Tahadhari: Huu ni msimu wa nyoka!

Tahadhari: Huu ni msimu wa nyoka!

#2020
Msambazie mwenzio usibaki nayo tafadhali,,,,

Wataalamu wa hali ya hewa na wanyama/wadudu kwa pamoja wanasema huu ni wakati wa majoka hasa jamii ya swira na hongo weusi kufuatia ongezeko la joto, hivyo majoka kutafuta makimbilio majumbani

Dondoo za usalama:

1. Epuka kuacha madirisha wazi kama hayana nyavu. Majoka kama swila na hongo wanaweza kukwea vimo virefu

2. Usiache mlango mkuu wazi jioni. Majoka huingia kimya kimya na kwa upole

3. Kabla hujaketi chini ya mti kivulini kagua matawi kama kuna majoka yamening'inia

4. Kagua kitanda na mazingira yake, swira hupenda kujiingiza kwenye mashuka kujipooza

5. Acha kukaa nje kama zamani kupunga upepo kwenye matandiko. Majoka yanapenda kuwinda usiku

6. Siyo nyoka tu wanatambaa hata chatu anaweza kukumeza

7. Ondoa vichaka inayozunguka nyumba yako. Vichaka huvutia panya ambao ni chakula lishe kwa majoka

8. Nunua dawa za kufukuza nyoka mwaga kuzunguka boma, inaweza kufukuza nyoka kwa 90%

9. Ukiamua kumpiga nyoka uwe makini. Majoka yanaua. Nyoka aina ya hongo ('black mamba') akitishiwa atakukimbiza huku anakugonga. Sumu yake inaua ndani ya dakika 40.

Chukua taadhari, huu ni musimu wa majoka. Ni joto sana na majoka yanakereka na kuudhika haraka

Sambaza ujumbe huo kwa wote, ili kuokoa maisha.......
#tahadhari muhimu,,,,
#like page bonyeza hapa

Mwana Sayansi
 
...Hakika Maisha yanakwenda Kasi sana....has kwa Wadudu na Wanyama!

Kukiwa na baridi Kali na Mvua nyoka wanakimbilia Ndani kutafuta Fukuto..

Kukiwa na Jua. Na Joto Kali, Nyoka wanakimbilia ndali kutafuta Kivuli..!
Ni Hatari!
 
kUNA NYOKA MWINGINE HATARI wengi hawamjui. Ni kama mwoga ila ukimchokoza ndio asili yake hujionyesha. Green Mamba ni yule nyoka wa kijani. Sifa zake ni kama Black Mamba. Ila Wengi humuita nyoka wa kijani. Ni mpole na kama mwoga vile mana unaweza mkaribia yeye akakukimbia. Ila ukimfuatilia zaidi au akajua unataka kumdhuru ndio dhoruba yake huanzia hapo. Tabia yake inakuwa kama Black mamba.
Siyo nyoka wote wa kijani ni mamba,wale wanaokaa sehemu za mito wana kijani iliokolea siyo green mamba,halafu huna haja ya kuogopa Sana nyoka uwapo nyumbani sababu mojawapo ni kwamba nyoka akiwa kwenye sehemu yenye tiles speed yake inapungua kwa 90%,halafu nyoka wakali kama familia ya mamba(hongera) hawapendi bugudha za wanadamu,hapa unielewe kwamba jinsi makazi ya binadamu yanavyozidi kusogea katika pori nao wanazidi kuhama,halafu unaweza kuishi maeneo yenye nyoka Hawa iakuchukua miaka kuweza kuwaona sababu hata unapopita njiani anasikia kishindo cha binadamu halafu anaondoka,ukiona amefikia hatua ya kushambulia ujue ameshtukizwa,ila kwa bahati mbaya kama utakutananae uso kuwa uso ana asilimia kubwa za kukung'ata kutokana na spidi yake ya kushambulia.
 
Nilimkuta gheto... Mama ake na msaka vibaya mno. View attachment 1265438
Nishaua kama hawa wawili mwaka huu tayari, wanapenda kuingia pahala pana mitungi ya Maji, kwenye corner. Mmoja nilimpata amejiingiza bafuni, uzuri kuna tiles, si alichezea kichapo wewe 🤣 mm mwoga wa nyoka lakini nimuone karibu na home, nitamtafuta juu chini, vuruga kila sehemu, bora nimkamate, ale kichapo cha kufa mtu alafu nimwagie vidonda vyake Acid, hehe... Torture ka yote 🤣
 
Kuna yale mabuibui makubwa kama ganja la mkono
Yanaitwa great tarantula
Kama yana manyoya hivi.
Tarantula ni wadogo, na sidhani yako hizi nchi zetu. Utawapata Australia kwa wingi, na ni hatari kuruka, akifuatiwa na shemeji yake "Black widow"
Africa, yale makubwa yanayokaa kwenye dari upande wa nje ya nyumba, sidhani yana sumu, lakini nikiyaona siyapi time, choma choma, sitaki mchezo!
 
1.Angalizo msije dhani black mamba aliitwa hivyo vile mweusi la hasha wapo black mamba wa kijani.
Waliitwa hivyo sababu ufizi wao ni mweusi sio mwekundu.
2.Ni kweli mafuta ya taa na jamii za petrol ni kero kwao sana na mafuta ya samli.Ukifanikiwa kumpaka mwilini anapata hasira mno atakutafuta kukushambulia ila ukweli baadae atakufa lazima
Mahali popote penye maoil yaliyomwagika garage au petrol station uliza wameshawahi ona nyoka?
Kweli, kwenye garage hapafiki nyoka. Hapa home kila baada ya mwezi, wanamwaga oil chafu ya pikipiki au gari, kila kona ya nyumba upande wa nje, nakwambia utakawia kabla hujapishana na hao wadudu. Na ukiwaona basi bahati mbaya kapenya pahali hapajafikiwa na ile oil vizuri.
 
kUNA NYOKA MWINGINE HATARI wengi hawamjui. Ni kama mwoga ila ukimchokoza ndio asili yake hujionyesha. Green Mamba ni yule nyoka wa kijani. Sifa zake ni kama Black Mamba. Ila Wengi humuita nyoka wa kijani. Ni mpole na kama mwoga vile mana unaweza mkaribia yeye akakukimbia. Ila ukimfuatilia zaidi au akajua unataka kumdhuru ndio dhoruba yake huanzia hapo. Tabia yake inakuwa kama Black mamba.
Kule Pemba wanamuita ukukwi tuliwachezea sana kama vifaranga vya kuku.
 
Kama kakimbia nyumba kisa kitoto cha nyoka hiyo offer ya kwende kutalii snake island si atakimbia Dunia na kuhamia Mars kabisa.
Offer hiyo haiwezekani, hakuna anayekubaliwa kufika Snake Island. Wanajeshi wa Brazil wamehakikisha hivyo.
 
Wabongo bana huko Australia ,Canada na nchi zenye misitu kuna kipindi unaweza kutana na chatu kwenye sinki la choo tena ch a kukaa
Hao nyoka walioko Australia, hata chatu ukikutana naye tena afadhali sana, ile nchi ina bahati mbaya ya kuwa na kiwango kikubwa cha nyoka deadly wanaoshikilia record ya juu dunia nzima. 😂
 
Back
Top Bottom