Tafakar:Mbwembwe na ufahari mazishini kwa nini?

Tafakar:Mbwembwe na ufahari mazishini kwa nini?

Mimi siafiki matumizi ya namna hiyo nimeona marehemu anazikwa na saa ya gold huko itamsaidia namna gani ataenda nayo mbinguni??wanadamu tutafakari.

Sasa aachiwe nani hiyo saa?utakuta alisema nizikeni na saa yangu,kisa dhahabu watu wanapinga na kuitolea macho.
Jamani sote tumezaliwa,kila mtu asake pesa sio kutolea macho mali za marehemu.
 
Marehemu kaacha fedha nyingi sana ambazo hana faida nazo tena hapa duniani kwani hayupo hivyo ni bora zitumike kwa mazishi yake!! Mi binafsi siioni tatizo si ni fedha yake na ya marafiki zake!!
Wadau hebu tushiriki tafakari hii kwa busara zetu. Kwa upande wangu siafiki hili suala la kutumia mamilioni ya shilingi kwa mazishi pasipo sababu pevu. Mathalan, marehemu ananunuliwa jeneza la dhahabu, fedha au anazikwa na vito vya thamani. Mfano hai ni pale ilipotangazwa gharama za mamilion kwa ajili ya mazishi ya mfanyabiashara mmoja kule kanda ya kaskazini. Eti jeneza la mamilioni, hizo mbwembwe zinamwongezea nini marehemu? Bajeti ya mazishi kuandikwa kwenye vyombo vya habari mantiki yake ni nini? Maisha mbwembwe, mazishi mbwembwe, vpi huko mwisho wa safari? Mathalani, sioni mantiki ya jenezd lenye madoido sijui rimoti, kiyoyozi,feni na mbwembwe nyinginezo. Tufahamu kuwa aliye kwenye jeneza la mabanzi na aliye kwenye jeneza la dhahabu wote hadhi yao ni moja, hakuna mwenye pumzi, wote wamelala na wasijue habari ya dunia.
 
Very TRUE!!!
sasa maMbo ya Mungu na kuzikwa wapi na wapi?
hata kwenye maisha ya kawaida hatufanani hata kidogo
Your dream is another man's reality
kama hukujudge jinsi anaishi iweje ujudge anavyozikwa?mambo ya Mungu na jinsi amekufa hayo muachie yeye na Mungu wake
huwezi kufananisha jinsi mtanzania wa kawaida anavyoishi na lets say,Oprah na ndo hivyo hivyo hutaweza kufananisha watakavyozikwa
wengine wanafikia hatua ya kusema hizo hela wangetumia watu wasiokuwa nazo(seriously)hela mtu atafute kwa jasho lake ummpangie jinsi anatumia na hapo hapo ukute yeye ndo anasaidia watu kuzidi hata wewe unayepokea laki tano kwa mwezi wakati hujawahi hata kumsaidia ndugu yako na elfu kumi tu au mtoto yatima?
ndo maana matajiri wnazidi kubarikiwaoff topic)
kama ambavyo kwa udongo utarudi kwa udongo lakini jinsi ya kurudi kwenye udongo kila mtu ana njia yake.
stop judging!
 
Madame B umeongea!!! Ni kweli kabisa, kufa maskini mtu hujitakia. Ukichapa kazi sana hakika utafanikiwa tu. Matajiri wengi wametoka familia masikini kupindukia.
Kwa kuwa si ndugu yangu, ila angekuwa ana undugu na mimi, walah nakwambia familia yetu ingemrudisha.
Nyie ndio wale mnaoombea wagonjwa wafe ili mrithi mali.
Tafuta kwa jasho.
Btw Usipanic mkuu kwa maana umasikini umeutaka mwenyewe.

Kuzaliwa Maskini ni kudra za Mungu, lakini kufa Maskini ni Ujinga na upumbavu wako wewe mwenyewe.
 
Wivu tu na umaskini ndio umewatawala.
Kama pesa ni za kwake kwa nini asizitumie.
As long as fedha ni zake tatizo likowapi?....matumizi ya fedha ni very subjective!watu wana vipaumbele vyao kulingana na vipato....kuna wengine basic stuff kama chakula ni ishu while wengineku- spend millions kwenda kutalii anga za mbali kama yule milionea wa Urusi aliyetumia USD 20 million sio ishu.
 
Sasa aachiwe nani hiyo saa?utakuta alisema nizikeni na saa yangu,kisa dhahabu watu wanapinga na kuitolea macho.
Jamani sote tumezaliwa,kila mtu asake pesa sio kutolea macho mali za marehemu.
Waafrika tuna matatizo sana...imefikia mahali sasa ukitaka uchukiwe sana uwe tajiri!They will hate you,you cars,your cat and even your dog!
 
Huna hela tu ndo maana unasema mbwembwe, na kuna unavyovifanya wewe na familia yako wasio na hela kama wewe nao wanasema mbwembwe. Tulia, zisake na wewe ufnye mbwembwe. Kuna jamaa kijijini kwetu alikuwa anasema eti akina fulani wamefiwa wameenda kukodi viti kwenye msiba viti vya nini watu si watakaa kwenye magome au chini kwani kwenye msiba kuna unadhifu? sasa ndo wewe

Kweli bana umasikini unamsumbuwa tu! Sikuhizi wenzake wanachapisha tisheti, wanapeleka hadi Bango!
Kwenye misiba yake anaweza hadi asipike chakula eti anasa!
 
Nie kinawauma nini, hela si nizao, acheni wafu wazike wafu wenzao
 
Madame B umeongea!!! Ni kweli kabisa, kufa maskini mtu hujitakia. Ukichapa kazi sana hakika utafanikiwa tu. Matajiri wengi wametoka familia masikini kupindukia.

Ndio mkuu.
Watu hawataki kuukubali ukweli.
Ila ndio hvo.
Waache wivu wa kijinga.
Mali za kwake.
Kazitafuta kwa jasho lake hvo ni haki yake kuitumia aitakavyo.
 
As long as fedha ni zake tatizo likowapi?....matumizi ya fedha ni very subjective!watu wana vipaumbele vyao kulingana na vipato....kuna wengine basic stuff kama chakula ni ishu while wengineku- spend millions kwenda kutalii anga za mbali kama yule milionea wa Urusi aliyetumia USD 20 million sio ishu.

Kweli umenena.
Ila hao ambao wanaowasema, kumbuka walivuja sana jasho katika kuzitafuta.
Afu jitu litoke tu huko lije kula hela yake, akiulizwa eti thawabu...
 
Watoto wa mama wa kambo!!!!! ngoja niiweke sawa hii.... Watoto wa Hajira kijakazi wa Ibrahim!!!! Sio wa ndoa kama Sarah!!!! Bastard children!!!!!
 
Halafu wanaona gere!!! Watafute na wao halafu tuje tuwazike kwa mbwembwe!!!
Ndio mkuu.
Watu hawataki kuukubali ukweli.
Ila ndio hvo.
Waache wivu wa kijinga.
Mali za kwake.
Kazitafuta kwa jasho lake hvo ni haki yake kuitumia aitakavyo.
 
Hacha usengerema wewe, uislamu ni dini inayojitoshereza na kila kitu kimeshawekewa utaratibu wake hakuna fursa ya kujitungiatungia upuuzi, mazishi atakayozikwa Bakhresa, mfalme wa saudia na muislamu yeyote fukara kabisa ni yale yale, mbwembwe zitaishia nje tu ndani ya kaburi wote watalala wakiwa na sanda, ubao na majani hakuna cha dhahabu, rimoti wala kiyoyozi. Kama unaamini hata Bhakhresa atazikwa hivyo kwa kuwa ni masikini wa kiislamu haya.
Usitoke nje ya mada.
Na usipindishe ukweli.
Ina mana mayatima wako vituoni ili kuzisubiri pesa za Marehemu waliovuja jasho katika kuzitafuta?
Ashhhh....!!!
Mke,ndugu,jamaa,akina anko nk wamejaa tele, acha waile pesa yake.
Unaacha kufanya kazi ukitegemea utapata mgao wa pesa ya Marehemu, jamani!
Ukiulizwa, eti ohh aende peponi....Peponi huko, ...wote wakienda Peponi na Motoni aende nani?

Hapo kwa Red nashukuru kwa kulitambua hilo.
Hiyo ndio hali halisi.
 
Hacha usengerema wewe, uislamu ni dini inayojitoshereza na kila kitu kimeshawekewa utaratibu wake hakuna fursa ya kujitungiatungia upuuzi, mazishi atakayozikwa Bakhresa, mfalme wa saudia na muislamu yeyote fukara kabisa ni yale yale, mbwembwe zitaishia nje tu ndani ya kaburi wote watalala wakiwa na sanda, ubao na majani hakuna cha dhahabu, rimoti wala kiyoyozi. Kama unaamini hata Bhakhresa atazikwa hivyo kwa kuwa ni masikini wa kiislamu haya.

Heheheee....
Ukisikia Paaa!!!, jua mtu kachanika kund.u.
Pilipili usiyoila yakuwashiani wewe Msengerema obwato?
Unataka kuleta ushindani wa kidini na mimi?
Nani kaongelea suala hilo au ugumu wa maisha unaanza kukunyemelea?
Usikurupuke na njaa zako toka huko uje kunifia mie hapa!
Hebu nipishe mie..!!!

Kwanza hata kinachojadiliwa hukijui...kakojoe ukalale.
 
Last edited by a moderator:
Kwani akina Bill Gates watoavyo misaada Africa hizo pesa ni zenu? Sasa mwataka nani asaidie yatima? Kabla hujafa, agiza pesa zako zipelekwe kwa wahitaji. Toa kwa yatima, toa kwa wazee, toa kwa wajane. Wengine wanataka uwavushe hatua moja tu ili waweze kusimama wenyewe. Ni heri kutoa sadaka, kuliko kuzikwa na mali zitakazooza huku watoto wakifa kabla ya muda wao kwa sababu ya njaa na magonjwa.
 
pesa ndo yenye thamani hayo mambao na accesories nyingine sio issue sana

kama angefukiwa na noti chini hapo ni habari nyngine.....ila kama alimpa muuza majeneza bac hakuna shida hata muuza majeneza pia anaweza kusaidia maskini pia

ndo matumizi ya pesa hayo ndugu yangu....ZICHANGE!
 
Back
Top Bottom