TAHADHARI: Mnaotafuta wachumba JamiiForums

TAHADHARI: Mnaotafuta wachumba JamiiForums

Mi simlaumu MTU kwani hata mgekutana live bado yagekuwa Yale Yale ila kumbe watu wanapata familia hapa
 
WAPI NILIPOANDIKA NIMEZAA KABLA YA NDOA? UNADHANI MAMA YAKO ALIOLEWA NA BIKRA? NA ISHU YA KUZAA IMEINGIAJE HAPO? SIO KOSA LAKO UTAKUA BADO NI KIJANA WA MIAKA 25 AU 26 HUJUI UNACHOONGEA.

NAJUA UTAJIBU MATUSI MAANA NDO ZENU DESIGN HII

Achana nae my dear fuata ya muhim yasikusumbue kichwa hayo Maneno.
 
Kilichonishangaza,tume muamin huyu Dada as if anachosema ni ukweli.Tumeshindwa kumbana akaelezea madhaifu yake,hata aliyoyaeleza tumeshindwa kumnyooshea kodole.Amesema "anataka nimpapase Mimi sitaki,boxer zake naziangalia tuu",mwanamke anatakiwa kuwa hivyo?Kakiri kumtelekeza mtoto wa mwanamme saloon tumekaa kimya.Kwa maandishi yake,lugha ya matusi yeye mwenyewe anatumia sana tuu.Hapa kaja kutafuta sympathy.
 
Salaam zenu bandugu.. Naandika uzi huu ili angalau nipunguze msongo wa mawazo maana naweza kupasuka kichwa...

Mimi ni mdada nina kazi yangu nzuri tu Alhamdulihah na niko na watoto wawili (usiiulize baba yao alipo hayakuhusu) mnamo mwaka jana 2016 mwezi wa tisa hivi nilipata mkaka humuhumu JF aliyekua anatafuta mwanamke.

Tukapanga tukaonana na kwa mujibu wake akanipenda na mimi nikaona si mbaya nikaridhia mawasiliano yakawa makubwa tu. Huyu mkaka aliachana na mkewe wa ndoa ingawa bado si rasmi legally.

Ana 2 watoto na mmoja anaishi nae mwingine yupo kwa mama yake. Akanisisitiza mno nihamie kwake na wanangu ili tuishi pamoja na kusaidiana life.

Nikaona ni jambo jema maana sikua na nyumba sababu bado najikongoja mno kwenye ujenzi... Nikahamia na wanangu na watoto walimpenda kweli yani maisha yalikua murua kwakweli.

At that time, nilikua na vihela vyangu kidogo nikamsaidia kulipa ada ya wanae ya term ya kwanza takriban laki saba unusu. Na yeye nikamsaidia kumlipia ada ya open university asome Law maana alikua hapendi degree yake aliyonayo nikamlipia semester ya kwanza laki 4 na sabini.

Akaanza chuo na amefaulu first year na anatakiwa awe second year mwaka huu. Matumizi ya ndani tunashare ananipa mshahara wake ingawa mdogo lakini nina hulka ya kushukuru.

Tatizo kubwa ni kunisimanga kuhusu nyumba yake yani its too much, na pia mtoto wake hata nimpemdaje haoni anadai nambagua yani kiukweli huyu mtoto age 14 simbagui, kila nacholeta nagawa mara 3 sijawahi kumkaripia wala kumpiga wala kumgusa.

Hata yeye mtoto hana shida na mimi tatizo ni baba yake. Jana nilienda nao saluni ili mwanangu anyoe, sasa ikawa bonge la bifu eti why na yeye wa kwake sijamnyoa. Kiukweli hakua na nywele mbaya.

Akarudi jioni amelewa na kunipiga juu huku akidai mkewe alikua better kwamba ameruka mkojo amekanyaga mavi na kama vipi nihame chumba nikalale na watoto.

Huyu anataka sex mara 3 kwa siku. Usiku mara 2 na asubuhi ya saa 12 mara moja hadi huwa nachelewa job. Yani sex yenyewe haoimbi, ananivuta tu, "lete **** " anaingiza kwa lazima. Yani sex ni daily.

Akishalewa ni kunitukana kuniita ****** na mpuuzi. Jamani huyu mtu nimetoka kuchukua loan ya laki 4 kumlipia mwanae anayesema nambagua.......

Kiukweli kama ni kuingizwa chaka basi mimi ni chaka bovu. Hapa nilipo nina mimba ya miezi 3 na kwakweli moyoni nimeshamkinia....mungu anitangulie kwenye mipango yangu ya kujikomboa kutoka kwenye huu utumwa.

Tuna mwaka mmoja na miezi kama miwili tangu tuanze mahusiano last year......

Jamani kina dada na kina kaka pia msikurupuke kwenye haya mambo! Go slowly, mimi nilikurupuka sababu ya upweke niliokua nao kipindi hicho.
Aisee Pole sana Duuuu... Mapenzi Penzini
 
Mizigo msiwe mnaitua kama hiyo ukichoka bega la kulia hamishia la kushoto ili la kulia lipoe, na hilo likichoka la kushoto rudishia la kulia mpaka mtafika mwisho wa safari ya maisha yenu, maana men wote karibia wapo sawa, mechi ikisha chezwa ipo gori 2-2 hayo ndo matatizo yake tuu, yakikushinda sepa tu uyo sio maza au faza ako kuwa ndo umefika apo.
 
Tena bongo yetu hii wanawake na wanaume wapo kila kona.
Ndio cha kujiuliza,ulikoishi kooote hola, ulikosoma koooote hola, ulimosafiri mwoooote hola, ulimokula mwoooooote hola heeeeee,ulimosali/swali mwooote hola Khaaaaa wapi bado
 
POLE NA WEWE KWA KUKOSA AJIRA...NAONA SEHEMU ULIYONAYO YA KUTOLEA WATU MAPOVU NI HUMU JF...... WAPI NIMESEMA AMENIDUMP? AND WHAT DO YOU MEAN BY BEING TOO CHEAP TO FALL.... ACHANA NA KIZUNGU MAANA HUKIWEZI.

WEWE NDO UNAYEENDA KINYUME NA NATURE KWA KUTOA Makalio, MIE NIMETOA K.U.M.A NIKAZAA KAMA NATURE INAVYOHITAJI UNLESS HUELEWI MAANA YA NATURE....HALI YANGU NAPAMBANA NAYO THANK YOU VERY MUCH MDOGO WANGU
Huyu ndiyo anachukia matusi.
 
Watu walioachia awe me au ke ni wa kuwa nao tahadhali sana! Chunguza kwanza nini kilitoke kabla mtu hujajitosa
 
Kuna mtu aliwahi ongelea kuwa tuogope sana wanaume wanaotafuta wanawake mitandaoni, kama naanza kumuelewa hivi!!!
Kweli mkemwenza hata mimi nilikuwa siwaelewi kabisa
 
Back
Top Bottom