Tahadhari kwa viongozi wa umma: Watanzania ni waoga? Nani kakudanganya. Wape platform wakuonyeshe

system hacker

JF-Expert Member
Mar 13, 2022
426
706
Hii natoa tahadhari kwa kiongozi yeyote wa Umma kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini. Msiwachukulie poa watanzania....watanzania sio kabisa. Ni wavumilivu kweli, lakini uvumilivu una mwisho. Tuishi.

Nasikia sikiaga watu wakisema watanzania ni waoga, tena sana. Kwamba, Kenya ndio watu sio waoga. Eeeehhhh?

Tema mate chini. Wape platform wakuonyeshe. Usiwanyime platform ndo utawajua vizuri zaidi watanzania ni watu gani. Kariakoo iwafumbue macho na muelewe.

Ule mkutano wa Kariakoo na Waziri Mkuu wananchi wa kawaida waliwachanachana vibaya sana viongozi wa Serikali bila kujali cheo wala umri.

Kuanzia waziri, polisi na yeyote yule alichanwachanwa vibaya sana live kwenye runinga Dunia nzima ikiona. Tena waliwasuta hasa na maneno ya shombo wakiwa live kwenye runinga. Wote wanaume kwa wanawake.


Kamuulize Mwigulu, Kijaji, TRA na polisi watakwambia. Kuna mwamba alichana hadi jukwaa la waziri mkuu mwenyewe mbele ya uso wake. Ilibidi PM aishie kucheka tu.

Wasiwasi wangu ni huu: Itakuja kutokea nyakati watanzania watapata platform huru kisiasa na katika kila eneo. My friend ogopa sana hao watu unaowadhania ni waoga. Ogopa sana.

Take care, watanzania ni watu tofauti sana na wengi wanavyowachukulia.
 
Kama una clip ya matukio mkutano wa Kariakoo tunaomba share hapa kwenye huu uzi
 
Back
Top Bottom