wacha majelous wewe
Wadau hebu tushiriki tafakari hii kwa busara zetu. Kwa upande wangu siafiki hili suala la kutumia mamilioni ya shilingi kwa mazishi pasipo sababu pevu. Mathalan, marehemu ananunuliwa jeneza la dhahabu, fedha au anazikwa na vito vya thamani. Mfano hai ni pale ilipotangazwa gharama za mamilion kwa ajili ya mazishi ya mfanyabiashara mmoja kule kanda ya kaskazini. Eti jeneza la mamilioni, hizo mbwembwe zinamwongezea nini marehemu? Bajeti ya mazishi kuandikwa kwenye vyombo vya habari mantiki yake ni nini? Maisha mbwembwe, mazishi mbwembwe, vpi huko mwisho wa safari? Mathalani, sioni mantiki ya jenezd lenye madoido sijui rimoti, kiyoyozi,feni na mbwembwe nyinginezo. Tufahamu kuwa aliye kwenye jeneza la mabanzi na aliye kwenye jeneza la dhahabu wote hadhi yao ni moja, hakuna mwenye pumzi, wote wamelala na wasijue habari ya dunia.
wivu tu na umaskini ndio umewatawala.
Kama pesa ni za kwake kwa nini asizitumie.

Kwanini pesa hzo zisitumike kumpa uhai japo sekunde tu? Unafikiri ukimzika kwa jeneza la dhahabu hadhi yake itabadilika au akushukuru? Hii inaonyesha ufupi wa upeo wenu. Sitashangaa kuskia watu kama myinyi mkimzika marehemu na tv au kiyoyozi ili aendelee kuburudika.
Nyie msio na wivu na msio masikini kwanini msifanye mchango wa pesa ili Mungu amrudishe kwenu?
anazitumiaje na wakati ameshakufa, huo sio wivu bali ni kufuru, na kufanya jambo lolote la kufuru linamwondolea nafasi ya kuingia peponi. Unadhani waislamu wote duniani ni masikini na matajiri ni wakristo tu?
Naunga mkono hoja hiyo ni mbwembwe haina ulazima sana, tumia jeneza la kawaida tu pesa aliyoiacha marehemu isaidie wajane na mayatima ili ulale kwa amani ( rest in peace)
wacha majelous wewe
Kaburi halihitaji mbwembwe!!