Tahadhari ya magonjwa mlipuko msimu huu wa mvua

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,514
Habari wakuu,

Kama mjuavyo sehemu za majiji hasa Dar msimu wa mvua kuna wanaoachilia maji taka yenye mchanganyiko na maji ya chooni.

Hii ni hatari sana hasa kwa wale wanaokuwa wanakula vyakula kwenye migahawa kwakuwa usafi hakuna..

Wakati mwingine sio makosa yao ila kuna baadhi ya watu wanaachia maji machafu yanazagaa hovyo...

Unakuta migahawa mingi ipo karibu na mitaro ya maji machafu, pia maji yanasambaa sana huwezi jua yapi ni masafi au machafu.

Haya maji ya mvua yenye mchanganyiko na maji ya chooni yanapokuwa yametuama kwa muda huleta madhara.

Hivyo napenda kuwapa tahadhari baadhi ya watu ambao wanakula mitaani..

Kipindi hiko magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuhara damu, ndio hutokea.

Tuwakumbuke kuwaonya na watoto wetu huko mitaani ambao baadhi yao nao wanakula vitafunwa mbalimbali.

Tahadhari kabla ya hatari
 
Back
Top Bottom