TAHADHARI: Kwa watumiaji wa juice za AZAM

Mkuu kwenye issue kama hizi ni vema ukiambatanisha na picha maana ukileta bla bla kama hizo tunahisi kwamba lengo lako ni kuvuruga biashara ya SSB,mie ni mtumiaji mzuri sana wa bidhaa zake sijawahi ona kosa au hayo mambo,weka picha tuone hayo mauchafu....[/QUOTE
MIMI ILINITOKEA DOM NIKAPOTEZEA SAS NIMESHTUKA!
 
nafikiri azam kama wamesikia wanawezakurekebisha haraka na kuboresha bidhaa zao, kwasababu actually uwepo wao umewapa wabogo wengi ajira na kipato, hata kuuza uza majuice yao na ma cola yao tu hayo wabongo wanapata kitu cha kuweka kinywani, we need to support and correct him kwa minajiri ya kumsaidia aimarike, sio kumporomosha....
 
Uliza nembo ya tbs pale inafany nn? Uhuni uhni tu ktk maisha ya watu na serikali inachekacheka. Silkiliza saiz siwez kusema nitaifanyia nn tz wakat tz haioni umhm wangu eg ajali ya moro watu kushindwa kupata msaada kwa saa 16!!!!
 
We kafiri acha fitina zako.we umekuwa tbs.kama huna hela kunywa togwa.wivu chuki vinakusumbua

mm nafikiri lugha uliotumia sio ya kiungwana, hata kama amekosea namna ya kuleta ujumbe wake. kumbuka ujumbe mmoja unaweza kufikishwa kwa namna tofauti na watu tofauti. la msingi hapa anataka kujua je wote tumepata madhara aliyopata na kama sivyo tuchukue tahadhari. ww kama gt ulipaswa kueleza kuwa hilo halijakutokea na ni mtumiaji mzuri wa juisi za azam. pili ungemshauri afanye nn ili kuondoa kasoro hiyo

kukosoa ubora wa bidhaa yoyote ni haki ya mlaji, hii haina tofauti na dawa feki za malaria zilizoingia nchini, ni wale waliolalamika ndio waliokoa maisha yetu, vinginevyo tungetumia dawa hizo na kufa bila kujua chanzo. hivyo yy anatupa tahadhari na fursa na kuongeza umakini kuangalia pale tunaponunua bidhaa hizo ili tukiona kasoro tuone nn cha kufanya

mm nashauri gt tuache tabia ya kuwa negative kwa kila kitu, hebu tujaribu kutafakari kila jambo na kushauri au kutoa maelezo yanayotosha kueleweka kwa watu wote.tujue matatizo haya yamewatokea watu wengi ila wengine wamekaa kimya sasa tutakuwa hatumsaidii Azam tusipomwambia kuwa katika kuwanda chake umakini wa kuzalisha bidhaa umepungua. hili ni jambo la kawaida katika uzalishaji, inawezekana kuna makosa yalifanyika katika eneo ya ufungashaji

kumbuka mjumbe hauawi na sio vibaya kupokea ujumbe na kuufanyia kazi ili kujua ukweli wake
 
Kwenye biashara michezo kama hii ni rahisi mtu kuifanya ili kuharibu biashara za watu, zamani sijui siku hizi kama bado upo. Watumiaji wa soda walikuwa wanakumbana na uchafu kwenye Pepsi au Coca cola! Lakini kwa hili la Azam ni vyema kama mtumiaji si wa Azam pekee bali juisi na vinywaji vingine hasa vya viwandani kagua expiring date na mambo mengine.Lakini kuacha ni juu yako ila kama sie wengine vijoti tunavipiga sana toka vimeanza na hakuna madhar
 
Nyie ndo mafala. Watu haalali wakiimalisha biashara zao wewe uko mtandaoni kumdiscourage. Huna tofauti na aloandaa mkanda wa rwakatale

Mkuu kashorobanwa,hata kama mtu anauza sumu tunyamaze kimya watu wadhurike, eti kwa sababu anaimarisha biashara YAKE? Kama tumefikia hapo basi hakuna haja ya kuwaripoti polisi majambazi maana nao wanatafuta riziki!
huu ni wakati wa Barhesa kujichunguza ama kuna wanaomhujumu au anajihujumu mwenyewe,wana JF watakumbuka uzi uliowahi kuwekwa humu kuhusu juice zake zilizopelekwa kenya zikakataliwa na KBS zikarudishwa hapa na zikauzwa madukani,nami nilifuatilia kwa waliotumia juice hizo walipata matatizo akiwemo mke wangu.
Mtoa mada amewatahadharisha wanaohitaji kujiami kama huna haja na afya yako na familia,pita zako wala hakuna sababu ya kurumbana.
 
Nyie ndo mafala. Watu haalali wakiimalisha biashara zao wewe uko mtandaoni kumdiscourage. Huna tofauti na aloandaa mkanda wa rwakatale

Ulitaka nikae kimya au nini labda?? Wewe ndo ---- namba moja kama unaona sikupaswa kuyasema niliyokutana nayo ili kulinda biashara za watu, what for??
 
Kama kweli una nia njema, kwa nini hukuipeleka hiyo Juice kwa Azam ili nao waichunguze? Kumbuka kuna watengeneza bidhaa feki. Otherwise ndio yale yale ya wivu wa kike.
Yaani niache shughuli zangu niwapelekee juice eti kisa nina nia njema? nashukuru Mungu haikunidhuru baasi.
 
We kafiri acha fitina zako.we umekuwa tbs.kama huna hela kunywa togwa.wivu chuki vinakusumbua

Neno kafiri linatoka wapi tena? Inaonesha jinsi ulivyojawa na udini? So unatumia dini kupigania ujinga, kweli ujinga ni sumu.
 
the geek had a point km mtaona inawahusu kuchukua hatua kwaajili ya afya zenu zingatieni,mkiona ni upuuzi basi ipotezeeni,sidhan km the geek ana ishu yoyote against azam,products za bahkresa hata maji ya uhai kuna kipindi yalikuwa na itirafu.
 
hizi juice bado ni janga kiasi flani nilifikir ni mikoani tu coz zinakaa mda mrefu mpaka zinamea upya zikiwa kwene friji hata hapa dar ni the same problem unakuta exp date bado bt ukiinywa ni casco.
 
Habari Watanzania na Wasio Watanzania,

Jana nilinunua juice ya Azam ya "tropical mix" ya TZS. 2500,
Nilipofika home nikamimina kwenye glass ili ninywe, nikapiga funda la kwanza nikastuka kidogo, nikapiga la pili nikakutana na radha ambayo ni ya ajabu ajabu sana yani kama uozo ulochanganyika na mafuta ya taa, nikataka nimrudishie mwenye duka ila nikaona niachane naye, nikaenda kuitupa niki-assume labda mwenye duka aliiangushia mafuta ya taa.

Leo tena nikaamua kununua juice ya AZAM sehemu ya mbali kabisa na niliponunulia jana, this time nikanunua juice aina ya "APPLE", basi mida ya usiku hivi baada ya msoc nikaamua nichukue glass moja niipige, nimefika nusu kabla haijaisha nikaiwa nimeiweka ile glass kwenye meza ambapo inapigwa na mwanga direct ndani, OMG... nimeona mauchafu uchafu kibao aisee kwenye glass, nikaanza kujiuliza au glass ni chafu??? Ikabidi nichukue glass kubwa halafu nimimine ile ile iliyopo kwenye box niione nayo, daaaaaaahhhh, aisee ni mauchafu kibao yan.

Hapa nilipo hadi nahisi nishaanza kuumwa, nimeamua kuiweka hapa ili iwe ushahidi nikiumwa walau nikashtaki. (Mungu Aniponye kwa kweli).

Nawashauri wapenzi wa hizi juice kabla hujaibugia uwe unapenda kuangalia ikoje kwanza maana waweza dhurika kwa kweli.

N.B

Sijaweka bandiko hili ili kuvuruga biashara ya AZAM, nop, ninawatahadharisha wenzangu na nilichokiandika ni ukweli mtupu.[/QUOTE) Nahisi huyu jamaa alisha RIP
 
Mkuu mimi ni moja ya watu tulioshangilia ujio wa hizi juice ili tuache kutumia za nje lakini kweli umakini wao umepungua nadhani hii ni changamoto tu kuboresha hii kitu yetu wenyewe!!

Haiwezekani ukawa ni wewe peke yako, production line ya juice yote hiyo ingekuwa mbovu na si packet yako tuu, acha upuuzi wakutumiwa na makampuni ya nje kuharibu biashara za watu
 
KIla wakati tunaandika kuhusu ubovu wa vyakula vya viwandani lakini watu hawasikii. Pole sana.
 
Aise bac azam kuna tatizo hapa mtoni mtongani kuna mtoto wa shule ya msingi kama miaka 6hv amefariki kwa kunywa juice ya azama zile nyeusi ndani,alilia asubuhi akapewa hela kaenda nunua, gafla akaanza kulia tukaona ni tatizo kufika muhimbili akawa hoisana akafariki,tukarudi nyumbani tukachukua juice walivyoipima wakasema ina kemikali hatari kwa afya,ndio imemuua,nikasema nitakwepa bidhaa zote za azam,c juice wala maji ctaki tena,KUWENI MAKINI.
Alafu mkanyamaza? Yaani watu wengine sijui wakoje!
 
Habari Watanzania na Wasio Watanzania,

Jana nilinunua juice ya Azam ya "tropical mix" ya TZS. 2500,
Nilipofika home nikamimina kwenye glass ili ninywe, nikapiga funda la kwanza nikastuka kidogo, nikapiga la pili nikakutana na radha ambayo ni ya ajabu ajabu sana yani kama uozo ulochanganyika na mafuta ya taa, nikataka nimrudishie mwenye duka ila nikaona niachane naye, nikaenda kuitupa niki-assume labda mwenye duka aliiangushia mafuta ya taa.

Leo tena nikaamua kununua juice ya AZAM sehemu ya mbali kabisa na niliponunulia jana, this time nikanunua juice aina ya "APPLE", basi mida ya usiku hivi baada ya msoc nikaamua nichukue glass moja niipige, nimefika nusu kabla haijaisha nikaiwa nimeiweka ile glass kwenye meza ambapo inapigwa na mwanga direct ndani, OMG... nimeona mauchafu uchafu kibao aisee kwenye glass, nikaanza kujiuliza au glass ni chafu??? Ikabidi nichukue glass kubwa halafu nimimine ile ile iliyopo kwenye box niione nayo, daaaaaaahhhh, aisee ni mauchafu kibao yan.

Hapa nilipo hadi nahisi nishaanza kuumwa, nimeamua kuiweka hapa ili iwe ushahidi nikiumwa walau nikashtaki. (Mungu Aniponye kwa kweli).

Nawashauri wapenzi wa hizi juice kabla hujaibugia uwe unapenda kuangalia ikoje kwanza maana waweza dhurika kwa kweli.

N.B

Sijaweka bandiko hili ili kuvuruga biashara ya AZAM, nop, ninawatahadharisha wenzangu na nilichokiandika ni ukweli mtupu.
Picha tafadhal
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom