DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
1768744331441.jpg
 
Pia ukienda sokoni kununua kuku hakikisha wanamchinja kuku ukiwa unamuona. Usikubali waende sehemu ambayo huoni. Wengi huwa wanabadilishiwa anachukuliwa kuku aliyekufa wana kata kichwa na kumyonyoa na kumkata vipande kuku aliyekufa alafu mzima wanabaki nae anarudishwa bandani .
Tena!
 
Chinjiwa, kanyonyolee nyumbani.

Hata usipobadilishiwa kibudu, wanyonyoaji hupunguza viungo vya kuku bila ridhaa yako, mf: miguu, maini/firigisi, utumbo na mkia wakati tayari ushawalipa hela ya huduma!

Wakikupimia kwamba 'huyu mzee hana shida' ndipo penye tatizo.

Na ni kweli, nimening'iniza kitambi na mkanda nje, siwezi anza kuhakiki vipande vya kuku hadharani.

Napofika nyumbani ndo'napata ripoti kwamba viungo kadha wa kadha vimeondolewa!

Dawa, nunua kuku, chinjiwa kanyonyolee home.
 
Duuh hadi hamu ya kula kuku imeisha!
Kula bila kuwaza sana mkuu.

Chakula halali ni kile unachoandaa mwenyewe, vinginevyo 'kulishanizwa' ni jambo la kawaida sana kwenye jamii zisizostaarabika zenye kuangalia faida kuliko uadilifu pamoja na ubinadamu.

Kinachotusaidi ni 'moto wa kupikia', vinginevyo life expectancy yetu ingelikuwa ni ndogo sana kama walivyo wanyama wengine.
 
Back
Top Bottom