Tafakar:Mbwembwe na ufahari mazishini kwa nini?

Tafakar:Mbwembwe na ufahari mazishini kwa nini?

mathabane

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
2,405
Reaction score
1,900
Wadau hebu tushiriki tafakari hii kwa busara zetu. Kwa upande wangu siafiki hili suala la kutumia mamilioni ya shilingi kwa mazishi pasipo sababu pevu. Mathalan, marehemu ananunuliwa jeneza la dhahabu, fedha au anazikwa na vito vya thamani. Mfano hai ni pale ilipotangazwa gharama za mamilion kwa ajili ya mazishi ya mfanyabiashara mmoja kule kanda ya kaskazini. Eti jeneza la mamilioni, hizo mbwembwe zinamwongezea nini marehemu? Bajeti ya mazishi kuandikwa kwenye vyombo vya habari mantiki yake ni nini? Maisha mbwembwe, mazishi mbwembwe, vpi huko mwisho wa safari? Mathalani, sioni mantiki ya jenezd lenye madoido sijui rimoti, kiyoyozi,feni na mbwembwe nyinginezo. Tufahamu kuwa aliye kwenye jeneza la mabanzi na aliye kwenye jeneza la dhahabu wote hadhi yao ni moja, hakuna mwenye pumzi, wote wamelala na wasijue habari ya dunia.
 
Huna hela tu ndo maana unasema mbwembwe, na kuna unavyovifanya wewe na familia yako wasio na hela kama wewe nao wanasema mbwembwe. Tulia, zisake na wewe ufnye mbwembwe. Kuna jamaa kijijini kwetu alikuwa anasema eti akina fulani wamefiwa wameenda kukodi viti kwenye msiba viti vya nini watu si watakaa kwenye magome au chini kwani kwenye msiba kuna unadhifu? sasa ndo wewe
 
Upuuzi mtupu. Anyway wanaojiita wanapolo wa huko mmererani hawajaenda shule, wala msishange. Hamkumbuki yule aliyepanda gorofani akawa anarusha fedha chini watu wagombanie? Siku hizi yu wapi?
 
Nadhani inategemea huyo mtu anatoka kwenye jamii gani na ile jamii anayotoka wanamheshimu vipi ndugu marehemu hayati. Saa nyingine unakuta misiba inachukuliwa na jamii husika hata familia wanaambiwa waache kununua vitu kama jeneza na kadhalika. Itategemea marehemu kipindi cha uhai wake aliainisha azikweje atakapokufa.
Kinyume cha hapo ni mbwe mbwe tu ambazo zinaishia kaburini.
 
Kaka usipate shida hizo mbwembwe zote mwisho wake si zaidi ya urefu wa kaburi alilozikwa mambo yoote yanaanzia mbele ya kiti cha hukumu je ataweza kusimama?
 
Wivu tu na umaskini ndio umewatawala.
Kama pesa ni za kwake kwa nini asizitumie.
 
Huna hela tu ndo maana unasema mbwembwe, na kuna unavyovifanya wewe na familia yako wasio na hela kama wewe nao wanasema mbwembwe. Tulia, zisake na wewe ufnye mbwembwe. Kuna jamaa kijijini kwetu alikuwa anasema eti akina fulani wamefiwa wameenda kukodi viti kwenye msiba viti vya nini watu si watakaa kwenye magome au chini kwani kwenye msiba kuna unadhifu? sasa ndo wewe
Kwanini pesa hzo zisitumike kumpa uhai japo sekunde tu? Unafikiri ukimzika kwa jeneza la dhahabu hadhi yake itabadilika au akushukuru? Hii inaonyesha ufupi wa upeo wenu. Sitashangaa kuskia watu kama myinyi mkimzika marehemu na tv au kiyoyozi ili aendelee kuburudika.
 
Kama kweli watu wanafahamu kifo ni nini hiyo fedha ingesaidia yatima kama haikuwa na kazi nyingine. Hii ni kufuru. Utadhani marehemu aahifadhiwa ili afufuke akiwa msafi. Ukweli.ni kwamba tangu siku ile alipofariki Mungu aliiweka roho yake inapostahili. Hicho watu wanachokililia na kuhangaikia sana ni udongo tu. Mungu tufundishe kuzihesabu siku zetu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wivu tu na umaskini ndio umewatawala.
Kama pesa ni za kwake kwa nini asizitumie.

Nyie msio na wivu na msio masikini kwanini msifanye mchango wa pesa ili Mungu amrudishe kwenu?
 
sasa maMbo ya Mungu na kuzikwa wapi na wapi?
hata kwenye maisha ya kawaida hatufanani hata kidogo
Your dream is another man's reality
kama hukujudge jinsi anaishi iweje ujudge anavyozikwa?mambo ya Mungu na jinsi amekufa hayo muachie yeye na Mungu wake
huwezi kufananisha jinsi mtanzania wa kawaida anavyoishi na lets say,Oprah na ndo hivyo hivyo hutaweza kufananisha watakavyozikwa
wengine wanafikia hatua ya kusema hizo hela wangetumia watu wasiokuwa nazo(seriously)hela mtu atafute kwa jasho lake ummpangie jinsi anatumia na hapo hapo ukute yeye ndo anasaidia watu kuzidi hata wewe unayepokea laki tano kwa mwezi wakati hujawahi hata kumsaidia ndugu yako na elfu kumi tu au mtoto yatima?
ndo maana matajiri wnazidi kubarikiwaoff topic)
kama ambavyo kwa udongo utarudi kwa udongo lakini jinsi ya kurudi kwenye udongo kila mtu ana njia yake.
stop judging!
 
Utandawazi ndio matokeo yake haya,tutegemee mengi zaidi siku zinavyozidi...mbona zaman watu hawakua na mabendi wala kushonesha sare ama mbwembwe nyiiingi kama sasa ktk misiba..
 
Nyie msio na wivu na msio masikini kwanini msifanye mchango wa pesa ili Mungu amrudishe kwenu?

Kwa kuwa si ndugu yangu, ila angekuwa ana undugu na mimi, walah nakwambia familia yetu ingemrudisha.
Nyie ndio wale mnaoombea wagonjwa wafe ili mrithi mali.
Tafuta kwa jasho.
Btw Usipanic mkuu kwa maana umasikini umeutaka mwenyewe.

Kuzaliwa Maskini ni kudra za Mungu, lakini kufa Maskini ni Ujinga na upumbavu wako wewe mwenyewe.
 
Acha ulofa wewe, kwenu hamna makaburi? umewafufua wangapi ndugu zako? Fikiria kwanza. Kwa thread yako hii tu tayari umeudhihirishia umma upeo wako dhaifu. I'm westing my tie arguing w't u.
 
Back
Top Bottom