANISM, JUDAISM, ISLAM NA CHRISTIANITY.

Yakobo/Israel katika kitabu cha Mwanzo 34:1...., Tunasoma kisa cha Mwana wa Mfalme Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa Nchi, Shekemu, katika pitapita yake, anakutana na Dina binti ya Yakobo/Israeli. Akatokea kumtamani, akamtwaa akalala nae kwa nguvu akambaka na kumbikiri.

Hakuishia hapo, akaenda na kumsihi babaye akapose kwa Yakobo/Israeli ili ndoa ifungwe, Dina aolewe na Mhivi, Shekemu mwana wa Mfalme.

Israeli aliposikia habari kuwa Dina amebakwa na Shekemu Mwana wa Mfalme, akanyamaa na kuwasubiri vijana wake wakubwa warudi kutoka kazini Ili wajadili nini cha kufanya.

Mfalme Hamori, akaja nyumbani kwa Israeli/Yakobo ili kuposa na akaomba atajiwe Mahari yoyote Ili mwanae Shekemu amwoe Dina myahudi.

Baada ya kikao kufanyika, wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu kwa hila wakisema, hatuwezi kufanya neno hili, tumpe dada yetu mtu ASIYETAHIRIWA!!

Wakasema, ikiwa mnataka dada yetu, basi nanyi mtahiriwe nchi nzima ili muwe kama sisi, sisi tupe kwenu, nanyi muoe kwetu tuwe ndugu.

Shekemu na babaye, kwa upofu wa mapenzi, wakaenda na kuamrisha wanaume nchi nzima watahiriwe, Mfalme Hamori na Mwanae Shekemu wakiwemo.

Baada ya siku tatu kupita, wakiwa na maumivu ya kukatwa MAGOVI yao, wana wa Yakobo/Israeli wakachukua panga zao na kuwafyeka wanaume wote wa Nchi ile na kuiteka nchi sababu wanaume wa mji walikuwa wakiuguza vidonda vya magovi yao!

(1 Samwel 18:25)

Mapenzi upofu yanaendelea kutupa simulizi;

Kamanda, mpiganaji mahiri, konandoo, aitwaye Daudi, anatokea kumpenda Mikali binti wa Mfalme Sauli.

Sauli kusikia hivyo, akamwambia Daudi, ikiwa umempenda Binti mfalme na unataka kumwoa, Mahari yako, nenda, niletee govi 100 za Wafilisti/ Wapalestina.

Mfalme Sauli alijua Daudi akienda kutafuta magovi 100 ya Wafilisti atauwawa hivyo kumaliza Daudi kirahisi sababu alimwona kama threat kwenye utawala wake.

Mapenzi yana nguvu, Daudi asingepata magovi 100 kwa askari wake wa Kiisrael sababu Waisraeli hutahiriwa wakiwa na siku 8 tu.

Ikambidi komandoo Daudi achukue rafiki zake, na kuvamia Wafilisti na kufanikiwa kuua wafilisti 200 na kukusanya magovi 200 ambayo ndio mahari Mfalme Sauli aliyohitaji kumwoza bintiye Mikali kwa Daudi.

Swali ni je, ikiwa Wafilisti/Wapalestina walikuwa wakiitwa MAKAFIRI sababu ya KUTOKUTAHIRIWA na walikuwa waabudu miungu, waabudu baali tangu zamani,

Ni lini katika historia ilibadilika, Wafilisti wakaanza KUTAHIRIWA na kuwageuzia kibao waisraeli na kuwaona MAKAFIRI?

Wenye taarifa sahihi karibuni.🙏

Cc Faiza fox.
 
Mapenzi Yana nguvu sana, yaani uwatahiri wanaume Nchi nzima kisa umepewa masharti Ili umwoe ulompenda🙂
 
Wakasema, ikiwa mnataka dada yetu, basi nanyi mtahiriwe nchi nzima ili muwe kama sisi, sisi tupe kwenu, nanyi muoe kwetu tuwe ndugu.

Shekemu na babaye, kwa upofu wa mapenzi, wakaenda na kuamrisha wanaume nchi nzima watahiriwe, Mfalme Hamori na Mwanae Shekemu wakiwemo.
Wakabadili Katiba kwasababu ya mwanamke
 
baada ya mood kusambaza dini yake. zamani walikuwa na magovi. hata goliath wa Gaza na jeshi lake alikuwa na govi. nakumbuka Daudi alishaenda kuwauwa wengi kweli akawakata magovi yaliyojaa magunia. wawashukuru wayahudi waliwaletea ustaarabu wangekuwa na mikono ya sweta hao. na mood aliiga utamaduni toka kwa wayahudi.

Mudi mwenywe hakuwahi kutailiwa.
 

Israel sasa yashambulia makanisa baada ya kushambulia Misikiti na hospitali Ghaza​

 
Back
Top Bottom