TAHADHARI: Kwa watumiaji wa juice za AZAM

Kuna uwezekano kuwa hivo, lakini pia wapinzani wake kibiashara wanaweza ingiza hujuma ndani ya makampuni ya Azam.

Kama kuna mfanyakazi wa azam anasoma thread hii ni vizuri afanyie kazi na siyo kupinga tu. Mimi mwenyewe nilikuwa na mke wangu nilinunua EMBE Juice kumbe zote zimeoza, sikujali maana najua admin ya kiswahili, kuna uwezekano haikuwa na preservatives sahihi, sasa ikienea sana ataingia hasara kubwa maana watu tumejenga imani kiasi fulani na bidhaa za huyu jamaa na pia nadhani ni uzalendo TANZANIAN buy TANZANIAN but not to the expense of my life

Biashara ni upinzani.
 
Kama kweli una nia njema, kwa nini hukuipeleka hiyo Juice kwa Azam ili nao waichunguze? Kumbuka kuna watengeneza bidhaa feki. Otherwise ndio yale yale ya wivu wa kike.

Wazo jema hili mdau maana sisi ni mabingwa wa kulalamika tunasahau wanaotengeneza ni binadamu pia uzembe unaweza kufanyika miongoni mwao either makusudi au bahati mbaya, kama angeipeleka maana yake wangeweza kufanya upembuzi yakinifu wa namna ya kuangalia kosa limefanyika wapi ili hatua zaidi za kuboresha zifanyike kulikoni kuishia huku mtandaoni na mbaya zaidi ID zetu si halisi tulio wengi. Haya mambo huwa yanatokea kwenye viwanda vya vinywaji iwe soda au kileo na wakati mwingine mpinzani wako anaweza kupandikiza mtu kiwandani ili achafue bidhaa yako.

Siwatetei hwa AZAM bali ni kuangalia kwa jicho lililohuru yaani wakati tunalalamika tunaangalia na upande mwingine wa shilingi wa kuwashirikisha AZAM wenyewe lakini bila kuwasahau TFDA
 
Sasa huu ni ukorofi sasa,waislam tunaingiaje??

unataka tunywe bia za mengi??sisi kwetu hiyo ni haram ndugu..

Na kwa taarifa yako,hata usipokunywa wewe,sisi tutakunywa..

AZAM anauza AFRIKA YOTE HII NA NJE YA BARA HILI SEMBUSE WEWE WA BUGURUNI KWA MNYAMANI??

Una nini la kutambia?

Mengi anakiwanda cha bia gani?
 
Kuna siku nilitembelea kiwanda kimoja cha soda, kwa jinsi nilivyoona wakiziosha zile chupa, huku wengine wamevaa ndala, bila gloves, kichwa wazi, nika apa sitakunywa tena soda za chupa.
 
Mi natoa ushauri kila m1 wetu akanunue juice ya Azam sasahivi aimimine kwenye glass kubwa aitizame kwamakini kisha turudi tuandike tumekuta nini mauchafu or mausafi.
 
Rudisha hiyo juice kwa mtengenezaji ili aweze kuthibitisha kuwa imetoka kiwandani kwake.
Watu wengine wanaweza kutengeneza bidhaa fake kwa jina la kampuni nyingine.
 
Thats is bullshit Ally Kombo,the guy is talking sense here,hiyo state of the art mashine anawazidi cocacola? Mbona tumeshashuhudia coca au beer chafu,haya mambo kwenye mass production hutokea,we mzee wa maziwa vipi?
Jamaa ana mashine latest ! State of the art ! Kama unataka Study Tour naweza kukufanyia taratibu uvitembelee !
 
Hii ni kweli kabisa!! imenitisha sana nimezipiga marufuku ndani!

Kibaya zaidi my CEO last week nae ilitokea kwake nae akazipiga marufuku!

Watoto wanazipenda sana lakini nadhani umakini wa Azam umepungua.


Hapo kwenye red ........... wanazipenda kuliko hata CERES??? Wanazipenda kuliko FRESH toka kwenye matunda
halisi ya KITANZANIA??

HEBU WAJARIBISHE ....:lalala:
 
shukrani kwa taarifa,ingawa mashtaka yako itakuwa ngumu kwako kushinda kesi kutokana na mazingira yalivyo maana juice umeifungulia kwako,huo uchafu umeuona peke yako,watakuruka mita mia kama ujuavyo wafanyabiashara wanasema kitu kikifika nyumbani hawana imani nacho sababu waweza kuta ww ndo umefanya huo uchafuzi halafu unawatupia shutuma.
u

Huyu mhanga hajafungua kesi kutaka ashinde. Angetaka angeenda mahakamani. Yeye katoa tahadhari. afya yako iko juu yako. Ukitaka hadi ashinde mahakamani ama hadi azam wakubali ama awashinde kwa kelele hilo ni lako. Mwenye ufahamu atachukua hatua za kulinda afya yake. Hulazimishwi. Wewe endelea kunywa. Wenye ufahamu wa kuoanisha taarifa hii na mazingira halisi ya tz na utendaji kazi wa tbs, atajua nini afanye.

kazi kwako.
 
uko sahihi kabisa nadhani ni baadhi tu ya bidhaa hizo zina kasoro tufike mahali kupenda bidhaa za kwetu na hasa za mzawa kama azam ambaye amesaidia sana kuongeza ajira na pesa yake inatumika hapa hapa nchinitunaona

Endeea kusema siasa za ajira wakati hata fedha unazopata kwa azam hazitshi kukutibu utakapokuwa umedhurika. Kua dogo.
 
u

Huyu mhanga hajafungua kesi kutaka ashinde. Angetaka angeenda mahakamani. Yeye katoa tahadhari. afya yako iko juu yako. Ukitaka hadi ashinde mahakamani ama hadi azam wakubali ama awashinde kwa kelele hilo ni lako. Mwenye ufahamu atachukua hatua za kulinda afya yake. Hulazimishwi. Wewe endelea kunywa. Wenye ufahamu wa kuoanisha taarifa hii na mazingira halisi ya tz na utendaji kazi wa tbs, atajua nini afanye.

kazi kwako.

wewe ndo unadandia gari kwa mbele mwenyewe kasema anahisi kashaanza kuumwa hali hiyo ikiendelea ataenda kushitaki nakushangaa unakurupuka na kulipuka bila kusoma habari kwa makini,ishia zako.
 
Thats is bullshit Ally Kombo,the guy is talking sense here,hiyo state of the art mashine anawazidi cocacola? Mbona tumeshashuhudia coca au beer chafu,haya mambo kwenye mass production hutokea,we mzee wa maziwa vipi?

Mimi sioni kwa nini watu wanabisha bila kutafiti. Usitetee wala kupinga bila sababu za msingi. Sumu zipo na uwezekano wa kunywa uchafu ama sumu kwenye azam ni mkubwa tu. Mambo mangapi tunaona TFDA wana fumble? Unaweza kuwa na uhakika mkubbwa kiaasi gani kwamba TFDA na tbs na nani sijui kwamba wao wako tofauti na vyombo vingine vya serikali kwa uzembe?

Mimi na moyo wangu na Mungu wangu ni shahidi kwamba kuna siku nilikuta nzi amekufa na katika soda ya pepsi na ndiyo ilikuwa siku yangu ya mwisho kunywa soda za pepsi na coca cola na chochote chenye mwonekano huo. Sintasahau. Leo wanataka kumburuza kijana eti kasema vibaya kwa uchafu wa azam. Mbona hata radha na texture hata rangi ya hayo madudu ya azam iko dhahiri kabisa kwamba kuna ufake kibao?

Acheni siasa za kulindana. Kubalini ukweli mlinde afya zenu.
 
Kwa mamlaka niliyopewa na katiba ya JMT nawaomba wenzangu msinunue TENA na kama mnataka juice nunueni matunda mukablendi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom