TAHADHARI: Mnaotafuta wachumba JamiiForums

TAHADHARI: Mnaotafuta wachumba JamiiForums

ayanda

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Posts
1,340
Reaction score
751
Salaam zenu bandugu.. Naandika uzi huu ili angalau nipunguze msongo wa mawazo maana naweza kupasuka kichwa...

Mimi ni mdada nina kazi yangu nzuri tu Alhamdulihah na niko na watoto wawili (usiiulize baba yao alipo hayakuhusu) mnamo mwaka jana 2016 mwezi wa tisa hivi nilipata mkaka humuhumu JF aliyekua anatafuta mwanamke.

Tukapanga tukaonana na kwa mujibu wake akanipenda na mimi nikaona si mbaya nikaridhia mawasiliano yakawa makubwa tu. Huyu mkaka aliachana na mkewe wa ndoa ingawa bado si rasmi legally.

Ana 2 watoto na mmoja anaishi nae mwingine yupo kwa mama yake. Akanisisitiza mno nihamie kwake na wanangu ili tuishi pamoja na kusaidiana life.

Nikaona ni jambo jema maana sikua na nyumba sababu bado najikongoja mno kwenye ujenzi... Nikahamia na wanangu na watoto walimpenda kweli yani maisha yalikua murua kwakweli.

At that time, nilikua na vihela vyangu kidogo nikamsaidia kulipa ada ya wanae ya term ya kwanza takriban laki saba unusu. Na yeye nikamsaidia kumlipia ada ya open university asome Law maana alikua hapendi degree yake aliyonayo nikamlipia semester ya kwanza laki 4 na sabini.

Akaanza chuo na amefaulu first year na anatakiwa awe second year mwaka huu. Matumizi ya ndani tunashare ananipa mshahara wake ingawa mdogo lakini nina hulka ya kushukuru.

Tatizo kubwa ni kunisimanga kuhusu nyumba yake yani its too much, na pia mtoto wake hata nimpemdaje haoni anadai nambagua yani kiukweli huyu mtoto age 14 simbagui, kila nacholeta nagawa mara 3 sijawahi kumkaripia wala kumpiga wala kumgusa.

Hata yeye mtoto hana shida na mimi tatizo ni baba yake. Jana nilienda nao saluni ili mwanangu anyoe, sasa ikawa bonge la bifu eti why na yeye wa kwake sijamnyoa. Kiukweli hakua na nywele mbaya.

Akarudi jioni amelewa na kunipiga juu huku akidai mkewe alikua better kwamba ameruka mkojo amekanyaga mavi na kama vipi nihame chumba nikalale na watoto.

Huyu anataka sex mara 3 kwa siku. Usiku mara 2 na asubuhi ya saa 12 mara moja hadi huwa nachelewa job. Yani sex yenyewe haoimbi, ananivuta tu, "lete **** " anaingiza kwa lazima. Yani sex ni daily.

Akishalewa ni kunitukana kuniita msenge na mpuuzi. Jamani huyu mtu nimetoka kuchukua loan ya laki 4 kumlipia mwanae anayesema nambagua.......

Kiukweli kama ni kuingizwa chaka basi mimi ni chaka bovu. Hapa nilipo nina mimba ya miezi 3 na kwakweli moyoni nimeshamkinia....mungu anitangulie kwenye mipango yangu ya kujikomboa kutoka kwenye huu utumwa.

Tuna mwaka mmoja na miezi kama miwili tangu tuanze mahusiano last year......

Jamani kina dada na kina kaka pia msikurupuke kwenye haya mambo! Go slowly, mimi nilikurupuka sababu ya upweke niliokua nao kipindi hicho.
 
Upweke mbaya sana! pole mwaya.
Tatizo liko pale pale ulishakosea kwa kutomchunguza vema kabla hujakubali kuhamia kwake au hata baada ya kuhamia kwake usingejiachia mzima mzima, ungekaa kwa akili ukichunguza kama safari ndio imefika au unatakiwa kuinua mabegi kusonga mbele. Uwiii mbaya zaidi ukafungulia mageti yote ya papuchi na mbegu zikaota... una mimba!! Dah!

Sikulaumu lakini naamini umejifunza kitu.... ningekuwa wewe ningeanza kujiwekea akiba kidogo kidogo, nisingekopa tena ili kumfurahisha..... ongea nae kuona kama atajirekebisha na mnaweza kuendelea kuwa pamoja. Kama haiwezekani anza kujipanga upyaaaa... dunduliza visenti kwa kukaba kila kona, tunza mimba yako hadi utakapojifungua na kupata nguvu utachagua moja. Kazi ni kwako!
 
Pole sana Mrembo.
Nilikuambia uje kwangu, ukagoma kwa kuwa nimepanga sijajenga. Tungekuwa wawili tungeshasimamisha yakwetu.
Sasa, umekutana na mwenye nyumba yake, masimango kila kukicha.
Nilikuambia tutajenga tu usijali, ukabisha, kumbe jamaa alikuwa anakuzuzua?

Anyway, pole sana dada.
 
Pole sana cha muhimu wewe temana nae huyo atakupotezea ramani ,cha muhimu rudisha nguvu kwenye hiyo nyumba yako usirudi tena kupanga,kubali kupoteza itakusaidia kwa future yako na watoto! Huyo ni kunguru hafugiki.
 
Upweke mbaya sana! pole mwaya.
Tatizo liko pale pale ulishakosea kwa kutomchunguza vema kabla hujakubali kuhamia kwake au hata baada ya kuhamia kwake usingejiachia mzima mzima, ungekaa kwa akili ukichunguza kama safari ndio imefika au unatakiwa kuinua mabegi kusonga mbele. Uwiii mbaya zaidi ukafungulia mageti yote ya papuchi na mbegu zikaota... una mimba!! Dah!

Sikulaumu lakini naamini umejifunza kitu.... ningekuwa wewe ningeanza kujiwekea akiba kidogo kidogo, nisingekopa tena ili kumfurahisha..... ongea nae kuona kama atajirekebisha na mnaweza kuendelea kuwa pamoja. Kama haiwezekani anza kujipanga upyaaaa... dunduliza visenti kwa kukaba kila kona, tunza mimba yako hadi utakapojifungua na kupata nguvu utachagua moja. Kazi ni kwako!

Sijutii mimba hata maana niliitaka wala sijaipata kwa bahati mbaya.. hata yeye aliitaka pia. Najipanga niwe mwenyewe nikishajifungua, pesa nitadunduliza.. kuhusu kuchukua mkopo ili kulipa ada, sikufanya ili kumfurahisha niliona ni jambo jema maana mimi ndo nina gari ilikua rahisi kupata mkopo fasta kwa kuweka gari rehani.........sijutii mtoto as the matter of fact am happy with the pregnancy, na hicho pia ni kitu kinachonishangaza maana ingekua enzi zangu nishaitoa kitambo
 
Back
Top Bottom